Mtaala mpya wa elimu, walimu jiandaeni kurudi shule

Diploma kufundisha sekondary sio sahihi hana tofauti na form six

Ndio.maana shule nyingi za sekondary za serikali zina matokeo mabaya sana

Private walikojaa walimu wenye digrii kuko vizuri.mno
Hahaahhahh
ivi ni kweli?????
 
Elimu ya Tz mnawapa wanasiasa wasiojitambua that way watu hupeleka watoto wao kusoma nje

Yaani kila kichaa akipata uwaziri anakuja na Ajenda na sera Mpya kuhusu Elimu yetu ...ujinga mtupu
Umepitia mchakato mzima wa maandalizi ya hiyo sera na mitaala ya Elimu au umekurupuka tuu??
 
Kweli hujielewi soma Sera ya Elimu ya mwaka 2914 kama huna nikupe nakala laini
Kijana msumbufu sana ww .. em soma hii summary ...kwa vile mvivu soma numbe 4..👇👇
MAPENDEKEZO YA RASIMU YA RIPOTI YA KAMATI YA KITAIFA YA MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU .

Na Baltazari Luhanga.

1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).

3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa Kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa shule za English medium.

5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa.

11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na
uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
-kilimo na ufugaji
-umakenika
-biashara na ujasiriamali
-sanaa bunifu
-elimu ya michezo
-ufugaji wa nyuki
-uchimbaji wa madini
-urembo

13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
-hisabati
-elimu ya biashara
-kiingereza
-historia ya Tanzania na maadili

15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
-cheti cha amali (NACTVET)

16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.

19. Coding itafundishwa shule ya msingi.

20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.

21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.

25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
-sanaa
-lugha
-muziki
-michezo
-TEHAMA

28. Masomo ya O-level yatakuwa:
-biology
-physics
-chemistry
-history
-geography
-historia ya Tanzania na maadili
-hisabati
-kiswahili
-english
-elimu ya biashara
-utunzaji wa taarifa za fedha
-computer science
-bible knowledge
-elimu ya dini ya kiislamu etc

29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.

31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

32. Walimu watakaofundisha mkondo wa amali (ufundi) watakuwa Wahitimu wa kozi mbalimbali za amali na watapewa astashahada
(cheti) ya ualimu huo kwa miezi 6.

33. Vyuo vya elimu ya juu vitaanzisha kozi za ualimu wa uandisi, urembo, uvuvi, sanaa bunifu nk. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika maeneo hayo ya ufundi.

34. Kutakuwa na internship kwa walimu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumaliza ualimu ili wawe
na umahiri zaidi. Kisha walimu watapata leseni.

35. Mafunzo kwa vitendo ya walimu tarajali yatafanyika katika shule zilizo karibu na vyuo vya ualimu ili zifanyike kwa umakini zaidi.

36. Kutakuwa na motisha kwa walimu na upandaji wa madaraja utakuwa kwa utaratibu mzuri.

37. Bodi ya usajili wa walimu itaanza kufanya kazi.

38. Utekelezaji wa mtaala mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 itaanza kwa awamu kwa darasa moja moja katika kila level. Hii itasaidia kwenda sawa na bajeti kwasababu kuanza kwa madarasa yote na levels zote ni gharama kubwa sana. Utekelezaji utaanza mwaka 2024 kama sera na mtaala zitapitishwa kama ilivyo.

Maoni yangu:

1. Kutolewe mafunzo kwa watekelezaji wa mtaala huu kwa mfano walimu, workshop instructors nk. Hii itasaidia kuendana na mabadiliko haya hasa hasa kwa walimu waliokwepo kabla ya mabadiliko.

2. Kuongeza wafanyakazi kuendana na mahitaji ya utekelezaji wa mtaala kwa mfano walimu wa kozi na masomo mapya

3. Serikali ijipange kwa upande wa bajeti kugharamia miundombinu, mishahara, vitabu, mitambo nk.

4. Career guidance iwepo kwa wanafunzi watakaochukua mkondo wa amali ili wajue ni fani zipi zinaendana na vipaji vyao, malengo yao, uwezo wao na uhitaji katika soko la ajira.

