Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port

Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port

Dp world hawezi jenga bandari huko kwasababu uwekezaji wa dp world ni wa kimichongomichongo ndio maana kwenye mkataba wa bandari ya dar es salaam hakuna sehemu wanayosema watapanua hata sentimita moja zaidi ya kuleta management
Kazi Yao sio kuwekeza kwenye miundombinu ya upanuzi Bali miundombinu ya operations kama mitambo
 
Kama hawawekezi kwenye upanuzi ndio wajenge bandari huko congo
Ile ya DRC Congo ni kama wamepewa Waanzishe from scratch,hata hivyo lazima watalazimika kupanua ya kwetu kama uhitaji utakuja maana wanatakiwa wawekeze Trilioni 2.5 Kwa miaka 5 ijayo.
 
Huu mpango ulikuwapo muda mrefu sana ukazungurushwa uka simama pale Mazabuka Zambia kuna Dry port ilikuwa imeshaanza kujengwa pale na Joseph Kabila aliichangia pesa wakati yupo madarakani ili mzigo wa DRC utue pale, hebu ngoja tutulie tuangalie wachumi wetu wana mpango gani wa kuigombania Nchi.
 
Potelea pote maana hata hiyo bandari miaka na miaka imefanya kazi lakini tunachonufaika nacho kama wananchi ni mikodi na mitozo kibao unaagiza gari japan bei M8 unakuja bandarini unaambiwa M12 sasa kuna haja ya kuwa na bandari
 
Nchi ya Mozambique imeamua kuteka biashara ya Usafirishaji Kwa njia ya Maji Kwa Nchi zote za Sadc na kuiachia Tanzania maumivu makubwa.

Katika kutekeleza Hilo, Mozambique wameamua kuikodisha Bandari Yao ya Nacala Kwa Nchi ya Malawi na Zambia ambapo wataitumia Kwa kipindi Cha miaka 100 ijayo.

Nchi hizo 3 zinapanga kujenga miundombinu ya reli kutoka Nakala Hadi Mji Mkuu wa Malawi Lilongwe na kisha Hadi Mji Mkuu wa Zambia Lusaka.

Njia hiyo Mpya ya reli itapunguza umbali wa Zambia kuifikia Bandari ya Dar hivyo zaidi ya asilimia 90% ya mzigo wa Zambia utapitia Bandari za Msumbiji za Nakala na Beira.

Kwa hatua hiyo itakuwa ni pigo kubwa sana kwa Tanzania ambayo Bandari ya Dar ilikuwa inategemea zaidi mzigo wa Nchi ya Congo DRC na Zambia kama wateja Wakuu huko Nchi zingine zikiongesea ongezea shehena.

Endapo Zambia itaondoka rasmi kuwa mteja wa Tanzania sio tuu itapunguza mzigo wa Bandari ya Dar Bali itaua kabisa biashara ya Malori ya mizigo Tanzania ambapo Kwa sehemu kubwa yatahamia Nchi hizo za Zambia,Malawi na Msumbiji na zingine za Afrika Ili kuendelea na Biashara ya Usafirishaji.
View attachment 3080432

Pia soma: Bandari za Dar na Mtwara Kuwa Mashakani Kutokana na Nchi za Zambia,Malawi na Mozambique Kuzindua Upanuzi Mkubwa wa Miundombinu ya Nacala Port.

Kwa maelezo zaidi soma hapa Ili Kuongeza Ufanisi wa reli ya TAZARA,Tanzania na Zambia Ziiombe China Wajenge reli Mpya ya Makambako-Mtwara & Kasama-Lubumbashi/Likasi

Ushauri,;

Serikali ihakikishe mipango yetu yote Kwa Sasa iwe inalenga kuikumbatia DRC kuanzia Kusini Hadi Kaskazini maana ndio mteja pekee ambae walau jiografia inatupa nafasi.

Serikali ifanye yafuatayo
1.Lazima tujihusishe na kutafuta amani directly ndani ya DRC Ikibidi Kwa gharama zetu.

2.Lazima Sgr na Barabara zivuke na kuifikia DRC(Bukavu,Goma,Kinshasa,Kindu)

3.Lazima tuwashawishi Zambia na DRC tujenge reli kutoka Tunduma-Kasama-Lubumbashi-Likasi na Kutoka Makambako-Mtwara Port.

