Mstari gani wa BIBLIA umegusa maisha yako?

Mstari gani wa BIBLIA umegusa maisha yako?

Ila unaamini uchawi upo
Nimekwambia kwamba, Siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yeyote ile.

Hakuna uchawi bali kuna maarifa ambayo wewe huyaelewi.

Kama huelewi kitu kinavyofanyika, Usiite uchawi.

Kama huelewi jambo fulani lilivyo fanyika, Usiseme ni uchawi.

Ni maarifa ambayo wewe huna au huyaelewi.
 
Yohana 8 :5 Basi katika Torati ,Musa alituamuru kuwapiga mawe wanawake namna hii:nawe (Yesu) wasemaje?

hii iende moja kwa moja kwa wale wanaojichukulia sheria mkononi
 
Siifahamu zaidi ila wakati fln nlikutanaga na haka kamstari sijui sura ila kanasema.yanini kuhangaikia kesho wakati kesho inajihangaikia yenyewe! Kila nikipata hela huwa nakatumia hako ka slogan .natamani kangekuwepo kweny quruan pia.
 
Nampango niongeze mistari kwenye Bible naona bado nafasi zipo wazi
 
Nimekwambia kwamba, Siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yeyote ile.

Hakuna uchawi bali kuna maarifa ambayo wewe huyaelewi.

Kama huelewi kitu kinavyofanyika, Usiite uchawi.

Kama huelewi jambo fulani lilivyo fanyika, Usiseme ni uchawi.

Ni maarifa ambayo wewe huna au huyaelewi.
Why is it that when I read this the sound that comes into my head sounds rude

Is this a rude reply
 
Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu.
 
Hakuna mstari unaogusa maisha yangu mimi mmatumbi, zaidi naona kama helaya za kijinga tu.
 
Filp 4:13
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Just imagine mambo yote how amazing. Inanipa imani na kuzidi kupambana nikijua kuwa nayaweza hata yawe magumu vipi.
Hii ipo kwenye Whatsapp profile yangu. Nilitaka niiweke humu, nikaona tayari ushaiweka. Tuko pamoja Kiongozi.
 
Ufu 14:13 Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam asema roho, wapate kupumzika baada ya tabu zao; kwakuwa matendo yao yafuatana nao.

Mhu 3: 1-8
(Kila jambo na wakati wake)
 
Zaburi 126:1

[1]BWANA alipowarejeza mateka wa Sayuni,
Tulikuwa kama waotao ndoto.

When the LORD turned again the captivity of Zion, we were like them that dream.

Huu mstari! Ninaupenda sana, ni wazi kuwa waliosema haya maneno "... Tulikuwa kama waotao ndoto"

Ni wazi kuwa walikuwa wamekwisha kukata tamaa na kupoteza Tumaini. Yaani waliamini ndo basi Tena, haiwezekani jambo Hilo Kutokea!

Umewahi Kutafuta kazi, ndoa, mahusiano yenye Amani, mtoto, uponyaji, au Chochote kwa muda mrefu sana!

Kwa maombi, sadaka na kufunga lakini jambo Hilo hukulipata! Ukafikia hatua ya kukata tamaa na kumkatia tamaa Mungu!

Katika Hali hiyo Sasa! Mara gafla siku moja unashangaa unapokea haja ya moyo wako ya muda mrefu!

Ndio Hawa Sasa wanasema "Tulikuwa kama waotao ndoto" yaani hakutegemea kabisa!

🤓
👏👏👏
 
Back
Top Bottom