Tangantika
JF-Expert Member
- Aug 12, 2018
- 5,586
- 7,087
Elimu ya Tanzanua mbwembwe nyingi utekelezaji sifuri. Wanabadili mitaala lakini hakuna tija yoyote.Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na mitaala ya elimu toleo la 2023 utaanza kwa awamu mwakani, huku walimu watakaofundisha shule ya msingi wakipaswa kuwa na stashahada ya ualimu.
Akiwasilisha rasimu za sera na mitaala hiyo kwenye semina ya wabunge jijini hapo, Kamishna wa Elimu Tanzania, Dk. Lyabwene Mtahabwa, alisema katika mapendekezo ya rasimu hizo, walimu watakaofundisha elimu ya msingi itakuwa lazima wawe na stashahada ya ualimu baada ya kumaliza kidato cha sita.
Alisema kwa watakaofundisha elimu ya sekondari, ni lazima wawe na shahada ya ualimu, hivyo walimu waliopo kazini ambao hawatokuwa na sifa hawataondolewa kwenye ajira bali watapewa fursa ya kujiendeleza ili kufikia viwango.
Akitoa ufafanuzi kwa wabunge, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alisema hakutokuwa na mtihani wa kumaliza elimu ya msingi badala yake kutakuwa na mtihani wa upimaji, ili kuendelea na elimu ya sekondari ngazi ya chini.
Chanzo: Nipashe
Unaanzisha mada za computer halafu shuleni hakuna umeme wala kompyuta zenyewe, huo si uhawayani.
Hakuna mahusiano yoyote kati ya diploma na elimu ya msingi, ni mbwemmbwe tu.
Elimu ya Tanzania inahitaji resource na rasilimali watu.
Mwalimu mmoja anafundisha masomo 4 na zaidi, hivi kuna tija hapo hata kama mwalimu ana digrii.