4.Lazima Sgr itoke Mpanda-Karema na Kigoma

5.Lazima tutafute pesa za kujenga meli kubwa za mizigo na abiaria ndani ya Ziwa Viktoria na pia tujenge Bandari,Barabara na reli upande wa DRC hata Kwa kuwakomesha pesa

6.Lazima tuwape DRC,Rwanda na Burundi Ardhi za Bure za kumhudumia mizigo Yao Pwani.

My Take
Tusipofanya hayo tunaenda kupoteza hata hiyo DRC Kwa Kenya,Angola na Mozambique na ikizingatiwa DRC inajenga Bandari na reli kuunganisha na Zambia na Angola.

Washindani Wetu wa Kenya wao Wana uhakika na Uganda,South Sudan, Northern DRC na somehow Ethiopia na Rwanda.

Tuachane na Mpango wa kujenga reli ya Mtwara Corridor hiyo Haina maana tena imeshakufa,Nguvu zote zielekezwe Kujenga kioande Cha kutoka Makambako -Mtwara.
View attachment 3080431
h
k

kabisa malawi na zambia wako na hali mbaya kiuchumi ingawa pia si kuwapuuza mazima.
hizo nchi zimechoka sna afadhali ya bongo
 
We nae akili kisoda reli ile ni abiria na mizogo .....sasa ww unafikiria ...barabara za rami hujengwa kwa ajili ya mizigo au abiria na mzigo..... ndo ile reli ......tena sio dodoma sema kipande cha dodoma kimekamilika inaenda mwanza kisa mpakani rwanda
Tanzania matahira ni wengi .
Wapo viongozi matahira, wapo wananchi matahira wa kutosha.
Kuna mambo yanahitaji akili ndogo tu kuandaa future ya Watanzania lakini hatuoni viongozi wakitumia hizo fursa kwaajili ya Tanzania ya kesho .
Sasa unatumiaje matrilioni kwa nchi maskini kama hii kujenga reli ya mwendokasi ya kubeba watu kwenda Dodoma?
 
Potelea pote maana hata hiyo bandari miaka na miaka imefanya kazi lakini tunachonufaika nacho kama wananchi ni mikodi na mitozo kibao unaagiza gari japan bei M8 unakuja bandarini unaambiwa M12 sasa kuna haja ya kuwa na bandari
😀😀😀😀😀😀😀
 
h

hizo nchi zimechoka sna afadhali ya bongo
Kwani uchumi uko stagnant? Unasema zimechoka wakati hapo Mozambique wameshajenga kiwanda Cha LNG na exports imeanza,Tanzania ni stori tuu hakuna Cha maana.

Pili Mozambique hao wanaendelea na ujenzi wa kiwanda kikubwa Cha Chuma ambapo Tanzania tunaendelea na Hadithi za liganga
 
Ile ya DRC Congo ni kama wamepewa Waanzishe from scratch,hata hivyo lazima watalazimika kupanua ya kwetu kama uhitaji utakuja maana wanatakiwa wawekeze Trilioni 2.5 Kwa miaka 5 ijayo.
Hiyo trillioni 2.5 watakwambia wamewekeza kwenye management
 
😀😀😀😀😀😀😀
Mkuu usione watu wanatelekeza magari bandari unakutana na tozo hadi ya kujenga reli ina maana reli inajiendesha kwa hasara mpaka watuwekee tozo bandarini?
 
Kwani uchumi uko stagnant? Unasema zimechoka wakati hapo Mozambique wameshajenga kiwanda Cha LNG na exports imeanza,Tanzania ni stori tuu hakuna Cha maana.

Pili Mozambique hao wanaendelea na ujenzi wa kiwanda kikubwa Cha Chuma ambapo Tanzania tunaendelea na Hadithi za liganga
tatizo wabongo wengi exposure ni ndogo wanaongea sana nchi ambayo hata kununu petrol imekwama unailinganisha na tanzania
 
