Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Dr. Mke Wangu alijufungua mwezi wa pili, baada ya kujifungua ameanza tatizo la kuumwa kiuno mara mara je tatizo ni nini.
 
ninasubiri jibu na mimi.
 
Daktari nahitaji kujua ni vidonge gani huwa vinatumika katika kupunguza stress na pia kupunguza depression??
 
Nina tatizo la miguu hasa ktk goti inalia km vijiti vinavyovunjwa hivi ...lkn pia ute ni kama haupo ...pia mifupa huniuma na miguu kuchemka au kuwa ya moto sana na maumivu makali sana...na pia nikisimama muda mrefu nashindwa kabisa ...japo sina unene wowote ...naomba unisaidie
 
 
Dr mi nauliza tatizo la mimba, mke wangu anateseka sana na hili tatizo, na tulishajaaliwa kupata watoto bila shida, ila kwa sasa tangu mimba ya mwisho ilipoharibika ukiwa na Miezi 3 akacheleweshwa kisafishwa tangu hapo sasa ni zaidi ya miaka 4 hatujafanikiwa tena, na utra sound akipimwa majibu ni kizungumkuti, kwingine unaambiwa kizazi na mirija safi, kwingine unaambiwa mirija imeziba madawa amekunywa ya kufungua mirija karibu nafungua famasi, mimi nimepima mbegu zimejaa, nisaidie la kufanya maana umri nao unatukimbia sasa hivi mke wangu Ana 42 age lakini bado anableed
 
Ninalotatizo la miaka mingi nikisumbuliwa na sub-mandibular salivary glands kwa pande zote mbili. Zinapata blockage na kuzuia mate kutoka. Niliambiwa inaweza kuwa ni stones lakini uchunguzi wangu siyo stones, tatizo ni salivary inakuwa very thick na kushindwa kutoka. nikilazimisha kwa kubonyeza glands, salivary inatoka ikiwa ngumu na wakati mwingine kama uzi.

Nitumie dawa gani?
 
Natatizo mmoja.napokuwa na lala kabla sijapata usingizi Wa jumla au nikiwa naelekea kuchukulia na usingizi.nashutuka kwa nguvu sana na hapo ndio napata usingizi nalala moja kwa moja naomba msaada nini tatizo
 


Asante sana

Dr. mimi nimeambiwa nina fat kwenye ini (utra sound). Pia nimeambiwa nina stone katika mrija mmojawapo utokao kwenye kibofu cha mkojo (ultrasound). Nipe ushauri nifanyeje.
Nilifanya hivi vipimo katika taratibu zangu za kawaida, hivyo sikuwa nasumbuliwa na tatizo lolote kabla ya hapo na mpaka sasa sihisi tatizo lolote na sijabadili utaratibu wangu wa maisha wa kawaida kwa sababu ya hayo.
 

Naomba unipelekee hizo vipimo kwenye PM.
 

Inawezekana kuwa tatizo la bladder. Tafadhali fika kwenye kituo cha afya na umuone daktari akufanyie ultrasound ya eneo hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…