Mstari gani wa BIBLIA umegusa maisha yako?

Mstari gani wa BIBLIA umegusa maisha yako?

Jana nilikuwa natafakari kitu, Jana usiku!

Kutokea kwenye mstari huu!

Mathayo 19:26
[26]Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.

But Jesus beheld them, and said unto them, With men this is impossible; but with God all things are possible.

Nikawaza hivi; Kwa kuwa Yeye, yu ndani yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Yeye Mungu aliye ndani yetu!

Akitaka Kufanya jambo lolote!
Amen mkuu ndio hivyo hata jaribu likitupata twajua tutalishinda.
1 Wak 13:10
hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu hataruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu.
 
Amen mkuu ndio hivyo hata jaribu likitupata twajua tutalishinda.
1 Wak 13:10
hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu hataruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu.
Sijui kwanini umejibu kwa kutumia mstari huu!

Ila umesema na Mimi kabisa 😂
 
Wakorintho 11:6
Ikiwa mwanamke hatafunika kichwa chake, basi na azinyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukata nywele zake au kuzinyoa kichwani mwake. Hivyo anapaswa kufunika kichwa chake.
 
2 Kor 9:7

"Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu."
 
Na tutengeneze mtu Kwa mfano wetu

Yani hao wetu ndyo wakina nani na wapo wangapi ?

Mfano wetu akiwaza sana lazima achanganyikiwe
 
Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako....Ee Mungu nitetee🙏
 
Ile yohana 14 nina miaka na miaka ndo mstari wangu pendwa.....
"Mnamwamini Mungu, niaminini na mimi..."
Yesu atakuja mara ya pili kutuchukua na maswaibu yote ya ulimwengu yatakoma. Tumuamini yeye aliye na uhakika na makao yetu ya milele
 
Back
Top Bottom