"Msukule" wa Mapenzi...

...aisee! Imenibidi nicheke tu...ndio kusema hii hali haikwepeki! Once a Victim always a victim unless umtie sumu mwanao/wanao nao waanze kumchukia mama/baba yao...!

Msibishe, hii nimeiona bana...mama mtu kawatia sumu ya maneno watoto hawataki hata kumsikia baba yao. Jamaa hana
mbinu yoyote ya mawasiliano na Ex-mkewe wala watoto. Jamaa kaishia kumwaga misaada ya pesa kwa ndugu wa mke kama hana akili uzuri. Mke ananuna lakini hali ya uchumi ndio hivyo tena...[ndugu] wakatae pesa za bure?

Psychological abuses hizi, hata hujui mshindi nani.



Mkuu hii issue iache bana inaumiza wengi na wengi wanaingia kwenye mtego bila kujua ni wapi wamenaswa na kujikuta wanaishia kuwa ndio mzee
Mwanamke anajua mkuu kushika na kucheza katara yake na utaicheza bila hata kulazimishwa au kushikiwa bunduki yaani unajikuta tuu unaendeshwa kama gari bovu. Tuache ile kitu ambayo anaitengeneza yeye kukufanya uumie rohoni "emotional torture" yaani kukufanya wewe ujisikie kuwa kila unalofanya though she is your Ex unamuumiza na hata kuwa na mwenza ulie nae sasa hivi unamuumiza so she needs your care, your hospitality, emotional care, kiss and hug through the night, sweet sms and even call and protection. Na anapohold another key issue, watoto ndio kabisa atawafanya kama ndio chambo cha kuvulia samaki baharini yaani kila anapokuhitaji anaweka issue ya watoto mbele. Na anawatanguliza mbele ili wewe ufuate na ujue kuna nini.
 
Reactions: Mbu

Asante nyumba kubwa kwa mfano mzuri na amini utatusaidia si wengine katika malezi ya watoto wetu. Mimi nilikua nafikiri tu kuwa tukianzisha ligi mi na huyu mwenzangu inaweza kumuathiri mtoto na baadae akatuona hatufai ikumbukwe nilikua nafikiri tu kwani mimi nimelelewa na baba yangu na mama yangu na mpaka sasa wanazeeka pamoja. Kumbe mawazo yangu ni sahihi thanks a lot nyumba kubwa na kwa kweli niko tayari kufanya lolote liwezekanalo kumfanya binti yangu awe na amani na sio kuanza kuwaza kujifurahisha mimi na utu uzima huu lol.
 
Reactions: Mbu
Hongera mbu kwa mada tatanishi sana...maty jaribu kuyaangalia maisha ya simba mnyama...wewe kama mwanamke ni lazima utampigania mwanao...na huyo mumeo yeye anaangalia kukumiliki 100% ikiwemo kuwa na kizazi naye na kwa taarifa huyo mwanao sio ishu kwake kabisaaa...na kuendelea kumuendekeza huyo ex kisa mtoto ni kujitafutia jambo jingine..hapa kuna utata wa kimaumbile. Hata maandiko yanasema Yusuph baada ya kujua Marimu yu mjamzito akapanga kwa siri 'kumuacha'mpaka alipopigwa mkwara mzito (alitengenezwa kiroho)
 

Gaga hapo ndo ninapochoka mimi na nadhani ndo mzizi wa hiyo Emotional Roller Coaster....maana mtu mmeachana na mmeshajipandisha vyeo vye u-Ex. Anaitumia hiyo feeling yako kuendelea kukuhunia!! mimi nashindwa kuelewa ni nini hasa anachokitaka........ingekuwa mara moja au mbili akicheza na hizo feelings zako ukarespond positively aache na kutulia but yeye, anaponyeza button, ikijibu anachomoa au anafanya kituko kisha tena anabonyeza......mimi kusema ukweli Mbu ungekuwia leo umetoa mtihani juu ya huu mkitu ningepata zero yenye masikio na vinywele viwili!!

Nia ni kuharibu tu equillibrium yako ya mapenzi na maisha kwa ujumla! Mie kusema ukweli nashukuru nimejifunza ingawa nshazeeka najihesabu ndo nimekua sasa kimapenzi ..................
 

Chauro, usiombee yaani hapa ndipo sometimes hujikuta natafakari sana ule usemi wa 'Bora uishi na anayekupenda zaidi ya unavyompenda wewe" kwa sababu maumivu ya kumpenda mtu ambaye mwanzoni alionyesha kukupenda halafu kumbe ndani ya moyo ka'kihifadhi' hayaelezeki. Mwe!!
 

haya sasa,...lol...'nataka sitaki!'...NN, kwanini inakuwa ngumu wengi ku give up for good japo hawamtaki 'kidz mama?'
 

