mpasta
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 919
- 2,004
Daah... asubuhi asubuhi leo nimeshuhudia kituko, Mstaafu akionja shubiri ya huba baada ya kuhonga nauli yake ya Daladala. Picha lilianzia kituo cha Daladala cha Njia Nne, anapanda msichana wa rika la miaka 25-30. Siri iliyobaki tupu, amekaa mstaafu mmoja wa Jeshi namfahamu tupo nawe Club moja ya Jogging kitaa.
Basi binti alipokaa tu kwenye siti, Babu kaanza kumuimbisha maneno ya lolo lolo...mpaka na namba za simu wakabadilishana. Sasa wote wanashukia kituo cha shule, kituo kimoja kabla haujafika Mbezi Mwisho. Babu akachomoa elfu moja, akamkabidhi Binti alipe watu wawili.
Sasa Babu katangulia kushuka kamwambia kondakta kuna mtu atanilipia yupo nyuma. Yule Binti hakushuka haraka kavuta muda kidogo, aliposhuka kamwambia kondakta akate mtu mmoja. Basi Kondakta kafura kama kifutu anaanza kuuliza yule "Mzee mbele kaniambia kuna mtu anamlipia, nani anamlipia??"
Daladala lote kimyaaa. Basi dereva alitoa gari kwa nguvu wakamuwahi Mzee mbele anatembea zake wakasimamisha gari. "Babu acha uhuni, leta 500 yangu, usinitanie..!". Babu nae kapaniki anaanza kugomba kuwa anavunjiwa heshima. Abiria wakaanza kumshukia Babu kama Kipanga wakimtaka alipe pesa ya watu asilete ubabaishaji wameshuhudia sakata zima, kondakta hana makosa. Ikabidi ajitokeze Msamaria mwema akalipa nauli ya babu safari ikaendelea.
Leo nimeamini kweli wanaume hatuzeeki, mtu una above 60 kwa umri bado unahangaika na vibinti vya mwaka 2000...mpaka unahonga nauli yako aiseee.