Ndio tunarudi palepale shida ni uzalendo,ubinafsi huwa unakuja baada ya kukosa uzalendo.
Rwanda ni kanchi kadogo sana ila wametuzidi uzalendo tu ndio maana wanapata maendeleo kwa spidi kwa sababu kila mtu ni mzalendo kwa nchi yake na wanashirikiana kwenye mambo yote ya kiuchumi,kijamii na kiulinzi,unaambiwa Rwanda kwenye mambo ya ulinzi mitaani wako mbali sana hakuna wizi wa kijinga mitaani yaani hata ukitoka nyumba yako ukaacha milango wazi hagusi mtu na atakayejaribu kuiba ananaswa chap na kila baada ya nyumba tatu kuna afisa usalama wakati sisi huku kwetu mtu anatekwa watu wengine hawana habari.
Kwenye nchi za waarabu pia maendeleo yao yanatokana na uzalendo mtu akichaguliwa kuwa kiongozi anaijali nchi yake na kuwajali raia wengine(Dubai kila raia hata asiyekuwa na kazi wanalipwa hela kila mwezi,hela ya kodi ya nyumba,hela ya mafuta ya gari,hela ya kulipia bili kama za umeme na maji kitu ambacho hata sisi tungeweza pia kama tungekuwa wazalendo na rasilimali zetu kutumika kwa usawa)
Kwa Afrika inawezekana tatizo ni kwamba shamba letu halikauki na limeshamiri vipindi vyote, kujaribu kuweka mazingira mazuri kwa watu kwa namna fulani ni kujaribu kujiondoa kwenye utegemezi, kwa namna hiyo itafanyika namna yoyote ya kuwaweka kuwa wategemezi mpaka mwisho kujinasua huko kuna hitaji mfumo na watu imara sio tuu kwa nchi yetu bali bara zima.

Ni kazi ambayo inaweza ondoka na kumbukumbu, maisha na mengine mengi ya watu
 
tatizo sio serikali ya zambia ni wanaosafirisha mizigo wanatafuta unafuu wa mizigo yao ili bidhaa ifike sokoni kwa bei nzuri wauze kwa ushindani, tukae na wenye mizigo hasa Barrick BHP Trafigura, tuweke hesabu mezani, tunahitaji watu wenye uwezo mkubwa wa ushawishi akina prof kabudi, tusiwatumie kwenda kuongea na wamasai hao tumwachie makonda, tuunde team ya wajuzi akina Kabudi Muhongo mataragio
Boresheni bandari ya mtwara, tatizo tunaongea Sana, hizi pesa tunawapa yanga na Simba please peleka kuboresha bandari
 
Kwa Afrika inawezekana tatizo ni kwamba shamba letu halikauki na limeshamiri vipindi vyote, kujaribu kuweka mazingira mazuri kwa watu kwa namna fulani ni kujaribu kujiondoa kwenye utegemezi, kwa namna hiyo itafanyika namna yoyote ya kuwaweka kuwa wategemezi mpaka mwisho kujinasua huko kuna hitaji mfumo na watu imara sio tuu kwa nchi yetu bali bara zima.

Ni kazi ambayo inaweza ondoka na kumbukumbu, maisha na mengine mengi ya watu
Nimekuelewa,mfano nauona kwa nchi ya burkinafaso Rais wao anavyowindwa na kukoswakoswa na mikasa mara kwa mara ila anakomaa kwa vile na yeye ni mwanajeshi ila kama ni raia tu wa kawaida angelegea mapema tu.
 
Umemaliza mbu wa dengue, kwa hiyo mambo ni zaidi ya haya walio kwenye nafasi nao wana jitahidi ila kuna limit kujinasua huko kunahitaji zaidi ya kujiamini kwa sababu inaweza ibuliwa skendo ama propaganda zikafanya uone kwa nini hata nilikalia hichi kiti
 
Huu mpango ulikuwapo muda mrefu sana ukazungurushwa uka simama pale Mazabuka Zambia kuna Dry port ilikuwa imeshaanza kujengwa pale na Joseph Kabila aliichangia pesa wakati yupo madarakani ili mzigo wa DRC utue pale, hebu ngoja tutulie tuangalie wachumi wetu wana mpango gani wa kuigombania Nchi.
Watu wetu wengine hawana uzalendo, TPA wana ofisi DRC na Rwanda kule kuna staff wanashindwa kuandika hata proposal ya kuomba eneo wajenge Bandari kavu Tunduma,Zambia au DRC.

DP world aliona Rwanda akiweka Logistics centre itafaa, Kagame akampa eneo akaweka miaka ya 2019
 
Back
Top Bottom