Mtaala mpya wa elimu, walimu jiandaeni kurudi shule

Mtaala mpya wa elimu, walimu jiandaeni kurudi shule

Kuufuta mtihani wa darasa la saba Professor Adolf Mkenda nimekupongeza na unazo sifa Za kujaza fomu 2025.

Huo mtihani ni kero, Gharama kubwa Za bure, usimbufu na ni eneo la maafisaelimu kupiga fedha Za Umma.

2. Walimu wenye diploma huko secondary warudishwe Msingi Ili kutoa mwanya kwa kuajiri wapya walimu wa sekondari wenye Degree

3. Walimu wenye cheti wapewe Muda wa miaka 2 kujiendeleza baada ya hapo wasioweza wapishe wenye diploma.

3. Baadhi ya shule Za sekondari Za kata ziwe shule Za ufundi Za kata.

3. Baadhi ya vyuo vikuu viondolewe kwenye mfumo Mfano arusha university, masomo yanayotolewa huko hayana faida kabisa kwa vijana wetu.

4. Baadhi ya Course zinazotolewa SUA ni mzigo na haxiendani na Soko la ajira zifutwe.
Mkuu Sio rahisi kama ulivyoandika hapa,itachukua miaka hata 10 kulikamilisha hili,Mimi mwenyewe Nina diploma ya ualimu,kwa muda niliokaa kazini nimefundisha shule nne kwa sasa ,shule zote unakuta walimu wa degree ni wachache kuliko diploma,ukiwaondoa hawa unaleta usumbufu.


Hii shule nilipo Mimi pekee ndo mwalimu wa kiswahili form one hadi four,sasa ukisema nitoke hii ni balaa,serikali itafanya ila kwa utaratibu mwisho wa siku kunakuwa na msawazo
 
Mkuu Sio rahisi kama ulivyoandika hapa,itachukua miaka hata 10 kulikamilisha hili,Mimi mwenyewe Nina diploma ya ualimu,kwa muda niliokaa kazini nimefundisha shule nne kwa sasa ,shule zote unakuta walimu wa degree ni wachache kuliko diploma,ukiwaondoa hawa unaleta usumbufu.


Hii shule nilipo Mimi pekee ndo mwalimu wa kiswahili form one hadi four,sasa ukisema nitoke hii ni balaa,serikali itafanya ila kwa utaratibu mwisho wa siku kunakuwa na msawazo
Of course litaenda Kwa awamu Hadi wote wasio na sifa wafikie vigezo.
 
Aisee kwo wameamua iwe bora liende kila mtu afike form four
 
Hii sera si imetamka kuwa lugha ya kufundishia ngazi zote ni KISWAHILI?
............
Huku utekelezaji tunaambiana no English no service.
Daaah.....
 
Natamani ningekua diploma Ili niende primary mwenzenu Tena Kwa Dar Primary Dili balaaa... certificate
Certificate walimu 95% hawajitambui,kooo naungamkonoo hoja ya Diploma ndio wafundishe primary.
1. Hawajali ethics za ualimu....eg.uleviii, kupiganaa mbele ya wanafunzi.
2.Waoga Sanaa,hawana constructive views zidi ya uboreshaji wa Elimu yetu. Eg: Mtu anaomba kupewa mafunzo ya kishikwambi....kha!! Inashangaza. Changamotoo zilivyoo nyiingii hivyooo nyumba mbovu,kuhamishwa pasipo malipo,,mishahara kiduchu na kuchangia et mwenge( hawayasemii).
3.Majungu,wivu kufitiniaanaaa....uwiiiii usiombee walimu wa certificate hamna tofauti na umbeya upigwao uswahiliniii....asa Hawa ndo wafundishe wannetu.#TUMECHELEWA.
 
Sijui walitumia kigezo gani
Waliofeli shule ndo wakapewa kazi ya kuelekeza Awali na msingi
 
Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na mitaala ya elimu toleo la 2023 utaanza kwa awamu mwakani, huku walimu watakaofundisha shule ya msingi wakipaswa kuwa na stashahada ya ualimu.

Akiwasilisha rasimu za sera na mitaala hiyo kwenye semina ya wabunge jijini hapo, Kamishna wa Elimu Tanzania, Dk. Lyabwene Mtahabwa, alisema katika mapendekezo ya rasimu hizo, walimu watakaofundisha elimu ya msingi itakuwa lazima wawe na stashahada ya ualimu baada ya kumaliza kidato cha sita.

Alisema kwa watakaofundisha elimu ya sekondari, ni lazima wawe na shahada ya ualimu, hivyo walimu waliopo kazini ambao hawatokuwa na sifa hawataondolewa kwenye ajira bali watapewa fursa ya kujiendeleza ili kufikia viwango.

Akitoa ufafanuzi kwa wabunge, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alisema hakutokuwa na mtihani wa kumaliza elimu ya msingi badala yake kutakuwa na mtihani wa upimaji, ili kuendelea na elimu ya sekondari ngazi ya chini.

Chanzo: Nipashe
Kipindi cha Serikali ya kubana matumizi, walikuwa wana'prefer sana Walimu wa certificate kwenye primary schools na Diploma wengi mixer na Degree kidogo kwenye Secondary schools ili kufinya mishahara.

Labda tuwaambie vijana wetu wenye certificate ambao hawapo mfumoni, sasa wakajiendeleze tu ili kuendana na kasi ya CCM.
 
Back
Top Bottom