Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port

Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port

Kwanza ukiangalia hata hii ramani hapa chini,ni wazi Nacala na Beira port zikipata reli hata Mizigo inayoenda Lubumbashi tutapoteza View attachment 3080429View attachment 3080430
Benguela railway tayari marekani ameingiza mkono anaijenga, copper ya congo kwenda USA itakuwa inasafirishwa KUTOKEA lubumbashi to Lobito by railway...ni maumivu...na KUTOKEA Dar port to Lubumbashi ni mbali kulinganiaha na Lobito to Lubumbashi. Yote hii imesababishwa na msongamano na ufanisi wa hali ya chini katika bandari za Africa mashariki
 
Kuna wakati tunalaumu viongozi ila kuna watu hata hawako Serikalini lakini wana nguvu ya kujaza ujinga kwa watanzania hadi unashangaa. Tuna akili za muda mfupi sana. Kila kitu chenye long term impact kinapingwa.

Angalia program ya BBT imavyopingwa kwa ujinga. Tutawezaji kufikia kilimo cha maana kama hujaanzisha programs za kuwa na mashamba makubwa yenye miundombinu yote. To be honest, tuna ujinga mwingi sana kama nchi.
Tuhuma nyingi anazopewa Bashe ni hisia tu zenye kutokana na uelewa mdogo wa baadhi yetu. Siamini kwamba nia ya hiyo mipango ya kilimo ina madhara kwa uchumi mkuu wa Tanzania.
 
angola nao wamejenga reli kutoka lubumbashi hadi Lobito tayari shehena ya kwanza ya shaba kwenda us imeshawasili bandarini salama, halafu sisi tuko busy na wamasai wa ngorongoro
Mkuu, pamoja na uhasama wa sisi kwa sisi( ccm na chadema) ambao haujengi bali unadidimiza maendeleo yetu. Jamani sisi ni wamoja, tuijenge NCHI yetu.
 
Unafurahia kushindwa kwa serikali yako mwenyewe?. hizi ndizo akili za kimaskini.
Mkuu, Serikali haijashindwa kutekeleza Mipango ya Maendeleo ya Nchi; bali Chama kinacho toa SERA na BAJETI ya Maendeleo, aidha hakitoi SERA na Bajeti sahihi kwa Maendeleo ama kimekuwa dhaifu kwenye kuisimamia Maendeleo ya Nchi.
 
Tanzania matahira ni wengi .
Wapo viongozi matahira, wapo wananchi matahira wa kutosha.
Kuna mambo yanahitaji akili ndogo tu kuandaa future ya Watanzania lakini hatuoni viongozi wakitumia hizo fursa kwaajili ya Tanzania ya kesho .
Sasa unatumiaje matrilioni kwa nchi maskini kama hii kujenga reli ya mwendokasi ya kubeba watu kwenda Dodoma?

Ni laana ya kuivamia Zanzibar , kila kitu kitakwenda songombingo mpaka mtuwache na muombe radhi kwa mateso mliyotutia toka 1964
 
..Lissu ana pointi nyingi za kiuchumi tatizo waandishi wa habari wamekazia kumuuliza mambo ya udaku.

..Unakumbuka darasa alilosomesha kuhusu Mgogoro wa Israel na Palestina na kila mtu ukashangaa?

..Sasa wa'challenge waandishi wamuulize kuhusu sera za uchumi ndio utajua jamaa anaifahamu dunia.
Mkuu, waandishi wetu hawawezi kumuliza Lisu maswali ambao yatamjenga yeye na wakati huo huo ana hakikisha hawaudhi walio mtuma.
 
Mizigo mingi ya hao wamiliki wakubwa wa Migodi, Kolwezi, katanga, SARL DRC inapita Dar es Salaam Port.

Hao makaburu wana train (Kalabashi)yao ya mizigo huwa inakuja Bongo kutumia Railway ya Tazara wanakuja kuleta mizigo ya kwenda China na Ulaya. Huko Msumbiji wanakwepa Challenge za usalama, watu kuiba mizigo
 
Mimi Sina tatizo na Rwanda na Burundi,hizo ni lazima watumie Dar Port Kwa sababu ndio njia fupi kwao,swala ni DRC na Zambia.

