Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port

..Na Chadema inapopata makwazo watu wa serikali hufurahia. Je, unafahamu?

..Pia kuna baadhi ya watu serikalini wanajihusisha na matukio ya utekaji, utesaji, na mauaji, dhidi ya wafuasi wa Chadema. Je, unaunga mkono?
Baba yake Chaula amepigiwa simu, anatakiwa Atoe mil 3,ili Chaula aachiwe!
 
HH rais wa Zambia ana akili sana!
 
Yes kinacho hitajika kwa sasa ni sera nzuri ya uchumi ikijumuisha maboresho mazuri ya mazingira ya uanzishwaji wa viwanda vidogo na hii iangalie mpaka biashara za wazawa, uboreshaji wa elimu

Tutume na kuwatumia watanzania wenye ujuzi kwenye nafasi au sekta zenye mapengo na ambazo zinaweza leta ufufuaji wa uchumi wa taifa hii aliitumia raisi wa china baada ya Mao nadhani ya kupeleka na kuwasomesha wazawa kisha kuwarudisha na wao wakafanya mageuzi lakini waliopewa dhamana na mfumo wao wote waliwapa back up ya kutosha na hii ndio China tuka anza kuisikia Kwenye level nyingine baada ya kipindi cha ukimya

Swala jingine ni kwamba mifumo yote iwe na nia ya kuendeleza taifa kwa ujumla tuwe na moyo wa kweli, tujitahidi angalau matumizi muhimu na vitu vinavyo tumiwa kila siku viwepo pasipo shida za hapa na pale wananchi wakipata usafiri wa uhakika, maji ya uhakika, umeme wa uhakika, chakula kinachoweza kuendana na kipato, nyumba zilizo boreshwa sidhani kama hawatokuwa na nia nzuri kwa taifa watakuwa tayari kuzalisha ili maisha yaende mbele zaidi.

Mfano tunaona hizi nchi za Asia zilizo fanya mapinduzi ya kiuchi China, sibgapore,Malaysia wananchi wao wanashirikiana na kupenda kila kitu na wana jitahidi kusogeza mbele uchumi wao kwa asilimia kubwa

Tanzania tueleke huko
 
Nchi yoyote haiwezi kusonga mbele bila ya raia wake kuwa na uzalendo kwa nchi yao.
Sisi tuko na rasilimali ila tumekosa uzalendo ndio maana kila siku tunaanza upya.
 
Nchi yoyote haiwezi kusonga mbele bila ya raia wake kuwa na uzalendo kwa nchi yao.
Sisi tuko na rasilimali ila tumekosa uzalendo ndio maana kila siku tunaanza upya.
Huenda ni kweli kabisa, tatizo sio uzalendo zaidi ni ubinafsi wa kimakundi, tunaweza songa kama taifa na wengine wakawa nacho kutokana na kupambana kwao lakini pia isiwe chanzo cha hali mbaya kwenye mahitaji muhimu ya jamii

Yaani wewe kuwa nacho isiwe sababu ya wengine kukosa huduma nzuri au kupungukiwa nazo ama kuendelea kuwa katika wimbi hilohili zaidi ya miaka mingi, unaweza miliki unachotaka lakini iwepo huruma na kujali wengine.

Itumike hekima na maarifa kwenye hilo jambo
 
Afrika ni unafiki tu,ndio maana hata DRC,ameona EAC haina faida kwake,na kutaka kujiondoa kwani kama wanachama walio ndani ya jumuia hiyo wanapokuwa hawaelewani na jumuia inashindwa kutafuta suluhisho,kwa kumuogopa mchokozi!!!na hizo nchi ndio roho ya bandari ya Dar
 
Nchi ya Mozambique imeamua kuteka biashara ya Usafirishaji Kwa njia ya Maji Kwa Nchi zote za Sadc na kuiachia Tanzania maumivu makubwa.

Katika kutekeleza Hilo, Mozambique wameamua kuikodisha Bandari Yao ya Nacala Kwa Nchi ya Malawi na Zambia ambapo wataitumia Kwa kipindi Cha miaka 100 ijayo.

Nchi hizo 3 zinapanga kujenga miundombinu ya reli kutoka Nakala Hadi Mji Mkuu wa Malawi Lilongwe na kisha Hadi Mji Mkuu wa Zambia Lusaka.