Tulizo ndugu yangu, hongera sana yaani natamani kweli ningeweza nami kuishi 'kikavu' kama uishivyo wewe!! unajua suala zima la maumivu linatokana na hisia ambazo zamani kidogo hazikuwa na umuhimu mkubwa kihiiivyo katika mapenzi (nadhani ndo maana ilikuwa pia rahic kuoa/lewa na mtu uliyechaguliwa na wazazi) Unfortunately kizazi chetu hiki tumejichakachusha kwa mapenzi ya kizungu ambayo yanaweka hisia mbele zaidi kuliko hali halic............ukitendewa jambo kidogo tu la kimaisha.... unalitafcri kihisia, kwa nini, why me, kwa nini anifanyie hivi, atakuwa hanipendi, eh atakuwa keshapata mwingine ili muradi tabu tupu...........Naomba shule wajameni
 
Tulizo ndugu yangu, hongera sana yaani natamani kweli ningeweza nami kuishi 'kikavu' kama uishivyo wewe!!

...mmnnh? kwanini umetamani hilo?

unajua suala zima la maumivu linatokana na hisia ambazo zamani kidogo hazikuwa na umuhimu mkubwa kihiiivyo katika mapenzi (nadhani ndo maana ilikuwa pia rahic kuoa/lewa na mtu uliyechaguliwa na wazazi)

...mnnhh? hisia za zamani zinatofauti gani na za sasa?


Mwj1, hali halisi ndio ikoje hiyo yarabi compared na mapenzi ya hisia?...
 

MJ1, Nakubaliana nawe kuwa moja ya chanzo cha misuguano ndani ya mahusiano ni jinsi gani tunavyoshindwa kudhibiti hisia zetu.

Kwa mtazamo wangu hapa kunaingia vitu vingi..Trust, kiasi gani nimemwamini mweza; sacrifice - kiasi gani nimejitoa muhanga yaani si kila siku mtu mmoja tu apate ushindi wa hoja ndani ya nyumba..lazima ushindi uwe wa kupokezana .leo mimi..na kesho yeye.labda tu kama hoja ni ya nguvu..hivyo basi hapo utaona kuna aina fulani ya kubali yashinde au kwa upande mwingine unakuwa msukule wa kujitakia ..ili kuleta usawa, kuaminiana na kupunguza hisia kali kwenye mahusiano.

Lakini ..Je? utandawazi unachangia kushuka thamani..kwa Sacrifice, Uaminifu, Heshima, Busara, Nidhamu etc.. Inawezekana ni kweli..Wazazi wetu wamezaliwa na kukua katika mila na tamaduni nyingine..wakatufundisha wanavyojua wao.. lakini sisi watoto wa dot com tukaacha tamaduni zetu na tunajaribu ku-experiment mseto wa tamaduni za utandawazi na za kiafrika yaani kinachotoka hapo ni chotara...na kusaga meno..
 
...mmnnh? kwanini umetamani hilo?


Darling, ndio najaribu kuomba msaada wa somo hapo! Maana kwangu mie (tofauti na Tulizo) siwezitenganisha mapenzi na hisia.......kwa sababu alivyoeleza kuwa tofauti na wale ambao wanajifanya wanajua kupenda (nimetafsiri kuwa ku'hangaika' kuonyesha unampenda mtu lazima kuendane na hisia........nitakukiss Mbu kwa kuwa ninahisia za kukupenda, nitaku-hug kwa kuwa ninahisia za kukupenda vivyo hivyo nitakuprotect na 'maumivu' ya moyo na nafsi kwa kuwa nahisi ninakupenda- Hii ni tafsiri yangu ya kuexpress love. Kwangu mie LOVE=Feelings ambazo zinadirect matendo yangu kwako.

...mnnhh? hisia za zamani zinatofauti gani na za sasa?


Hazina tofauti Mbu nilichomaanisha ni kuwa watu wa zamani hawakuwa wana'zisikiliza sana' hisia zao au hawakuwa wana'zitii' sana hisia zao za kimapenzi. Yaani ku'itikia' hisia kipindi hicho kulikuwa si kwa sana kama leo hii na ndio maana kulikuwa na 'tolerance' ya namna flani hivi kwamba baadhi ya makosa ya ndani ya ndoa (kimapenzi) yalichukuliwa ni madogo na yalitatuliwa kirahisi zaidi si kama siku hizi ambapo mtu akinyimwa unyumba siku moja tu kwa kuwa mwenzi anaumwa basi anatafsiri ana mwingine/ amegawa kwa houseboy/girl/bosi au secretary n.k. ni hisia ambazo zinajijenga kwenye imani na mwisho matendo ya revenge n.k.



