Hizi Elimu za vyuo vikuu wanazitukuza tu % kubwa hazina impact na wanaozisoma wenyewe % kubwa ni weupe kabisa kichwani. Nadhani waliomaliza vyuo vikuu mtanisapoti kwa hili. Huko vyuoni kuna mengi ya kuboresha. Km mtu anamaliza chuo kikuu lakini ni mweupe kichwani inakuwa haina maana. Hata lugha tu ya Kiingereza ambayo ndiyo lugha ya kufundishia na kujifunzia unakuta mhitimu hawezi hata kutengeneza sentence moja. Wakati nipo chuo kikuu nimeshuhudia wanachuo wanashindwa kabisa ku-present assignments wanazopewa. Wakati wa presentation mtu ana tetemeka mwili mzima utadhani kuku wa kideli, lakini mwisho wa sku anapitia mgongo wa wenzake ktk course work na kuhitimu. Na huyo eti ndiyo tunataka awafundishe watoto wetu kisa kamaliza Diploma au Degree na GPA kubwa.
Mimi nadhani tulitakuwa tuanze na watoa hizo degree. Tatizo lililoko huko vyuoni kwa sasa limetokana na serikali kuthamini matokeo ya kwenye makaratasi(ufaulu wa vyeti) kuliko uhalisia wa mtu kichwani. Mfano eti ili uwe lecturer sharti uwe na 3.5 na kuendelea undergraduate wakati mtu anakuwa na 4.0 lakini reasoning yake na presentation of ideas are poor. Bora tungeimarisha huko kwanza kuondoa Walimu wa vyuo vikuu wenye GPA kubwa lakini kichwani wanatia mashaka na pia kudhibiti utoaji wa degree za ujanja ujanja(nimewahi kuskia vijana wakiziita degree za vyupi, sjui ni degree gani hizo).
Na niseme tu kuwa hata mambo wanayosoma kwa sasa huko vyuo vikuu wanaenda kutumia robo tu ktk ufundishaji hasa O-level. Enzi zetu Mwalimu wa degree alikuwa anafundisha A-level tu, sio km sasa eti wanafundishwa hadi Msingi. Are we serious. Sisi tumefundishwa na Walimu wa UPE na waliomaliza Elimu ya mkoloni darasa la 4 tukiwa shule ya Msingi, Walimu wa Diploma kwa O-level, na wa Degree kwa A-level na walikuwa wazuri sana hata kuliko wa sasa. Kwa nini hatujiulizi hilo na kujiuliza tulikosea wapi hadi baadae tukapata Walimu wenye uwezo hafifu.
Hivyo, tulitakiwa kupata majibu ya wapi tulipotoka, tumefikaje hapa, na tutaendaj huko mbele bila kubadilisha mtaala kwa kasi ya 4G na kuwabana Walimu kuwa na Elimu kubwa wakati application yake ktk kazi zao hata robo haifiki. Kuendelea kuthamini Elimu kubwa na GPA kubwa ni kujitekenya na kucheka wenyewe.
Sioni ulazimana wa Walimu wa shule ya Msingi kuwa na Diploma na Sekondarikuwa na degree kwa kuzingatia hayo niliyosema hapo juu. Wapo watakaonipinga lakini huo ndiyo ukweli. Kuna Walimu kibao tu Wana Elimu ya cheti au stashahda lakini wako makini na wanajuwa kuliko hao wa degree.
Km wingi wa madarasa kichwani ni utambulisho kwa mtu kuwa amesoma sana na kujua mengi mbona serikalini Elimu ya Uzamili ( Masters) kwa Walimu haitambuliki wala siyo ya lazima. Yani ukiwa nayo ni sawa na pambo tu haitakuongezea chochote ktk career yako ya Ualimu? Maanake ni kuwa mtu wa Masters kwa career ya Ualimu hana jipya tofauti na undergraduate. Na huo pia unabakia kuwa ukweli.
Nimemaliza, wale milozaliwa kwa ajili ya kupingapinga bila hoja madhubuti kazi kwenu.