Msonde maagizo yako yanaipoteza elimu

Msonde maagizo yako yanaipoteza elimu

Nakubaliana na wewe kwa 100% mleta mada uwenda anachuki binafsi na msode tatizo ni huyo kayombo mbaya zaidi msonde anaonekana kumuamini.
Ni chuki zake kwa Msonde na Kayombo. Kabla ya Kayombo alikuwepo nani (nimedokezwa alikuwa some body ...... Sumbuye). Alikuwa mzuri?

Hapa kuna maslahi ya mtu yameguswa!!!
 
alikuwa anapika data , umesahau kipindi kile hata nchi iliitwa ya uchumi wa kati . aisee tumepitia magumu mengi sana kwa kweli, walimu wanaonewa sana katika mambo mengi.
Nchi hii jamani 🤣🤣🤣🤣🤣 eti uchumi wa kati!

Kila siku ufaulu unaongezeka wakati mazingira ya kufundishia na kujifunzia siyo rafiki.

Kipindi Msonde anakuwa boss pale NECTA alionekana bonge la mtaalamu,lkn kumbe ni bonge la mwana siasa.
 
Ukitaka elimu bora boresha kwanza maslahi ya MWALIMU
Bila kuboresha maslahi hâta wangetoa matamko kutoka sayari ya Uranus Bado elimu haitapanda
Huwezi kupata matokeo without investment
Hakuna elimu bora bila maslahi bora kwa mwalimu
 
Huyu mwamba Msonde mnamwanzishia nyuzi hapa naamini ndiye mtu sahihi kwa sasa.

Hatuwezi kwenda kama tulivyozoea(business as usual).
Lazima apatikane mtu kama huyu mwenye uwezo wa kuchukua maamuzi kubadilisha mambo.
Tayari tumeona ndio watu waliosaidia kuondoa vitabu vya hovyo huko mashuleni.

Ninaanza kuwa na wasiwasi huenda ninyi mmetumwa na watu wa upinde kuleta fitna za kipuuzi hapa.

Acheni madhaifu ya elimu yetu yafanyiwe kazi.Vinginevyo mje na mapendekezo ya nini kifanyike na si kupinga tu ili mpunguziwe kazi

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Hakuna elimu bora kama maslahi ya MWALIMU ni duni
Facilitator namba Moja WA elimu ni mwalimu
 
Unaongelea wa sekondari na hawa wa primary ambao hawachujwi kutokea popote. Huoni kama walimu wa shule serikali kuna ulaini flan wanachukulia bora liende.
Mwanafnz anakuja hâta mlo WA ucku ulikuwa WA kususa sua,Hana daftar Hana kalamu,Ana njaa ukimfundsha ataelewaje?
Anakuja anakaa darasa Lina wanafunzi 80 ataelewaje? Ratio ya waalimu vs wanafunzi IPO Sawa? Mwalimu Hana makazi wakati watumishi WA ngazi za Juu Wana posho na makazi Safi alafu utegemee elimu bora? Sahau
Hakuna Elimu bora pasipo maslahi bora kwa mwalimu
 
Serikali inatengeneza tatizo la miaka ijayo

Kama mwanafunzi hajui kusoma asiendelee na darasa, ajifunze kusoma kwanza
Mwaka huu wajifunze kusoma, kuandika,kusikiliza na kuongea kiingereza, mwakani waanze masomo ya kidato Cha kwanza!!
 
Katika mazingira hayo hayo yenye changamoto bado tunaweza kuboresha utendaji kazi wetu.

Tuache visingizio (excuses).

Ni kweli maboresho yanahitajika kwenye utumishi wa Umma lakini bado katika mazingira hayo hayo hatujaweza kuwajibika ipasavyo kwa uaminifu wote.
 
Inawezekana kufanya zaidi tukiwa kwenye mazingira hayo hayo huku changamoto/matatizo yakiendelea kushughulikiwa.
 