Mwj1, hali halisi ndio ikoje hiyo yarabi compared na mapenzi ya hisia?...

Mbu mbona umeichambua sana hii post jamani?.........hali halisi mie ninadhani ni kujaribu kulink hisia na maisha halisi. Hii ninafikiri mie haiko sana kwa wenzetu wazungu ambao wao wana tendency ya Ku-dilink/kutenganisha hisia na maisha (kama kuna tafsiri yake!) ambapo kwao hisia zina nafasi kubwa zaidi na wanazitii sana sometimes unnecessarily... (mfano umekaa na mtu kwa miaka miwili---ndoa halali-- ghafla unaamka hujisikii kumpenda tena--- unafile divorce!!!) . So ninachomaanisha hapo Mbu ni kuwa hata ikitokea siku nimekujibu vibaya basi usikimbilie kuumia hisia zako kuwa mapenzi yamekwisha siku hizi! Au siku nikikwambia I need time alone (nendalala chumba cha wageni LOL) unielewe na sababu nitakayokupa uielewe usikimbilie kuconclude kuwa mapenzi yamepungua au siku hiyo nitakuwa nimepata 'dozi' kubwa kutoka kwa 'mwizi' wako!

Leo nimelichokoza .................Jamani mada ni Msukule wa Mapenzi na si nyingineyo.

Mbu na wale ambao walionja wakanogewa, wakaamua kubinafsisha then wakakinai wakakitelekeza lakini bado wanakushkilia kiaina (hizo emotional chains) huku wakikupa zile za ..............au .......Mie najua kuoa tu, sijui kuacha au Niliapa for Better, for worse on my wedding day so I wont give you a divorce??
 

.....Nafikiri tuko katika jahazi moja Tulizo ni sawa kabisa na niaminivyo mie. Mambo ya utandawazi na package yake yote ndio chanzo cha misuguano katika ndoa nyingi..... ingawa si kwa mabaya tu but hata kule kumfunua mtu juu ya haki zake kimapenzi/ndoa ambavyo kwa namna moja au nyingine kumesababishwa na Utandawazi umechangia sana katika kuvunjika kwa mahusiano mengi hasa ya kindoa. Uvumilivu na ile hali ya 'kuchukuliana' imepungua kwa kiasi kikubwa sana..........Mama yangu mara nyingi husema mahusiano yetu siku hizi ni ya 'ki-Egoli" yaani kama mchezo wa kuigiza hayana uhalisia hata kidogo.,, hayampi mtu mwanya wa kuishi kama yeye, kwa staili aionayo yeye inamfaa kuhakikisha ndoa/mahusiano yake yanadumu! Akikosewa kidogo ataanza kulinganisha na mwenzake na kuangalia mwenzakek alichukua hatua gani, vitabu, theories zinasemaje juu ya kitendo alichotendewa n.k
 

Mkuu hapa lazima utambue kuwa emotion ndo inakuwa silaha yake kubwa, so anaona akitumia hii anaweza pata fast help may b akikurecall hw you used to care for him/her.
 
Reactions: Mbu
Samahani wadau wa huu mjadala,

Naona nimekwama kabisa. Kila ninachosoma hakieleweki...Naogopa kunyonyoa hizi mvi zangu na kubaki na kipara (ukizingatia huku karibu na DRC kipara ni deal la nguvu)!

Kuna jamaa alinambia kuwa hii dhambi inayohusisha kugandishana kwa miili ni mbaya sana, kwani haifutiki milele! Ni zaidi ya kupigwa ndonya usoni!!

Halafu inakuwa mbaya endapo dhambi hiyo inaenda hatua moja mbele kuleta matunda ya uumbaji!

Kame Ex-BFs/Gfs hawachani milele, iweje wakiwa na mtoto....Hili naomba nijitoe katika mjadala wake!
 

Mzee wangu DC, with all due respect I beg to meander hapo kwenye red.........not to differ with you because to some it is and will remain true but I would like to meander kwa upande wangu. It only depend with sababu zilizowaachanisha na status mliyopo kwa sasa. Kama mliachana bila mapenzi yenu i.e. wazazi hawakupenda, au mitazamo tu ya maisha ikawafanya muachane ilihali bado mwapendana inawezekana kweli msiachane! But also inategemea na status yenu kwa sasa....kama mliachana mkingali mnapendana halafu kila mtu akamove na mahusiano mengine to some extent inakuwa ngumu kidogo (sisemi haiwezekani) kurudia kuwa na mahusiano.