Kwa Zambia Bandari za jirani kwake ni Nacala,Beira na Lobito the same applies to DRC.

Wanatumia Dar Kwa sababu ya kukosa ufanisi kwenye Bandari hizo za Mozambique na kama ujiavyo so far wateja wakubwa wa Tanzania ni Zina na DRC
Mkuu Beira Port ipo chini ya DP World na ndio ina hudumu meli nyingi za Containers. Hiyo mizigo ya Kutoka Congo hata ikifika pale lazima iwekwe kwenye Containers iwe Copper, Cobalt,Manganese ore,Zinc,Bauxite.

Usiogope habari za mitandaoni nenda kafatilie kwenye shipping lines ni Containers ngapi zinapakia mizigo Dar kwenda Nje iliyotoka Congo. Huko Congo wenye migodi mikubwa Kolwezi,Katanga,Goma wanaleta vifaa kupitia Dar Port na wanasafirisha mzigo hapo hapo
 
Mkuu Beira Port ipo chini ya DP World na ndio ina hudumu meli nyingi za Containers. Hiyo mizigo ya Kutoka Congo hata ikifika pale lazima iwekwe kwenye Containers iwe Copper, Cobalt,Manganese ore,Zinc,Bauxite.

Usiogope habari za mitandaoni nenda kafatilie kwenye shipping lines ni Containers ngapi zinapakia mizigo Dar kwenda Nje iliyotoka Congo. Huko Congo wenye migodi mikubwa Kolwezi,Katanga,Goma wanaleta vifaa kupitia Dar Port na wanasafirisha mzigo hapo hapo
Elewa mada,hizo Bandari na miundombinu yake ndio zinafanyiwa ujenzi Ili baadae zije ziweze kufanya kazi vizuri na kuwa shindani
 
Nchi ya Mozambique imeamua kuteka biashara ya Usafirishaji Kwa njia ya Maji Kwa Nchi zote za Sadc na kuiachia Tanzania maumivu makubwa.

Katika kutekeleza Hilo, Mozambique wameamua kuikodisha Bandari Yao ya Nacala Kwa Nchi ya Malawi na Zambia ambapo wataitumia Kwa kipindi Cha miaka 100 ijayo.

Nchi hizo 3 zinapanga kujenga miundombinu ya reli kutoka Nakala Hadi Mji Mkuu wa Malawi Lilongwe na kisha Hadi Mji Mkuu wa Zambia Lusaka.

Njia hiyo Mpya ya reli itapunguza umbali wa Zambia kuifikia Bandari ya Dar hivyo zaidi ya asilimia 90% ya mzigo wa Zambia utapitia Bandari za Msumbiji za Nakala na Beira.

Kwa hatua hiyo itakuwa ni pigo kubwa sana kwa Tanzania ambayo Bandari ya Dar ilikuwa inategemea zaidi mzigo wa Nchi ya Congo DRC na Zambia kama wateja Wakuu huko Nchi zingine zikiongesea ongezea shehena.

Endapo Zambia itaondoka rasmi kuwa mteja wa Tanzania sio tuu itapunguza mzigo wa Bandari ya Dar Bali itaua kabisa biashara ya Malori ya mizigo Tanzania ambapo Kwa sehemu kubwa yatahamia Nchi hizo za Zambia,Malawi na Msumbiji na zingine za Afrika Ili kuendelea na Biashara ya Usafirishaji.
View attachment 3080432

Pia soma: Bandari za Dar na Mtwara Kuwa Mashakani Kutokana na Nchi za Zambia,Malawi na Mozambique Kuzindua Upanuzi Mkubwa wa Miundombinu ya Nacala Port.