5. Wananchi waelekezwe zaidi kuhusu mabadiliko ya mtaala na fursa zilizopo pale utekelezaji wa mtaala ukianza.

Mwisho:

Naipongeza Serikali kwa maamuzi haya ya kuboresha mfumo wetu wa elimu, ambao unaenda sambamba na mabadiliko yaliyopo katika dunia ya sasa kwa kuzalisha watanzania ambao watakuwa wana utaalamu, wanajiamini, wana mtazamo chanya na wana fikra tunduizi.

Wadau tuendelee kutoa maoni yetu ili rasimu hizi ziboreshwe na ifike hatua ambayo serikali watafanya maamuzi katika utekelezaji wa sera na mtaala mpya.

Matokeo ya utekelezaji wa mtaala huu mpya na sera ya Elimu ya mwaka 2023 italeta tija na nchi yetu itaendelea kwa kasi kubwa.

Bw. Baltazari Luhanga
Mdau wa Elimu.
 
Unaongea usilolijua ww ..

Private schools never prefer graduates employee...

Nenda kesho private yeyote utakuta vijana form six...fresh kabisa wanapiga kazi..

Private shida yao content bas...
Jamaa hana ajualo anabaki kufanya uzushi,tuliosoma miaka 90- 2000 hakukuwa na walimu wa digrii lakini watu walifaulu kwa kiwango kikubwa tu,Mimi mpaka namaliza form four shuleni kwangu hakukuwa na mwalimu wa digrii
 
Msamehe bure... Labda yuko msibani.

🤭🤭😅😅
 
Diploma kufundisha sekondary sio sahihi hana tofauti na form six

Ndio.maana shule nyingi za sekondary za serikali zina matokeo mabaya sana

Private walikojaa walimu wenye digrii kuko vizuri.mno
Nmefundishwa Physics na chemistry O level na mwalimu mwenye Diploma hadi leo ni moja ya walimu bora ambao wamewahi kunifundisha, na wanafunzi wote waliokua serious tulifaulu hayo masomo vizuri sana bila kutumia nguvu nyingi

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Ikipemdeza serikali iweke daraja la promotion kwa walimu wenye masters

Ikiwa pamoja na posho ya kufundishia.

Ikiwa kweli tunataka kuboresha elimu yetu tuboreshe na maisha ya walimu.
 
Kuufuta mtihani wa darasa la saba Professor Adolf Mkenda nimekupongeza na unazo sifa Za kujaza fomu 2025.

Huo mtihani ni kero, Gharama kubwa Za bure, usimbufu na ni eneo la maafisaelimu kupiga fedha Za Umma.

2. Walimu wenye diploma huko secondary warudishwe Msingi Ili kutoa mwanya kwa kuajiri wapya walimu wa sekondari wenye Degree

3. Walimu wenye cheti wapewe Muda wa miaka 2 kujiendeleza baada ya hapo wasioweza wapishe wenye diploma.

3. Baadhi ya shule Za sekondari Za kata ziwe shule Za ufundi Za kata.

3. Baadhi ya vyuo vikuu viondolewe kwenye mfumo Mfano arusha university, masomo yanayotolewa huko hayana faida kabisa kwa vijana wetu.

4. Baadhi ya Course zinazotolewa SUA ni mzigo na haxiendani na Soko la ajira zifutwe.
Ila kiukweli elimu yetu hii ilikuwa vurugu mechi, kuna walimu niliokuwa nawajua wenye degree na walikuwa wanafundisha sekondari, ghafla been vuu nikawakuta wamehamishiwa shule za msingi!!! Kuwauliza wakasema ooh eti tumeambiwa walimu wa masomo ya arts huko sekondari tumekuwa wengi sana hivyo sisi wengine tumepunguziwa huku. Lakini katika uchunguzi wangu nikagundua huko huko sekondari walimu wenye diploma za kufundisha masomo ya arts bado wapo tuu. Sasa baada ya miaka kama 3 au 4 hivi nikakuta baadhi ya wale walimu wamehamia tena sekondari kule kule. So mimi naona huyu Prof mkenda na timu yake wamejipanga vizuri kuja na mfumo mzuri, reliable na wenye consistency na pakuanzia ni sera ya Elimu na mitaala kwa sababu mitaala ina translate SERA into action, so tuwape muda na kuombea asiondolewe hapo Wizarani ili akamilishe hilo.
 
