Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port

Kwanza ukiangalia hata hii ramani hapa chini,ni wazi Nacala na Beira port zikipata reli hata Mizigo inayoenda Lubumbashi tutapoteza View attachment 3080429View attachment 3080430
Benguela railway tayari marekani ameingiza mkono anaijenga, copper ya congo kwenda USA itakuwa inasafirishwa KUTOKEA lubumbashi to Lobito by railway...ni maumivu...na KUTOKEA Dar port to Lubumbashi ni mbali kulinganiaha na Lobito to Lubumbashi. Yote hii imesababishwa na msongamano na ufanisi wa hali ya chini katika bandari za Africa mashariki
 
Tuhuma nyingi anazopewa Bashe ni hisia tu zenye kutokana na uelewa mdogo wa baadhi yetu. Siamini kwamba nia ya hiyo mipango ya kilimo ina madhara kwa uchumi mkuu wa Tanzania.
 
angola nao wamejenga reli kutoka lubumbashi hadi Lobito tayari shehena ya kwanza ya shaba kwenda us imeshawasili bandarini salama, halafu sisi tuko busy na wamasai wa ngorongoro
Mkuu, pamoja na uhasama wa sisi kwa sisi( ccm na chadema) ambao haujengi bali unadidimiza maendeleo yetu. Jamani sisi ni wamoja, tuijenge NCHI yetu.
 
Unafurahia kushindwa kwa serikali yako mwenyewe?. hizi ndizo akili za kimaskini.
Mkuu, Serikali haijashindwa kutekeleza Mipango ya Maendeleo ya Nchi; bali Chama kinacho toa SERA na BAJETI ya Maendeleo, aidha hakitoi SERA na Bajeti sahihi kwa Maendeleo ama kimekuwa dhaifu kwenye kuisimamia Maendeleo ya Nchi.
 

Ni laana ya kuivamia Zanzibar , kila kitu kitakwenda songombingo mpaka mtuwache na muombe radhi kwa mateso mliyotutia toka 1964
 
Mkuu, waandishi wetu hawawezi kumuliza Lisu maswali ambao yatamjenga yeye na wakati huo huo ana hakikisha hawaudhi walio mtuma.
 
Mizigo mingi ya hao wamiliki wakubwa wa Migodi, Kolwezi, katanga, SARL DRC inapita Dar es Salaam Port.

Hao makaburu wana train (Kalabashi)yao ya mizigo huwa inakuja Bongo kutumia Railway ya Tazara wanakuja kuleta mizigo ya kwenda China na Ulaya. Huko Msumbiji wanakwepa Challenge za usalama, watu kuiba mizigo
 
Mkuu Beira Port ipo chini ya DP World na ndio ina hudumu meli nyingi za Containers. Hiyo mizigo ya Kutoka Congo hata ikifika pale lazima iwekwe kwenye Containers iwe Copper, Cobalt,Manganese ore,Zinc,Bauxite.

Usiogope habari za mitandaoni nenda kafatilie kwenye shipping lines ni Containers ngapi zinapakia mizigo Dar kwenda Nje iliyotoka Congo. Huko Congo wenye migodi mikubwa Kolwezi,Katanga,Goma wanaleta vifaa kupitia Dar Port na wanasafirisha mzigo hapo hapo
 
Elewa mada,hizo Bandari na miundombinu yake ndio zinafanyiwa ujenzi Ili baadae zije ziweze kufanya kazi vizuri na kuwa shindani
 
Kwani dar port ipo mbona washapewa Yote DP WORLD. Mama anaupiga mwingi mno kababdari kadg hako hakawez tetemesha DP WORLD
 
Sisi tunalalamika nchi jirani zitaacha kutumia bandari yetu wakati sisi rate ya ku export ipo chini sana.

Hawa DP world tunaowalalamikia ndio wasomali wamewatumia kusafirisha refrigerated goods, Somalia kila wiki wanasafirisha meli moja ya ndizi za kuiva kwenda Italy na wao hawalimi wanazitoa Kenya. Sisi tuna matunda kibao kuanzia Nanasi,ndizi,embe,parachichi na chungwa. Ilikuwa ni suala la kumshawishi DP world aweke refrigerated terminal ya kupokea na kuzitunza zinaposubiri kusafirishwa na warehouse 1 ya kufanya packaging za perishable goods. Kuna shipping Line kama CMA CGM mwaka huu walikuwa na program ya kubeba Container za refrigerated na kuzisafirisha nje na Shipping line nyingine zingevutiwa maana uhakika wa wateja ungekuwa mkubwa.
 
Wewe unamawazo mazuri sana,ila ccm wanamawazo ya kuiba na kufisadi mali za umma,hii nchi ili ipone ni kuondoa ccm madarakani tofauti na hapo hakuna la maana litakalofanyika.
Mkuu, sisi wenyewe tunashindwa kusimamia mipango yetu: Leo stand ya mabasi ya Magufuli haina tofauti na stand zingine, kama ya Kibaha maana zote mabasi yanapita tu hadi mwisho wa safari zao za Ubungo, Urafiki, Manzese hadi Kariako n.k; siku hizi kituo cha Magufuli ni transit tu. Serikali imetumia fedha nyingi kwenye project hii, lakini matumizi yake yanafikirisha.
 
Daah umezungumza madini matupu.
 
Malawi hawana hela wala uwezo wa kujengs reli hata kilomita 20

Pili kuna tishio la vita Mozambique la magaidi ni mwehu pekee aweza Ingia kichwa kichwa kuchukua bandari Mozambique
Acha dharau za kijinga, kwani Tanzania tuna uwezo gani zaidi ya Malawi? wote wakopaji tuu na contractor ni beberu, tofauti iko wapi
 
Samia ndio anatakiwa kuwaza badala ya Wizara husika? Acha kuwa mjinga ,huo ni wajibu wa wataalamu wa Wizara za Ujenzi,uchukuzi, Usafirishaji na biashara
Kumbuka hii nchi raisi ndo muongoza njia,watendaji wanafanya kitu kwa kusikilizia maono ya raisi,nitukane mjinga ila hiki nachokwambia ndo ukweli...kuna siku nilipata bahati ya kukaa na Mkurugenzi mstaafu wa Bandari...hivi ule ujenzi wa bandari ya mkoa wa Rukwa unaendeleaje?Maana nia ilikuwa kuondoa utegemezi wa njia ya kupitia Rwanda kwenda East DRC
 
Sio kweli kazi za Wizara ni nini? Rais ni muwezeshaji tuu na mtoa Kauli ya mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…