Kwa maelezo zaidi soma hapa Ili Kuongeza Ufanisi wa reli ya TAZARA,Tanzania na Zambia Ziiombe China Wajenge reli Mpya ya Makambako-Mtwara & Kasama-Lubumbashi/Likasi

Ushauri,;

Serikali ihakikishe mipango yetu yote Kwa Sasa iwe inalenga kuikumbatia DRC kuanzia Kusini Hadi Kaskazini maana ndio mteja pekee ambae walau jiografia inatupa nafasi.

Serikali ifanye yafuatayo
1.Lazima tujihusishe na kutafuta amani directly ndani ya DRC Ikibidi Kwa gharama zetu.

2.Lazima Sgr na Barabara zivuke na kuifikia DRC(Bukavu,Goma,Kinshasa,Kindu)

3.Lazima tuwashawishi Zambia na DRC tujenge reli kutoka Tunduma-Kasama-Lubumbashi-Likasi na Kutoka Makambako-Mtwara Port.

4.Lazima Sgr itoke Mpanda-Karema na Kigoma

5.Lazima tutafute pesa za kujenga meli kubwa za mizigo na abiaria ndani ya Ziwa Viktoria na pia tujenge Bandari,Barabara na reli upande wa DRC hata Kwa kuwakomesha pesa

6.Lazima tuwape DRC,Rwanda na Burundi Ardhi za Bure za kumhudumia mizigo Yao Pwani.

My Take
Tusipofanya hayo tunaenda kupoteza hata hiyo DRC Kwa Kenya,Angola na Mozambique na ikizingatiwa DRC inajenga Bandari na reli kuunganisha na Zambia na Angola.

Washindani Wetu wa Kenya wao Wana uhakika na Uganda,South Sudan, Northern DRC na somehow Ethiopia na Rwanda.

Tuachane na Mpango wa kujenga reli ya Mtwara Corridor hiyo Haina maana tena imeshakufa,Nguvu zote zielekezwe Kujenga kioande Cha kutoka Makambako -Mtwara.
View attachment 3080431
Kwani dar port ipo mbona washapewa Yote DP WORLD. Mama anaupiga mwingi mno kababdari kadg hako hakawez tetemesha DP WORLD
 
Sisi tunalalamika nchi jirani zitaacha kutumia bandari yetu wakati sisi rate ya ku export ipo chini sana.

Hawa DP world tunaowalalamikia ndio wasomali wamewatumia kusafirisha refrigerated goods, Somalia kila wiki wanasafirisha meli moja ya ndizi za kuiva kwenda Italy na wao hawalimi wanazitoa Kenya. Sisi tuna matunda kibao kuanzia Nanasi,ndizi,embe,parachichi na chungwa. Ilikuwa ni suala la kumshawishi DP world aweke refrigerated terminal ya kupokea na kuzitunza zinaposubiri kusafirishwa na warehouse 1 ya kufanya packaging za perishable goods. Kuna shipping Line kama CMA CGM mwaka huu walikuwa na program ya kubeba Container za refrigerated na kuzisafirisha nje na Shipping line nyingine zingevutiwa maana uhakika wa wateja ungekuwa mkubwa.
 
Wewe unamawazo mazuri sana,ila ccm wanamawazo ya kuiba na kufisadi mali za umma,hii nchi ili ipone ni kuondoa ccm madarakani tofauti na hapo hakuna la maana litakalofanyika.
Mkuu, sisi wenyewe tunashindwa kusimamia mipango yetu: Leo stand ya mabasi ya Magufuli haina tofauti na stand zingine, kama ya Kibaha maana zote mabasi yanapita tu hadi mwisho wa safari zao za Ubungo, Urafiki, Manzese hadi Kariako n.k; siku hizi kituo cha Magufuli ni transit tu. Serikali imetumia fedha nyingi kwenye project hii, lakini matumizi yake yanafikirisha.
 
Suala la Bandari ya Nacaram Msumbiji na Lobito Angola ni wazo la siku nyingi la hao watu.

Bahati mbaya sana wametukuta tunachelewa kufikiria na tunafikiri na kila mtu anachelewa kufikiria kama sisi.

