Mstari gani wa BIBLIA umegusa maisha yako?

Mstari gani wa BIBLIA umegusa maisha yako?

Joined
Jun 9, 2017
Posts
98
Reaction score
148
Binafsi kwa siku ya leo, mstari huu wa BIBLIA umegusa maisha yangu nazidi kuutafakari na kuomba neema nipate kuuelewa zaidi na kuyaishi mafundisho hayo.

Galatians 5:22-23
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
 
Attachments

  • LB_-_Fruit_of_the_Spirit_3c44e559-4cf8-4891-81b2-ca29c0d5b1d2_1080x.jpg
    LB_-_Fruit_of_the_Spirit_3c44e559-4cf8-4891-81b2-ca29c0d5b1d2_1080x.jpg
    104.3 KB · Views: 1
Binafsi kwa siku ya leo, mstari huu wa BIBLIA umegusa maisha yangu nazidi kuutafakari na kuomba neema nipate kuuelewa zaidi na kuyaishi mafundisho hayo.

Galatians 5:22-23
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Now the works of the flesh are evident, which are these: fornication, uncleanness, lasciviousness, idolatry, sorcery, enmity, strife, jealousy, fits of anger, dissensions, heresies, envy, drunkenness, revelries, and things like these. Of these I tell you beforehand, as I have told you in time past, that those who practice such things will not inherit the kingdom of God.
 
Ule mstari wa mzizi kiwa mjinga jamani nauomba. Maama hiyo ndio heading ya maisha yangu
 
Filp 4:13
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Just imagine mambo yote how amazing. Inanipa imani na kuzidi kupambana nikijua kuwa nayaweza hata yawe magumu vipi.
Jana nilikuwa natafakari kitu, Jana usiku!

Kutokea kwenye mstari huu!

Mathayo 19:26
[26]Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.

But Jesus beheld them, and said unto them, With men this is impossible; but with God all things are possible.

Nikawaza hivi; Kwa kuwa Yeye, yu ndani yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Yeye Mungu aliye ndani yetu!

Akitaka Kufanya jambo lolote! Kupitia Mimi, na wewe na yule! Inawezekana! It is Possible!

Kwa kuwa, sio sisi tutendao kazi Bali yeye aliye ndani yetu!

Hivyo tusiogope kuthubutu kufanya mambo makubwa tunayopata muamko wa kuyafanya kwa kuwa, si sisi ndio tutakayo Fanya ila yeye aliye ndani yetu

Sasa nilipoona na Hilo Neno lako! Ndio nikakumbuka
 
Jeremiah 11:11
Yeremia 11:11
[11]Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitaleta mabaya juu yao, ambayo hawataweza kuyakimbia; nao watanililia, walakini sitawasikiliza.

Therefore thus saith the LORD, Behold, I will bring evil upon them, which they shall not be able to escape; and though they shall cry unto me, I will not hearken unto them.
 
Now the works of the flesh are evident, which are these: fornication, uncleanness, lasciviousness, idolatry, sorcery, enmity, strife, jealousy, fits of anger, dissensions, heresies, envy, drunkenness, revelries, and things like these. Of these I tell you beforehand, as I have told you in time past, that those who practice such things will not inherit the kingdom of God.
Bila shaka ni Galatians 5 : 19-21 .
Shukrani sana mkuu, tuzidi kubarikiwa sote kwa pamoja, safari ya kujifunza haina kikomo.
 
Zaburi 126:1

[1]BWANA alipowarejeza mateka wa Sayuni,
Tulikuwa kama waotao ndoto.

When the LORD turned again the captivity of Zion, we were like them that dream.

Huu mstari! Ninaupenda sana, ni wazi kuwa waliosema haya maneno "... Tulikuwa kama waotao ndoto"

Ni wazi kuwa walikuwa wamekwisha kukata tamaa na kupoteza Tumaini. Yaani waliamini ndo basi Tena, haiwezekani jambo Hilo Kutokea!

Umewahi Kutafuta kazi, ndoa, mahusiano yenye Amani, mtoto, uponyaji, au Chochote kwa muda mrefu sana!

Kwa maombi, sadaka na kufunga lakini jambo Hilo hukulipata! Ukafikia hatua ya kukata tamaa na kumkatia tamaa Mungu!

Katika Hali hiyo Sasa! Mara gafla siku moja unashangaa unapokea haja ya moyo wako ya muda mrefu!

Ndio Hawa Sasa wanasema "Tulikuwa kama waotao ndoto" yaani hakutegemea kabisa!

🤓
 
Ndio kuwa mtu anaye zini basi ni hana akili...upo huo mstari
Mithali 6:32

[32]Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

But whoso committeth adultery with a woman lacketh understanding: he that doeth it destroyeth his own soul.
 
Back
Top Bottom