Mtaalam wa Saikolojia: Mwanaume asipolia tena kwa kutoa kabisa Machozi mara Nne kwa Mwezi ajue anaukaribisha Uwendawazimu

Mfano, Baba anarudi nyumbani na hasira anapokelewa na mkewe halafu inatokea jambo dogo tu kama chumvi imezidi ndani ya mboga na hapohapo anaamua kumcharanga vibao mkewe.

Huo sio wendawazimu kwa wanaume???
Kmmk πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Kwani ule 'utafiti kuwa kila walipo Waswahili ( Watanzania ) Wanne basi Mmoja wapo ni Mwendawazimu hukuwahi Kuusikia wala Kukutana nao tu?
Najaribu kuwaza vitu wanavyovifanya wanaume vinavyofana na uwendawazimuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Inabidi mliage sana ila sasa sipati picha hali itakavyokua vilio vya wanaume vitakavyoongezeka haha
 
Kuna wale watoto waliokua wanaambiwa "acha hiyo chafu" ndio hawa mabishoo wa saizi wanaolia.

Halafu kuna wale wakina sisi "ukiona yupo kimya ujue analamba mchanga na ukimuondoa ugomvi"
 
Alietoa huu ushauri ni aidha mwanamke au mwanaume alielelewa kikeni, au ni mtu anaeamini zile fikra potofu kuwa mwanaume na mwanamke ni sawa....

Sasa mwanaume anaanzaje kulia halafu ajiite mwanaume....?!
 
Kwa taarifa yako machozi pia ni dawa ya macho, mtu unapolia yale machozi yanasafisha macho na hivyo kuyapa nguvu macho. Hiyo ni faida nyingine ya kulia.

Go and read medical journals.
Nina miaka kama 17 au 20 hivi imepita sijalia na yawezekana labda ndiyo maana hivi sasa nina Uono hafifu. Ngoja nimchokoze Mtu anipige ili Nilie.
 
Nina miaka kama 17 au 20 hivi imepita sijalia na yawezekana labda ndiyo maana hivi sasa nina Uono hafifu. Ngoja nimchokoze Mtu anipige ili Nilie.


Mkuu, kulia kwa kipigo baada ya kumchokoza mtu ni kulia kusipofaa, hakuna manufaa hapo ila moyoni kunakuwa na majonzi na msiba tu katika hali hiyo huponi kisaikolojia bali unaongeza ugonjwa wa kisaikolojia na mbaya zaidi mtu huyo akupige hadi akujeruhi na akupe ulemavu wa maisha, halikadhalika kulia kwa huzuni au kupatwa na majanga huko sio kulia kwa manufaa, mimi "NIONAVYO" (na hapa nipo huru kukosolewa), kulia kwa furaha na kulia kwa kuonyesha shukrani kwa mtu baada ya, mfano, kupewa msaada na mtu huyo.

Mimi, kama nilivyosema, huwa nalia ninapokuwa naswali katika posture ya shujuda,ninapotaka kutoa shukrani wakati huo huwa navuta hisia kwamba nipo mbele ya Mungu ili nimpe shukrani kisha huwa najaribu kutafakari kwamba; bila ya Yeye (Mungu) jambo langu lisingefanikiwa na hakukuwa na mwingine angaliweza kunisaidia isipokuwa Yeye, ninapojenga hisia kwamba hakukuwa na Yeyote angaliweza kunisaidia katika shida niliyoiepuka nk, basi jambo hilo hutia "humility" ndani ya Moyo wangu hapo machozi hunitoka na huwa natamka maneno haya "Sifa zote njema zinakustahiki wewe Mungu", kwangu hicho huwa ni kitendo cha dakika 2-3 hivi.

Katika Mazingira ya kuomba msaada kwa kulia nayo yanafanana na mazingira ya kutoa shukrani isiookuwa katika kuomba msaada maneno ninayotamka huwa; "hakuna mwingine yeyote awezaye kunisaidia isipokuwa wewe mtukufu Mwenye nguvu".

Kumbuka Mungu anazo sifa nyingi sana na anao uwezo mkubwa sana na hapa sisemi kwamba hizo dua zangu ndizo perfect sana, laahasha, mimi bado ni mtu dhaifu na ninayo mapungufu kibao bali ninajaribu kuonyesha ni jinsi gani mtu mzima anavyo weza kulia "with a fruitful purpose"

Mwisho, Mungu ni Supreme being, yeye ndiye ametuumba sote na kila kitu hivyo tukiwa mbele yake huwa zaidi ya mtoto mdogo kwa mzazi wake, yaani ulinganisho wa Mzazi kwa mtoto haufanani na ulinganisho wa Mungu kwa mtu, kama mtoto anaweza kulia mbele ya mzazi wake akiomba pipi sasa vipi mtu mzima ashindwe kulia akitoa shukrani au akiomba msaada mbele ya the most supreme being, the creator ??. Nadhani huko ndiko kulia kwa manufaa na hapo moyo hufarijika kwa furaha na raha.
 
mwanaume kulia haijakaa powaaa

waza wanaume wakijitokeza wote siku za ibada za pamoja na kuimba kwa sauti ya kutosheleza hakika watakuwa wamepunguza msongo wa mawazo na mabadiliko makubwa yatatokea

waza kwa jinsi wanavyohamasishana kwenda michezono, ama kupata bia moja baridi wangehamasishana wotee kunda nyumba za ibada
 
Sasa nawezaje kulia bila kuwa na sababu! na kulia niswala la emotion mtu linakutokea kama vile kuwa na furaha nk.. ni hisia zinakuwepo hapo, mfano mm siwezi kulia mpaka niwenajambo la huzuni kwahiyo kila week niwe na huzuni nilie πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† haya sio maisha sasa ni kalaha muda mwingine machozi ni laana mjue.
 
Wenzako huwa tunalia takriban kila siku, tukisujudi kumuomba na kumshukuru Mungu katika shida na raha zetu.

Kulia kwa "reason" na sio kulia tu.
Nyie ndo huwa mnasumbua watu Usiku wa manane kwa kulia?,Siku moja mimi nikajua kuna msiba,kumbe wazee wa kazi wanalia.Dah aisee kulia lia hovyo sijui km kweli ni agizo la Mungu.Nasisitiza kulia lia hovyo,najua kulia kupo ila sio kwa uliaji wenu .SAMAHANI MKUU km nimekukwaza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…