Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port

Ndio hasara ya kukurupuka na kutochukulia jambo Kwa umaskini unaotakiwa.

Stendi sio kitu Cha kuweka mabilioni bila sababu za msingi
 
umeongea point muhimu sana hatuwezi taka kila kitu kiwe kwetu, hata hiyo Lobito ni kwa ajili ya mizigo inayoenda marekani kwa maana ya kupita bahari ya atlantic ilakwa dunia ya sasa mizigo mingi inaenda asia hivyo bado hiyo copper itaendelea pita kwenye bahari ya hindi
 
mzigo wa copper unahitajika kwa wingi kwenda bara la asia kuliko marekani alichokifanya marekani ni kutaka kumuovateki mchina ili apate madini hayo kwa wingi kumbuka marekani huyo ametaka reli iunganishwe na huo mradi ili aweze kuchukua nickel iliyopo kabanga (ngara )kwenda lobito
 
-Nirahisi sana kuwa kama Kagame, na ikawaona IS kama ndugu zako!,
Chadema watu wa negativity kwa taifa watapiga nderemo na vigelegele!
 
-Nirahisi sana kuwa kama Kagame, na ikawaona IS kama ndugu zako!,
Chadema watu wa negativity kwa taifa watapiga nderemo na vigelegele!

..miundombinu sio suala la Ccm vs Chadema.

..hata tukiwa na serikali ya TLP bado miundombinu itajengwa.

..hata wakoloni walijenga reli, bandari, ambazo leo tunaziboresha.

..kwa kifupi hakuna serikali isiyojenga miundombinu. Na miundombinu sio miliki ya chama cha siasa, au kiongozi fulani.
 
Hufahamu ya kuwa serekali yetu inapopata makwazo chadema hufurahia?
 
Kuishauri serikali ya CCM ni kupoteza muda wako tu...

Hao watu hawana akili ya kuhifadhi maarifa wanayoshauriwa...
 
Hufahamu ya kuwa serekali yetu inapopata makwazo chadema hufurahia?

..Na Chadema inapopata makwazo watu wa serikali hufurahia. Je, unafahamu?

..Pia kuna baadhi ya watu serikalini wanajihusisha na matukio ya utekaji, utesaji, na mauaji, dhidi ya wafuasi wa Chadema. Je, unaunga mkono?
 
Hii habari yako ni ya uongo. Nacala port haijakodishwa kwa Malawi kwa miaka 100. Na pia haijakodishwa tu
Malawi wamepewa eneo nje la kujenga terrminal tu

Hata huku Tanzania tuna Malawi cargo, tuna Zamcargo(zambia)
 
Kwa diplomasia ya uchumi najaribu kufikiri hivi:

Ni serikali ya Malawi na Zambia ndizo zinazokwenda kuwekeza hapo Nacala ?!!

Je nchi hizo mbili zitatoa zabuni kwa makampuni ya kigeni kuwekeza hapo kwa miaka 100?!!
Hii habari ni ya uongo, bahati mbaya kabisa mmeijadili kwa ukubwa. Jf hakuna watu makini?
 
Tanzania itengeneze bomba la LPG liende Zambia, malawi, drc? Mkuu umetoa maoni pengine ya jambo ambalo hulifahamu

Unaifahamu LPG ni nn? Na Tanzania tunaitoa wapi?
 
Tanzania bado itabaki kuwa njia salama zaidi katika maswala ya Bandari kutokana na hali za kiusalama
Tuzungushe ukuta bandari zote kama mererani kuongeza usalama, tutapata wateja mpaka tububujikwe na machozi ya furaha.
 
1. Usikariri mambo hubadilika, hiyo njia uliyosema sio salama ndio kwa sasa imeomgeza importation za mizigo kwa zaidi ya 200% kupitia bandari ya Mombasa

Nchi ambayo Tz ilipaswa kuconcetrate nayo zaidi ni Uganda, hizi nchi ambazo zinapitisha mizigo yao hapa Tanzania kupitia bandari bado zote hazijafilia ukubwa wa mizigo ambayo Uganda inapitisha Kenya
 
Rwanda na Burundi lazima wapitishe mizigo yao Bandari ya Dar? Hujui tu unachosema
Rwanda kaongeza idadi ya kupitisha mizigo bandari ya Mombasa kwa zaidi ya asilimia 400%

Mizigo anayopitisha Mombasa kwa sasa imeshoot juu kabisa
 
Rwanda na Burundi lazima wapitishe mizigo yao Bandari ya Dar? Hujui tu unachosema
Rwanda kaongeza idadi ya kupitisha mizigo bandari ya Mombasa kwa zaidi ya asilimia 400%

Mizigo anayopitisha Mombasa kwa sasa imeshoot juu kabisa
Sababu ni za ufanisi na sio umbali ila kwa.kigezo Cha umbali ni lazima.

Pamoja na hayo, ukweli unabakia pale pale kwamba mzigo mkubwa wa Rwanda na Burundi unapitia Tanzania.
 
Sababu ni za ufanisi na sio umbali ila kwa.kigezo Cha umbali ni lazima.

Pamoja na hayo, ukweli unabakia pale pale kwamba mzigo mkubwa wa Rwanda na Burundi unapitia Tanzania.
Mkuu umeelewa ulichoandika mwanzo na unachoandika hapa?

Umesema Rwanda na Burundi lazima wapitishe mizigo yao Dar port, mm nimekuambia sio kweli na nikakutolea mfano kuwa Rwanda imeongeza kutumia bandari ya Mombasa kwa mizigo kwa zaidi ya 400%

Unasema ni ufanisi na sio umbali. Kwan issue ni ufanisi umbali au issue Ni Rwanda kutokua na ulazima uliosema?

Pia hii post uliyoweka kuhusu hiyo bandari kupewa Malawi kwa miaka 100 sio ya kweli. Mara nyingi nakuambia acha kuandika UONGO
 
Mama anaupiga mwingi apongezwe kwa kusaidia malawi kupitisha mizigo msumbiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…