Laiti ungejua hao baraza wanavyopambana na hao wezi usingesema ivo. Fuatilia ishu ya Thaqaafa na ile ya Serengeti kisha useme kama baraza linahusika na wizi au
Weweeee,hivyo ni viini macho na zaidi utaona shule za binafsi mara nyingi ndo ukamatwa.
Za serikali ni mara chache sana.
Hivi Afisa elimu Mkoa REO, Afisa elimu Wilaya DEO kipindi cha mitihani si nao huwa kwenye kamati za Baraza?
Sasa yale maagizo ya ufaulu wa 100% kwa wasimamizi na wakuu wa shule huwa yanalenga nini?
Ukweli ni kwamba msimamizi wa mtihani,mkuu wa shule maagizo ya kuwezesha ufaulu wa 100% wanapewa ila wazingatie mambo mawili;
1. Wakifanikisha bila kukamatwa ni jambo la kitaifa.
2. Wakiwezesha ila wakakamatwa hapo linamhusu aliye kamatwa.
Lkn wakati wa kusahihisha mitihani hii,baraza ni wawezeshaji wakuu.
2021 English km siyo Literature form 4 ili sahihishiwa Mkoani Mbeya,ufaulu ulikuwa wa chini mno ila baraza wakawahimiza wasahihishaji wafanye namna mambo yawe angalau.
2022 Civics imesahihishiwa Visiwani Zanzibar,mambo hayakuwa mazuri hasa kwa shule za Mkoani Mtwara,hapa ndipo kauli za usisomesome alama siyo zako,ni za baraza mpatie mtoto alama zikawa zinatoka.
Walimu hawapendi haya maagizo na maigizo ndio maana wanasema baada ya zoezi kukamilika.
Inaeleweka shule hazina Walimu,miundombinu km nyumba za Walimu hakuna,dharahu mnazo waonesha Walimu,Uhamisho sasa hapo bora kunyamaza tu.
Kule shule za Msingi hakuna Walimu wa hisabati na inajulikana lkn mkaziba mashimo ya panya kwa kutumia mkate (hisabati ni kuchagua majibu) lkn Walimu wanajitahidi kiukweli kuhakikisha wanatekeleza mnachotaka na wanafaulisha sana.
HONGERENI KWA KUONGEZA UFAULU KILA MWAKA WAKATI SHULE HAZINA WALIMU HUKU IDADI YA WANAFUNZI IKIONGEZEKA KILA MWAKA.