A
Anonymous
Guest
Tunapenda kuwasilisha malalamiko yetu kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhusu changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji katika eneo la Kimara Stopover, Mtaa wa Bi Mtambo (upande wa kushoto ukitokea Kimara).
Kwa muda mrefu sasa wananchi wa eneo hili tumekuwa tukikabiliwa na tatizo la kukosa maji, licha ya kupewa ratiba rasmi ya mgao. Kinachosikitisha ni kwamba hata siku zinazotajwa kuwa ni zamu yetu ya kupata huduma ya maji hupita bila maji kutoka kabisa. Hali hii imewalazimu wananchi wengi kununua maji kutoka kwenye magari ya wauzaji binafsi kwa gharama kubwa, jambo ambalo si endelevu wala halipaswi kuwa suluhisho la kudumu.
Tumejaribu kufuatilia suala hili kupitia wahandisi na mafundi wa DAWASA wa eneo husika, lakini juhudi hizo hazijazaa matunda. Mara nyingi tumekuwa tukipewa ahadi kuwa maji yatapatikana katika siku za zamu zetu, lakini ahadi hizo zimeendelea kutotimizwa. Aidha, tumeshawasilisha taarifa na malalamiko yetu mara kadhaa kwa mamlaka husika, lakini hadi sasa hatujaona hatua yoyote ya maana ikichukuliwa kutatua tatizo hili.
Changamoto hii imekuwa kubwa zaidi tangu kuanza kwa mwaka huu na ni tofauti na hali ilivyokuwa mwaka jana. Kutokana na hali hiyo, wananchi wengi wameanza kuwa na mashaka kwamba huenda kuna hitilafu au mabadiliko katika mfumo wa usambazaji wa maji wa eneo letu, jambo linalochangia kuendelea kwa tatizo hili.
Tunaiomba kwa dhati Menejimenti ya DAWASA kulichukulia suala hili kwa uzito unaostahili na kuchukua hatua za haraka kulitatua. Ikiwa itahitajika, tunaomba hata Waziri mwenye dhamana ya maji aingilie kati ili kuhakikisha wananchi wa Kimara Stopover wanapata haki yao ya msingi ya huduma ya maji.
Tumefika hatua ya kuchoshwa na hali hii. Ni jambo la kusikitisha kuona wananchi wakiendelea kuteseka na kukosa huduma muhimu kama maji katika nchi yao wenyewe. Tunaomba hatua za haraka zichukuliwe kabla hali haijawa mbaya zaidi.
Hatua zachukuliwa ~ DAWASSA: Kimara Stop Over wameanza kupata maji baada ya maboresho ya miundombinu