Mtaala mpya wa elimu, walimu jiandaeni kurudi shule

Mkuu Sio rahisi kama ulivyoandika hapa,itachukua miaka hata 10 kulikamilisha hili,Mimi mwenyewe Nina diploma ya ualimu,kwa muda niliokaa kazini nimefundisha shule nne kwa sasa ,shule zote unakuta walimu wa degree ni wachache kuliko diploma,ukiwaondoa hawa unaleta usumbufu.


Hii shule nilipo Mimi pekee ndo mwalimu wa kiswahili form one hadi four,sasa ukisema nitoke hii ni balaa,serikali itafanya ila kwa utaratibu mwisho wa siku kunakuwa na msawazo
 
Mambo yanabadilika sana...huko tunakokwenda Walimu wa degree wataishia shule za misingi huko...Walimu wasibweteke wakipata nafasi wakasome wasiposoma kwa hiari mfumo utawalazimisha
 
Of course litaenda Kwa awamu Hadi wote wasio na sifa wafikie vigezo.
 
Aisee kwo wameamua iwe bora liende kila mtu afike form four
 
Hii sera si imetamka kuwa lugha ya kufundishia ngazi zote ni KISWAHILI?
............
Huku utekelezaji tunaambiana no English no service.
Daaah.....
 
Natamani ningekua diploma Ili niende primary mwenzenu Tena Kwa Dar Primary Dili balaaa... certificate
Certificate walimu 95% hawajitambui,kooo naungamkonoo hoja ya Diploma ndio wafundishe primary.
1. Hawajali ethics za ualimu....eg.uleviii, kupiganaa mbele ya wanafunzi.
2.Waoga Sanaa,hawana constructive views zidi ya uboreshaji wa Elimu yetu. Eg: Mtu anaomba kupewa mafunzo ya kishikwambi....kha!! Inashangaza. Changamotoo zilivyoo nyiingii hivyooo nyumba mbovu,kuhamishwa pasipo malipo,,mishahara kiduchu na kuchangia et mwenge( hawayasemii).
3.Majungu,wivu kufitiniaanaaa....uwiiiii usiombee walimu wa certificate hamna tofauti na umbeya upigwao uswahiliniii....asa Hawa ndo wafundishe wannetu.#TUMECHELEWA.
 
Sijui walitumia kigezo gani
Waliofeli shule ndo wakapewa kazi ya kuelekeza Awali na msingi
 
Kipindi cha Serikali ya kubana matumizi, walikuwa wana'prefer sana Walimu wa certificate kwenye primary schools na Diploma wengi mixer na Degree kidogo kwenye Secondary schools ili kufinya mishahara.

Labda tuwaambie vijana wetu wenye certificate ambao hawapo mfumoni, sasa wakajiendeleze tu ili kuendana na kasi ya CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…