Jamaa hana ajualo anabaki kufanya uzushi,tuliosoma miaka 90- 2000 hakukuwa na walimu wa digrii lakini watu walifaulu kwa kiwango kikubwa tu,Mimi mpaka namaliza form four shuleni kwangu hakukuwa na mwalimu wa digrii
Dunia imebadilika ya miaka hii sionya sasa
Mwalimu wa Diploma huwezi peleka hata kufundisha secondary Kenya wala hapo Uganda tu hauziki

Wa digrii aweza kwenda fundisha popote duniani

Shule za misingi na sekondari nyingi sasa hivi wanachukua walimu wenye digrii

Vyuo vyetu kitambo tu wanatoa walimu waliosomea digrii za uakimu wa chekechea,digrii za ualimu wa shule.za msingi na digrii za ualimu wa sekondary
Huo mtaala mpya kwa mwalimu wa diploma kamasi lazima zitamtoka kufundisha atajiona hayuko mahali sahihi
 
Hebu tujiulize kwa nchi zenye mifumo mizuri ya Elimu kama nchi za Scandinavians je kuna walimu wa Diploma?

Hazina walimu wenye Diploma lazima uwe na University degree ns teaching licence

Wao degree huita University Diploma

Mtu wa nje ukitaka kufundisha Scandinavian schools lazima ujue lugha yao na uwe na digrii ya education kwenye masomo husika

Bila degree hufundishi hata chekechea
 
Mkuu Sio rahisi kama ulivyoandika hapa,itachukua miaka hata 10 kulikamilisha hili,Mimi mwenyewe Nina diploma ya ualimu,kwa muda niliokaa kazini nimefundisha shule nne kwa sasa ,shule zote unakuta walimu wa degree ni wachache kuliko diploma,ukiwaondoa hawa unaleta usumbufu.

Hii shule nilipo Mimi pekee ndo mwalimu wa kiswahili form one hadi four,sasa ukisema nitoke hii ni balaa,serikali itafanya ila kwa utaratibu mwisho wa siku kunakuwa na msawazo
Lakini mtaani vijana graduates si wapo wengi mkuu? Na kama wataajiri kwa wingi kila miaka michache sidhani kama itachukua hiyo 10 yrs. To be on the safe side nashauri mjipange kujiendeleza hata kwa kusoma open university..
 
Certificate walimu 95% hawajitambui,kooo naungamkonoo hoja ya Diploma ndio wafundishe primary.
1. Hawajali ethics za ualimu....eg.uleviii, kupiganaa mbele ya wanafunzi.
2.Waoga Sanaa,hawana constructive views zidi ya uboreshaji wa Elimu yetu. Eg: Mtu anaomba kupewa mafunzo ya kishikwambi....kha!! Inashangaza. Changamotoo zilivyoo nyiingii hivyooo nyumba mbovu,kuhamishwa pasipo malipo,,mishahara kiduchu na kuchangia et mwenge( hawayasemii).
3.Majungu,wivu kufitiniaanaaa....uwiiiii usiombee walimu wa certificate hamna tofauti na umbeya upigwao uswahiliniii....asa Hawa ndo wafundishe wannetu.#TUMECHELEWA.
Hahahaaaa kufundishwa kutumia Kishikwambi?? [emoji12] [emoji12] Sasa smartphone wanatumia kuingia tiktok na Facebook siyo??
 
Kijana msumbufu sana ww .. em soma hii summary ...kwa vile mvivu soma numbe 4..👇👇
MAPENDEKEZO YA RASIMU YA RIPOTI YA KAMATI YA KITAIFA YA MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU .

Na Baltazari Luhanga.

1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).

3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa Kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa shule za English medium.

5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa.

11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na
uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
-kilimo na ufugaji
-umakenika
-biashara na ujasiriamali
-sanaa bunifu
-elimu ya michezo
-ufugaji wa nyuki
-uchimbaji wa madini
-urembo

13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
-hisabati
-elimu ya biashara
-kiingereza
-historia ya Tanzania na maadili

15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
-cheti cha amali (NACTVET)

16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.