Njia hiyo Mpya ya reli itapunguza umbali wa Zambia kuifikia Bandari ya Dar hivyo zaidi ya asilimia 90% ya mzigo wa Zambia utapitia Bandari za Msumbiji za Nakala na Beira.

Kwa hatua hiyo itakuwa ni pigo kubwa sana kwa Tanzania ambayo Bandari ya Dar ilikuwa inategemea zaidi mzigo wa Nchi ya Congo DRC na Zambia kama wateja Wakuu huko Nchi zingine zikiongesea ongezea shehena.

Endapo Zambia itaondoka rasmi kuwa mteja wa Tanzania sio tuu itapunguza mzigo wa Bandari ya Dar Bali itaua kabisa biashara ya Malori ya mizigo Tanzania ambapo Kwa sehemu kubwa yatahamia Nchi hizo za Zambia,Malawi na Msumbiji na zingine za Afrika Ili kuendelea na Biashara ya Usafirishaji.
 
Soko la bandari yetu lipo, kumbuka kuwa DPW alifungua biashara yake kule Rwanda na ameshajenga depot kubwa tu ya kuhifadhi mizigo ambayo itakuja na SGR hapa TPA tayari kupelekwa huko nje. Ni biashara kubwa na Samia ametumia nguvu nyingi kuhakikisha inasainiwa mikataba ya biashara hiyo, kuna wajinga wasiojua kitu gani wanapinga na walitumiwa katika kuichafua lakini ni ngumu kushindana na mfumo wa nchi.

Hao Congo wanaweza kwenda huko Lobito. Kabla DPW hajasaini mikataba ya uendeshaji wa bandari ya Dar tayari alikwishasaini na Paul Kagame kuhusu biashara kwa upande wa Rwanda.

Hatuwezi kuwa na hofu kubwa kwa sababu misingi ya utumiaji mpana wa SGR imekwishawekwa licha ya upinzani wa wajinga wa humu humu ndani ya Tanzania.
 
Punguzeni huu unabii wa majanga, haiwezekani biashara nzima ya usafirishaji wa mizigo ya DRC ikahamia huko nacala na lobito ile ni nchi kubwa sana na nina uhakika kuna mzigo mwingi tu wa DRC utaendelea kupitia hapa TPA. Punguzeni hizi siasa za kichawi, haziwasaidii.
 
Moja ya project ya hovyo kuwah kutokea
 
Ndio tunarudi palepale shida ni uzalendo,ubinafsi huwa unakuja baada ya kukosa uzalendo.
Rwanda ni kanchi kadogo sana ila wametuzidi uzalendo tu ndio maana wanapata maendeleo kwa spidi kwa sababu kila mtu ni mzalendo kwa nchi yake na wanashirikiana kwenye mambo yote ya kiuchumi,kijamii na kiulinzi,unaambiwa Rwanda kwenye mambo ya ulinzi mitaani wako mbali sana hakuna wizi wa kijinga mitaani yaani hata ukitoka nyumba yako ukaacha milango wazi hagusi mtu na atakayejaribu kuiba ananaswa chap na kila baada ya nyumba tatu kuna afisa usalama wakati sisi huku kwetu mtu anatekwa watu wengine hawana habari.
Kwenye nchi za waarabu pia maendeleo yao yanatokana na uzalendo mtu akichaguliwa kuwa kiongozi anaijali nchi yake na kuwajali raia wengine(Dubai kila raia hata asiyekuwa na kazi wanalipwa hela kila mwezi,hela ya kodi ya nyumba,hela ya mafuta ya gari,hela ya kulipia bili kama za umeme na maji kitu ambacho hata sisi tungeweza pia kama tungekuwa wazalendo na rasilimali zetu kutumika kwa usawa)
 
Ila Zambia tutaipoteza mazima ,tutasalia na part ndogo tuu ya DRC
 
Dp world hawezi jenga bandari huko kwasababu uwekezaji wa dp world ni wa kimichongomichongo ndio maana kwenye mkataba wa bandari ya dar es salaam hakuna sehemu wanayosema watapanua hata sentimita moja zaidi ya kuleta management
 
Kilichowapeleka Mombasa ni inefficiency ya Dar Port
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…