Msonde maagizo yako yanaipoteza elimu

Msonde maagizo yako yanaipoteza elimu

Twende mbele turudi nyums.

Msonde ni mtu kazi na ni mtu wa mabadiriko,nazani wote tumeona alichokifanya baraza,baraza lina oparate kama jeshi kiyfupi lipo smart.

Sasa huko tamisemi anataka mambo ya kale yaishe,japo kuna vitu hajazingatia ila sekta ya elimu na mifumo lazima ibadirike tuache kulia lia.

Sasa hapo mnaongelea likizo,likizo watumish ipo ya siku 28 kwa mwaka,likizo zingine ni za wanafunzi,kama kuna kazi za kufanyika mashulen bila wanafunzi kuwepo zifanyike,hiyo mifumo ishughulikiwe.

Jambo ambalo napingana nae ni hilo la watoto kurudia orientation course,kwa muda upi uliopo?je topic zitamalizwa lini?

Pia watoto wasilazimishwe shule na ufaulu usilazimishwe
Tatizo wanataka mgeuza mwalimu awe mungu Yani hata mtoto mwenye uelewa mdogo awe na uelewa mkubwa Yani mtoto wanapasisha kimagumashi uko akifika sekondari wanataka apate arama B somo la hesabu wakati ufauru wake uelewa wake magumashi
 
Kwa ufupi tu msonde tangu ufike Tamisemi umekuwa na Mambo mengi Sana ambayo mengine hayana ufanisi ebu yapunguze, kutokana na karenda kuanzia tarehe 31/03/2023 ni likizo Ila kutokana na maagizo yako ya ajaubu ajabu likizo imekuwa Kama kiini macho shule zinaendelea na kazi wanafunzi na walimu wanakiwa kuwepo shuleni eti KPI huu ujinga mmeutoa wapi Yani umeleta mambo mengi mpaka sasa uko mashuleni baada ya walimu kufundisha walimu wamekuwa bize na kuandaa documents tu maana unamini katika tarifa siyo ufundishaji hivi nani akwambia andalio la somo likiwepo mtoto ndio ataelewa Yani mmekalia uzamani zamani pasipo kuangalia dunia inataka nini

Na nyie watu wa vetting huwa mnakwama wapi mtu Kama alikuwa mwalimu shule ya msingi uko msimpe madaraka ya kusimamia vitu vikubwa hawa watu huwa wanaalibiwa na elimu yao ya cheti hata apate udokta bado atakuwa na mambo akili ile ile ya kidato Cha nne ndio haya msonde anayofanya Kama mnabisha subilieni natokea ya kidato Cha nne na darasa la saba na darasa la nne mwakani uyu msonde kaja na vitu vya hivyo hivyo katika elimu

Hivi mwalimu unasainishaje mkabata mpya eti wa kufaurisha wakati uyu mwalimu tayali ni mwajiriwa na anamkataba wa kudumu wa ajira yake na serikali Ila leo unageuza walimu watoto eti saini huu mkataba usipofaurisha upandi daraja huu si utoto Yani mkataba mama unasema hivi wewe inakuja na vitu vya ajabu ajabu ebu acheni huo utoto

Kama idara zenu zinapesa za kuzungukia mashule kukagua vitu vya ajabu ajabu nashauri hizo pesa endelezeni michezo
Nchi hii kadiri watu wanavyoelimika ndiyo wanazidi kuwa wajinga.
 
Msonde anazingua Yani maagizo kila siku Sasa hivi shule kila siku ukaguzi ajabu wanaokuja kukagua wanakagua vitu vile vile

Anakuja afisa elimu na watu wake leo, wanakagua, kesho wanakuja sijui ukaguzi nini wanawakagua, siku inayofuata anakuja afisa elimu kata anakagua Yani wote hao wanakagua jambo lile, arafu wakimaliza wanaitana kikao kujadili Yale Yale , wasainishana POSHO wanaondoka next week Tena wanakuja Yani ni ujinga ujinga ujinga tu wizi mtupo katika pesa ya umma mafisa wapo busy na ukaguzi wa Jambo moja kila mwezi
Huyu aliletaa mfumo wa kusahihisha mitihani kwa Computer wachaa tusubiri. Yaan kuna mambo ya hovyo hovyo sana kila siku mifumo mifumo
 