But Babu mmeachana baada ya kuumizana kwa maana halisi ya kuumizana hisia kiasi kwamba mioyo imejaa kutu halafu kila mmoja akawa na mahusiano mengine nadhani itakuwa ngumu kurudisha hisia! Ni mtazamo wangu tu inawezekana kabisa isiwe sawa.
 
Nyamayao; cpo na watoto ndio sababu kubwa cm haziwezi kuwa off, na hata yeye hatakubali cm ziwe off kwa sasa coz ameshakuwa na kawacwac fulani, anahakikisha cm zote(zake/zangu) zipo on na mahali pa1, nikisema umenitibua ni kweli kabisa, bado kuna vuguvugu ya call ya juzi juzi, nipo kwenye wakati mgumu jamani.....

Nyamayao dada, naona kama unakumbatia hiyo tabia ya X-wako kuendelea kukusumbua. Kama kweli huna nia naye basi ukijuwa anakupigia mida ya usiku usipokee simu wewe, mwambie mmeo apokee. Haiingii akilini X-wako anajuwa umeolewa alafu akupigie mida hiyo ya usiku bila ya wewe kumpandishia na kumwambia akome kukupigia. Unamung'unya maneno ya nini akiwepo mumeo? Mtolee uvivu kuwa asikupigie au uongee na mumeo kuhusu hilo na jinsi ya kulikomesha. Hata kama ni mimi ndo ningekuwa huyo mumeo ningekupandishia unieleze vizuri masuala ya simu za usiku mida ya kulala. Mumeo atakuwa na wasiwasi kuwa huwa mnaongea sana hata mida asiyokuwepo unajaribu kupotezea tu.
 
Reactions: Mbu

Hata mimi nina ex ambaye haachi kunitoneshatonesha vidonda.............................kwa kudai bado ananiwazawaza.........................lakini mimi humpuulizia mbali........................mara nyingi tunahitaji vitu ambavyo hatuna siyo kwa sababu ni vizuri ila huwa msukumo wa tamaa tu............claiming that it is one more time of finger licking pleasure.............................what a lie..........
 

with this input................you will never walk alone..............................because I am right behind you for all the right reasons........Ila ni swali hivi mwaweza kuachana bado mwapendana.................soma nyekundu...........naona hiyo ni migongano....................................I ma m just wondering aloud.........
 

Dahhh,...ungeniona nilivyokenua kwa jinsi ulivyonijibu vizuri!...In real life ukiwa unanijibu hivi potelea mbali niitwe msukule!



...nadhani hii pia inatokana na kasi ya maisha,...kwa sasa hatuna muda wa kukaa chini ya mwembe kusubiria dodo lianguke, au alfajr unaamkia chini ya miembe kutafuta yaliyoanguka usiku...Kizazi hiki ni cha kukimbilia Shoprite au Imalaseko kununua Mango juice ya Azam, tamu kuliko tunda lenyewe... yaani tunaishi maisha ya short cuts kibao,...na siku hazigandi vile vile...Tukubali mabadiliko. Zama za kuandikiana barua, niifukizie poda na marashi, kisha niitume kwa posta mpaka ikufikie wakati kuna emails/sms leo hii nitaonekana sijali muda.

Hizi theories, kusoma vitabu, au kubandika post JF upate msaada wa mawazo ni kiashiria kwamba hatuna muda wa kukaa na wazee wetu, mashangazi na wajomba kupata busara zao juu ya maisha kwa ujumla. Kama mnakumbuka ile Topik ya Wheel of Life?, kuna wengi waliipinga kwamba muda hautoshi kabisa. Twendeni na wakati kabla wakati haujatuacha tukabakia tunashangaa...

...Mzee DC bado anashangaa shangaa haya mambo tunayoongelea,....kwani kuzaa na mtu lazima muwe mlipendana nae kiviiile? Vile vile kuna zile One night stands ambazo mw'mke ana conceive kisha anachukulia mtoto kama bakora ya kukuchapia. Mwanaume unaishia kulambishwa kimtego mtego, ....mtoto hupewi, kwa mkeo hajulikani,....uhakika wa mtoto mwenyewe kama ni wako au sio wako hujui...ukijifanya kusahau unakumbushiwa...almuradi unachezeshwa makida-makida tu... mnh, maisha haya, misukule ipo ya aina nyingi!
 

Mkuu..Tunashukuru kwa somo! Hizo za RED ndiyo majibu ya mtihani wa maisha ya sasa..Nimekata na kuficha kwenye soksi.. Thanks!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…