Mstaafu ahonga nauli yake ya daladala

Mstaafu ahonga nauli yake ya daladala

mpasta

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
919
Reaction score
2,004
Daah... asubuhi asubuhi leo nimeshuhudia kituko, Mstaafu akionja shubiri ya huba baada ya kuhonga nauli yake ya Daladala. Picha lilianzia kituo cha Daladala cha Njia Nne, anapanda msichana wa rika la miaka 25-30. Siri iliyobaki tupu, amekaa mstaafu mmoja wa Jeshi namfahamu tupo nawe Club moja ya Jogging kitaa.

Basi binti alipokaa tu kwenye siti, Babu kaanza kumuimbisha maneno ya lolo lolo...mpaka na namba za simu wakabadilishana. Sasa wote wanashukia kituo cha shule, kituo kimoja kabla haujafika Mbezi Mwisho. Babu akachomoa elfu moja, akamkabidhi Binti alipe watu wawili.

Sasa Babu katangulia kushuka kamwambia kondakta kuna mtu atanilipia yupo nyuma. Yule Binti hakushuka haraka kavuta muda kidogo, aliposhuka kamwambia kondakta akate mtu mmoja. Basi Kondakta kafura kama kifutu anaanza kuuliza yule "Mzee mbele kaniambia kuna mtu anamlipia, nani anamlipia??"

Daladala lote kimyaaa. Basi dereva alitoa gari kwa nguvu wakamuwahi Mzee mbele anatembea zake wakasimamisha gari. "Babu acha uhuni, leta 500 yangu, usinitanie..!". Babu nae kapaniki anaanza kugomba kuwa anavunjiwa heshima. Abiria wakaanza kumshukia Babu kama Kipanga wakimtaka alipe pesa ya watu asilete ubabaishaji wameshuhudia sakata zima, kondakta hana makosa. Ikabidi ajitokeze Msamaria mwema akalipa nauli ya babu safari ikaendelea.

Leo nimeamini kweli wanaume hatuzeeki, mtu una above 60 kwa umri bado unahangaika na vibinti vya mwaka 2000...mpaka unahonga nauli yako aiseee.
 
Huyo sister anaonekana wale wadada wa mjini [emoji16]

Ila maisha magumu sana mtaani
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hatari sana ila nazo nuksi zingine tunazitafuta wenyewe yaani asubuhi asubuhi unaanza kutongoza hata jua halijachomoka vizuri
 
Juma lililopita nilishuhudia mzee mmoja kwenye bus safarini alikaa siti ya mbele yangu na Binti mmoja alikuwa kajiremba sana yule Binti. Katika hali ya kushangaza yule Binti aliitupa simu ya yule mzee nje huku bus likiwa limechanganya mwendo [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mzee alianzisha ugomvi wa kufa mtu huku akilalamika simu yangu simu yangu.

Ikamlazimu kondakta kuingilia kati, lahaulaaa mambo hadharani, yule Binti akaanika ukware wa yule mzee. Yule mzee alikuwa akimtongoza yule Binti alikataa , mzee akawa anamlazimisha ampe namba yake ya simu , alipojichanganya ni pale alipompa simu yake ili aandike namba , ayaa Binti kapokea simu vizuri akafungua kioo Cha dirisha akaitupilia simu nje huko kisha akafunga kioo akatoa kitenge chake kwenye mkoba akajifunika vizuri akatulia kama hakuna kilichotokea vile[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Tulicheka sana ,Sikuwahi kuona tukio kama lile kabla. Bus linatembea , mzee ilibidi ahamishwe seat kwa kubadilishana na abiria mwingine. Kila mmoja alikuwa na maoni yake juu ya lile tukio
 
Daa hii inatia simanzi.Vipi lakini ukimfungulia kesi.Yaan mi kutaka tujenge umoja ndo uniharibie mali zangu!!
 
Yaani unampa simu aandike namba yake yeye anatupa nje....nitamtandika vichwa viwili tu na ndio itakuwa chanzo cha mimi kurudi magereza....
 
Back
Top Bottom