Hivi mwalimu unasainishaje mkabata mpya eti wa kufaurisha wakati uyu mwalimu tayali ni mwajiriwa na anamkataba wa kudumu wa ajira yake na serikali Ila leo unageuza walimu watoto eti saini huu mkataba usipofaurisha upandi daraja huu si utoto Yani mkataba mama unasema hivi wewe inakuja na vitu vya ajabu ajabu ebu acheni huo utoto
Unaitwa mkataba mdogo ndani ya mkataba mkubwa,kwamba mkataba ndani mkataba😂

Taifa Lina mambo ya hovyo hili
 
Huyu aliletaa mfumo wa kusahihisha mitihani kwa Computer wachaa tusubiri. Yaan kuna mambo ya hovyo hovyo sana kila siku mifumo mifumo
Wanasiasa ilibidi watenganishwe na wanataaluma,,Kuchanganya siasa na taaluma Kuna athari kubwa Sana ,,,

Mkuu wa wilaya na mambo ya Taaluma wap na wap
 
Huyu aliletaa mfumo wa kusahihisha mitihani kwa Computer wachaa tusubiri. Yaan kuna mambo ya hovyo hovyo sana kila siku mifumo mifumo
Yani jamaa anakaa anawaza linalomuiijia anawasilisha wakihoji Unasikia wasomi wamekaa wameona Sasa wasomi hawawezi kosea nchi ya kijinga Sana hii
 
Unaitwa mkataba mdogo ndani ya mkataba mkubwa,kwamba mkataba ndani mkataba😂

Taifa Lina mambo ya hovyo hili
Wakitaka matokeo mazuri watoe motivation waone siyo wawatishe tishe kwa vitu vya hivyo ovyo ajabu walimu wapo kimya wanasubilia wadau wa wa elimu wawasemee
 
Mimi kitu kinachonishangaza ndio hicho. Tena unaambiwa div one mpaka three wafaulishe kwa 50% usipoweza upandi daraja, unaona Huu upuunzi kiongozi?....hivi kama huku Kijijini hakuna facilities zozote za kuwafanya hata walimu wawe motivated wataweza kwa hayo matamko?
Ila mbona malengo ya chini hivyo? Mi nilidhani labda div. 1 - 4 wawe walau 99%?!
 
Wakitaka matokeo mazuri watoe motivation waone siyo wawatishe tishe kwa vitu vya hivyo ovyo ajabu walimu wapo kimya wanasubilia wadau wa wa elimu wawasemee
Mwalimu, uandishi gani huu?

Wengine humu wanaandika bila kuzingatia herufi kubwa, koma,kituo kikuu,kufungua sentensi n.k. Mfano subiri anaandika subili. Walimu wenzangu mnakwama wapi kiuandishi? Andikeni vizuri basi tuwaelewe. Halafu mjue kuwa kila "transformation" yoyote inapotokea sehemu yoyote ya kazi wengi wetu huwa hatupendi kwa sababu ya kufanya kazi kimazoea miaka nenda rudi.
 
Msonde anazingua Yani maagizo kila siku Sasa hivi shule kila siku ukaguzi ajabu wanaokuja kukagua wanakagua vitu vile vile

Anakuja afisa elimu na watu wake leo, wanakagua, kesho wanakuja sijui ukaguzi nini wanawakagua, siku inayofuata anakuja afisa elimu kata anakagua Yani wote hao wanakagua jambo lile, arafu wakimaliza wanaitana kikao kujadili Yale Yale , wasainishana POSHO wanaondoka next week Tena wanakuja Yani ni ujinga ujinga ujinga tu wizi mtupo katika pesa ya umma mafisa wapo busy na ukaguzi wa Jambo moja kila mwezi
Scheme of work, lesson plans,log book.
Sijui hizi nyalaka kazi yake ni nini yaani.
 
Back
Top Bottom