19. Coding itafundishwa shule ya msingi.

20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.

21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.

25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
-sanaa
-lugha
-muziki
-michezo
-TEHAMA

28. Masomo ya O-level yatakuwa:
-biology
-physics
-chemistry
-history
-geography
-historia ya Tanzania na maadili
-hisabati
-kiswahili
-english
-elimu ya biashara
-utunzaji wa taarifa za fedha
-computer science
-bible knowledge
-elimu ya dini ya kiislamu etc

29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.

31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

32. Walimu watakaofundisha mkondo wa amali (ufundi) watakuwa Wahitimu wa kozi mbalimbali za amali na watapewa astashahada
(cheti) ya ualimu huo kwa miezi 6.

33. Vyuo vya elimu ya juu vitaanzisha kozi za ualimu wa uandisi, urembo, uvuvi, sanaa bunifu nk. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika maeneo hayo ya ufundi.

34. Kutakuwa na internship kwa walimu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumaliza ualimu ili wawe
na umahiri zaidi. Kisha walimu watapata leseni.

35. Mafunzo kwa vitendo ya walimu tarajali yatafanyika katika shule zilizo karibu na vyuo vya ualimu ili zifanyike kwa umakini zaidi.

36. Kutakuwa na motisha kwa walimu na upandaji wa madaraja utakuwa kwa utaratibu mzuri.

37. Bodi ya usajili wa walimu itaanza kufanya kazi.

38. Utekelezaji wa mtaala mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 itaanza kwa awamu kwa darasa moja moja katika kila level. Hii itasaidia kwenda sawa na bajeti kwasababu kuanza kwa madarasa yote na levels zote ni gharama kubwa sana. Utekelezaji utaanza mwaka 2024 kama sera na mtaala zitapitishwa kama ilivyo.

Maoni yangu:

1. Kutolewe mafunzo kwa watekelezaji wa mtaala huu kwa mfano walimu, workshop instructors nk. Hii itasaidia kuendana na mabadiliko haya hasa hasa kwa walimu waliokwepo kabla ya mabadiliko.

2. Kuongeza wafanyakazi kuendana na mahitaji ya utekelezaji wa mtaala kwa mfano walimu wa kozi na masomo mapya

3. Serikali ijipange kwa upande wa bajeti kugharamia miundombinu, mishahara, vitabu, mitambo nk.

4. Career guidance iwepo kwa wanafunzi watakaochukua mkondo wa amali ili wajue ni fani zipi zinaendana na vipaji vyao, malengo yao, uwezo wao na uhitaji katika soko la ajira.

5. Wananchi waelekezwe zaidi kuhusu mabadiliko ya mtaala na fursa zilizopo pale utekelezaji wa mtaala ukianza.

Mwisho:

Naipongeza Serikali kwa maamuzi haya ya kuboresha mfumo wetu wa elimu, ambao unaenda sambamba na mabadiliko yaliyopo katika dunia ya sasa kwa kuzalisha watanzania ambao watakuwa wana utaalamu, wanajiamini, wana mtazamo chanya na wana fikra tunduizi.

Wadau tuendelee kutoa maoni yetu ili rasimu hizi ziboreshwe na ifike hatua ambayo serikali watafanya maamuzi katika utekelezaji wa sera na mtaala mpya.

Matokeo ya utekelezaji wa mtaala huu mpya na sera ya Elimu ya mwaka 2023 italeta tija na nchi yetu itaendelea kwa kasi kubwa.

Bw. Baltazari Luhanga
Mdau wa Elimu.
Mkuu ukiulizwa ulipoandika roporopo ulimaanisha nini na hiki ulichotuma kina maudhui gani unaweza kujenga hoja kweli?
Niliandika kuwa sera ya Elimu ya mwaka 2014 ilitamka kuwa Kiswahili kitakuwa lugha ya kufundishia nwa ngazi zote.
Nioneshee hiyo roporopo hapo.
 
Hii sera si imetamka kuwa lugha ya kufundishia ngazi zote ni KISWAHILI?
............
Huku utekelezaji tunaambiana no English no service.
Daaah.....
Hebu rudia! Hata secondary? Hii ni itakuwa balaa.
 
Back
Top Bottom