Mtaalam wa Saikolojia: Mwanaume asipolia tena kwa kutoa kabisa Machozi mara Nne kwa Mwezi ajue anaukaribisha Uwendawazimu

Bila shaka kuna wanaume wengi ambao huwa hawafanyi hivi(na Mimi nikiwemo ), sasa siwangekuwa wendawazimu.

Au huwa inachukua muda gani mpaka kupata huo Wenda wazimu?

Au hili swala ni jipya limeanza na hii mitano tena?...... Natania
Mkuu tutasikia na kuyaona mengi
 
Babu wa mtoa mada itakuwa ana tabia za kikekike. Kila mwezi analia mara 4 au zaidi.
 
Ukilia Lia ndio shida zinatoka? Huo ni uwendawazimu haswaaa maana huwa mnashindana kukiliza mbele ya mapasta uchwara kwenye makanisa ya ujasiliamali afu mnanyamaza yaani mnapanga dakika za kulia,huu sasa ndio wehunwenyew imagine usingekuwa unalia ingekuwaje kama sio kutembea uchi
 


Wewe umeshikwa na hasira kusikia kwamba huwa ninalia.

Je umesoma vyema nilichoandika??

Watu wanalia mbele ya watu wengine kuumba msamaha au kuomba mahitaji yao yatimizwe sembuse mimi nisilie kuomba au kutoa shukrani mbele ya Mungu aliyeniumba???.

Yesu mwenyewe na manabii wengine walilia mbele ya Mungu kuomba misaada mimi ni nani nisilie mbele ya Mungu muumba??.

Wewe sio bure bali roho yako imetawaliwa na pepo mchafu, Ibilisi.

Mungu mwenye huruma akuongoze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…