Elimu yetu ina mauzauza mengi sana tena mnooo maana ni kama tunashindana japo haijulikani tunashindana na nani. Mfumo wa Elimu unatakiwa kuangalia upana na mtawanyiko wa wananchi wa Taifa hili. Uje mtaala ambao utakuwa na chaguo la watu wa nyanda za juu Kaskazini kuwa na ziada ya Elimu ambayo inaendana na ukanda wao, Kanda ya ziwa nao wawe na ziada ya kitu ambacho watafunzwa kulingana na mazingira yao!
Kuhusu KPI na vitu vifananavyo na hicho uandaaji wa lesson plan na vifaa vya kufundishia ili kumsaidia mwanafunzi kuelewa zaidi ni sawa viwepo na ufuatiliaji uwepo ila njia ya ufuatiliaji labda ndio ibadilike! Elimu yetu ni kwaajili ya kujibu mtihani sehemu kubwa ni hivyo!
Swala la likizo kwa wanafunzi ni muhimu sana maana hii ya Sasa ya kwenda hadi jumapili tangu asbuhi hadi saa 12 jioni inasababisha wazazi kukosa hata muda na watoto wao ambapo sehemu kubwa ndio wangewaelekeza maadili na Mila zao mbali mbali!
Nmesoma pahala Leo makamu wa Rais anasema Elimu yetu haikidhi mahitaji ya wanafunzi katika kujitegemea.
Kufanya jambo lile lile kwa namna ileile na kutegemea matokeo tofauti ni namna nyingine ya shida ya afya ya Akili.
Walimu wana stress
Wanafunzi wana stress
Wakuu wa shule nao stress
Tunatengeneza Taifa lenye stress
 
Kwani huwezi kuongea kama msomi mbn unabweka2 tu Sasa elimu ya cheti inahusiana Nini , watu wenyewe ndo mliopata digrii baada ya matokeo yenu mli standize Yale ya form four, nenda kakalie ww kiti kile tuone utumbo wako!
 
Kwani huwezi kuongea kama msomi mbn unabweka2 tu Sasa elimu ya cheti inahusiana Nini , watu wenyewe ndo mliopata digrii baada ya matokeo yenu my standize Yale ya form four, nenda kakalie ww kiti kile tuone utumbo wako!
Aliye standardize na mwenye matokeo ni nani mhalifu?
BTW kauli aliyo itoa pia siyo nzuri ijapo wewe pia umedhihirisha ubovu wa mfumo wa elimu yetu.
 
Kwa ufupi tu msonde tangu ufike Tamisemi umekuwa na Mambo mengi Sana ambayo mengine hayana ufanisi ebu yapunguze, kutokana na karenda kuanzia tarehe 31/03/2023 ni likizo Ila kutokana na maagizo yako ya ajaubu ajabu likizo imekuwa Kama kiini macho shule zinaendelea na kazi wanafunzi na walimu wanakiwa kuwepo shuleni eti KPI huu ujinga mmeutoa wapi Yani umeleta mambo mengi mpaka sasa uko mashuleni baada ya walimu kufundisha walimu wamekuwa bize na kuandaa documents tu maana unamini katika tarifa siyo ufundishaji hivi nani akwambia andalio la somo likiwepo mtoto ndio ataelewa Yani mmekalia uzamani zamani pasipo kuangalia dunia inataka nini

Na nyie watu wa vetting huwa mnakwama wapi mtu Kama alikuwa mwalimu shule ya msingi uko msimpe madaraka ya kusimamia vitu vikubwa hawa watu huwa wanaalibiwa na elimu yao ya cheti hata apate udokta bado atakuwa na mambo akili ile ile ya kidato Cha nne ndio haya msonde anayofanya Kama mnabisha subilieni natokea ya kidato Cha nne na darasa la saba na darasa la nne mwakani uyu msonde kaja na vitu vya hivyo hivyo katika elimu

Hivi mwalimu unasainishaje mkabata mpya eti wa kufaurisha wakati uyu mwalimu tayali ni mwajiriwa na anamkataba wa kudumu wa ajira yake na serikali Ila leo unageuza walimu watoto eti saini huu mkataba usipofaurisha upandi daraja huu si utoto Yani mkataba mama unasema hivi wewe inakuja na vitu vya ajabu ajabu ebu acheni huo utoto


Kama idara zenu zinapesa za kuzungukia mashule kukagua vitu vya ajabu ajabu nashauri hizo pesa endelezeni michezo
Hapo ulipotoa angalizo la kusubiri matokeo ya la 4, 7 na kidato Cha 4 unajidanganya tu,nyanga zitapigwa ili ionekane Mzee Msonde ana tija!
 
Vyeo vya kuteua watu kwa ukada na kujuana ni shida.
Juzi kati alikuja Tanga akafokea sana walimu.
Ajue walimu nao ni watu wazima wenye familia kama yeye.
 
Sio tu kufukuzwa kazi ila ningekuwa nipo jera maana ningepiga jiwe kichwa cha mkuu wa shule
Mwalimu wa part-time vipi?
JamiiForums471477416.jpg
 
Back
Top Bottom