Kuna kitu kinaitwa Blackmailing, blackmailing hutumika pia kwenye uchumi kwenye dunia ya kimafia na kibepari.
Tungekuwa tunawahi kufikiria basi tungeshafanya blackmailing kwenye mataifa mengi ya kusini na africa mashariki upande wa LOGISTIC NA ENERGY - na hela yake ingetosha kabisa kuendesha uchumi wa hii nchi.

Unapozungumzia LOGISTIC, unaziweka Bandari tatu kama main hub, unaziunganisha hizi bandari na Bandari kavu kwenye kila border yetu, pale tunduma unaweka Dry port kubwa na mizigo yote ya kusini Destination inakuwa Tunduma dry port. Reli kutoka Mtwara port via Songea inaunga pale Makambako, unaipeleka Tunduma.
Unajenga Dry port kuubwa pale Isaka kahama kuhudumia Rwanda, Burundi na baadhi ya maeneo ya DRC kutokea ISAKA na mizigo yao yote destination inakuwa pale Isaka.
Unajenga Dry port pale Mwanza karibu ya Ziwa Victoria kuhudumia baadhi ya maeneo ya Uganda na hata Kenya nk
Serikali ihakikishe inakuwa na shipping line ya Meli za uhakika za mizigo lake Tanganyika na lake Victoria kuhudia maeneo ya Uganda na DRC kwa kuyaconnect na hizi Dry port.
Kuwe na shipping line baharini Kwa ajili ya mizigo kuanganisha Bandari zote tatu.

Kuifanya hayo yote hapo juu unapunguza gharama za ushuru ukilenga kuongeza volume na cost unazicover volume ikiwa kubwa.

Kwenye upande wa Gas na Maji, kupitia hydro plants na Gas plants tungeweza kuzarisha umeme mwingiiii na kuuza Kwa gharama nafuu Kwa majirani wote hawa kuanzia kusini, mashariki mpaka magharibi, tungewalemaza Kwa kuwauzia umeme Kwa gharama ndoogo kabisa kiasi kwamba wasingefikiria tena kuzarisha umeme wao ilihali upo umeme wa gharama nafuu kutokea Tanzania.

Hivyo vyote tungekuwa tumefanya tungekuwa tumeshawablackmail majirani woote wa ukanda huu na Taifa hili lingekuwa economic giant wa Africa.
Daah umezungumza madini matupu.
 
Malawi hawana hela wala uwezo wa kujengs reli hata kilomita 20

Pili kuna tishio la vita Mozambique la magaidi ni mwehu pekee aweza Ingia kichwa kichwa kuchukua bandari Mozambique
Acha dharau za kijinga, kwani Tanzania tuna uwezo gani zaidi ya Malawi? wote wakopaji tuu na contractor ni beberu, tofauti iko wapi
 
Samia ndio anatakiwa kuwaza badala ya Wizara husika? Acha kuwa mjinga ,huo ni wajibu wa wataalamu wa Wizara za Ujenzi,uchukuzi, Usafirishaji na biashara
Kumbuka hii nchi raisi ndo muongoza njia,watendaji wanafanya kitu kwa kusikilizia maono ya raisi,nitukane mjinga ila hiki nachokwambia ndo ukweli...kuna siku nilipata bahati ya kukaa na Mkurugenzi mstaafu wa Bandari...hivi ule ujenzi wa bandari ya mkoa wa Rukwa unaendeleaje?Maana nia ilikuwa kuondoa utegemezi wa njia ya kupitia Rwanda kwenda East DRC
 
Kumbuka hii nchi raisi ndo muongoza njia,watendaji wanafanya kitu kwa kusikilizia maono ya raisi,nitukane mjinga ila hiki nachokwambia ndo ukweli...kuna siku nilipata bahati ya kukaa na Mkurugenzi mstaafu wa Bandari...hivi ule ujenzi wa bandari ya mkoa wa Rukwa unaendeleaje?Maana nia ilikuwa kuondoa utegemezi wa njia ya kupitia Rwanda kwenda East DRC
Sio kweli kazi za Wizara ni nini? Rais ni muwezeshaji tuu na mtoa Kauli ya mwisho.
 
Back
Top Bottom