Msukuma awajibu January na Nape asema kumkosoa hayati Magufuli ni nongwa kwa sababu wabunge wamekula viapo vya utii

Msukuma awajibu January na Nape asema kumkosoa hayati Magufuli ni nongwa kwa sababu wabunge wamekula viapo vya utii

UROHO na UCHU wa MADARAKA/ VYEO utawamaliza muda sio mrefu.

sisi watanzania tunawaangalia tu jinsi mnavyo jichimbia kaburi.

mwaka 2025 sio mbali, nyie endeleeni kuzongana zongana tu badala ya kujadili maendeleo ya wananchi.
 
Kwahiyo amechanganya madesa?
Hakika amechanganya mambo. Tumuhurumie. Anajua kuongea lakini hajui kuchanganua mambo hasa yanayohusu issues kubwa. Sasa hata kiapo ambacho huwa anaapa bungeni huwa hajui anaapa kwaajili ya nini. Yaani mbunge aape kumtii Rais!!!! Wakati bunge linatakiwa kuisimamia serikali. Hii ndiyo maana bungeni kumejaa mapambio na nyimbo za sifa, kwa sababu ya aina ya wabunge tulionao wakiwemo hawa wa "la 7 B"
 
Msukuma aambiwe na nani? Hao hao wenyewe wapambane nae kwa kumuelimisha na maneno yake yanayoshabikiwa na Ndugai!!! Mtu anasema bungeni eti matajili wote duniani hawajasoma na watu bungeni mnakubaliana na ujinga huo?? Matajili anaosema hawajasoma ni hao hao majambazi wenzie waliopata utajili kwa wizi!! Huko kwingine kwenye nchi za wenyewe MSUKUMA angekua jela kwa udanganyifu wa kupata hela benki na KUPARK kesi !!!
Yamkosaji hayo
 
Well said my friend!!!

Msukuma, Lusinde, Josephat Gwajima inaonekana wana lao jambo nyuma ya pazia ndio maana wanatumia nguvu mnoo kwenye hoja zao to the extent kwamba inakuwa inaku ni vigumu sana kueleweka na watu wenye upeo wa kuelewa mambo.
Wewe mwenye upeo mbona haupo bungeni. Kazi kushinda mitandaoni tu.
 
Hesabu zinazotumika na kina jk ni kali sana, hawa lasaba b hawatakuja kuamini macho yao! hao wanao wasema muda siyo mrefu watakuja kuwa mabosi wao. Hapo wametulizwa tu ila game itavyo change wasije kulialia.
Huu ndio ukweli
 
Kimsingi ccm si wamoja, bali ilikuwa inabidi waungane kinafiki kwa hofu ya kupoteza dola kwa cdm. Sasa wako bungeni bungeni wenyewe, hawana cha kuwaungasha zaidi ya kupoteana kutokana na makundi yao. Inatakiwa hilo genge haramu la ccm ligawanyike ili nchi hii ipone.
...Alisha sema Julius Nyerere...dhambi ya kubaguana ni kama kula nyama ya mtu....ukianza hutoweza iacha....
 
Mbunge wa Geita vijijini mh Msukuma amesema kuna wabunge wanadai kumkosoa hayati Magufuli siyo nongwa lakini sisi tunasema ni nongwa kwa sababu wabunge tumekula kiapo cha utii.

Msukuma alikuwa anampa taarifa mbunge wa makambako mh Jah people aliyesema wabunge wameingia bungeni kwa nguvu ya hayati Magufuli na wasaidizi wake mama Samia na mh Majaliwa Jah people amesisitiza waliokosa teuzi wawe wavumilivu kwani wabunge ni wengi vyeo ni vichache.

Hayo ni majibu murua kwa wabunge waliopitishwa bila kupingwa January Makamba na Nape Nnauye.

Ramadhan Kareem!
Siasa ni mchezo wa maneno
 
Kimsingi ccm si wamoja, bali ilikuwa inabidi waungane kinafiki kwa hofu ya kupoteza dola kwa cdm. Sasa wako bungeni bungeni wenyewe, hawana cha kuwaungasha zaidi ya kupoteana kutokana na makundi yao. Inatakiwa hilo genge haramu la ccm ligawanyike ili nchi hii ipone.
...Alisha sema Julius Nyerere...dhambi ya kubaguana ni kama kula nyama ya mtu....ukianza hutoweza iacha....
 
UROHO na UCHU wa MADARAKA/ VYEO utawamaliza muda sio mrefu.

sisi watanzania tunawaangalia tu jinsi mnavyo jichimbia kaburi.

mwaka 2025 sio mbali, nyie endeleeni kuzongana zongana tu badala ya kujadili maendeleo ya wananchi.
CCM itaendelea kuongoza maana upinzani wote ni machoko tu.
 
Mbunge wa Geita vijijini mh Msukuma amesema kuna wabunge wanadai kumkosoa hayati Magufuli siyo nongwa lakini sisi tunasema ni nongwa kwa sababu wabunge tumekula kiapo cha utii.

Msukuma alikuwa anampa taarifa mbunge wa makambako mh Jah people aliyesema wabunge wameingia bungeni kwa nguvu ya hayati Magufuli na wasaidizi wake mama Samia na mh Majaliwa Jah people amesisitiza waliokosa teuzi wawe wavumilivu kwani wabunge ni wengi vyeo ni vichache.

Hayo ni majibu murua kwa wabunge waliopitishwa bila kupingwa January Makamba na Nape Nnauye.

Ramadhan Kareem!

Natamani sana kumsikia Nape akichangia hoja kwenye sheria ya vyombo vya habari itakapojadiliwa

Maendeleo hayana vyama
 
Back
Top Bottom