Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

dr samahan hv kwenye suala la rhizhas factors ni combination gan isiyofaa kupata mtoto kwa mke na mume wakioana? je, ni +&-, blood groups, the like or

Ndiyo kama mama anayo + Na mtoto anayo - ndipo tatizo linatokea Na mama anachomwa Anti-D injection.
 
Dr inabidi uwe unatuvumilia kwa maswali.. Maana maswali mengine unauliswa ni kwa hatuna kidato hata kimoja, pengine tungekuwa nacho yangekuwa yamejibika mashule. Je Dr MTU anatakiwa kupata haja kubwa kwa wingi au kidogo?
 
MSAADA WA MATIBABU YA NGOZI

Ni zaidi ya miaka kumi sasa nasumbuliwa na tatizo muwasho katika ngozi. Nimefanya jitihada mbalimbali katika kutafuta matibabu bila ya mafanikio. Nimefanyiwa vipimo vya HIV, VDRLA na allergies lakini nashukuru katika uchunguzi wote nimekutwa sina tatizo lolote. Ila pia nimekuwa nikitumia dawa mbalimbali bila mafanikio.

Ngozi yangu ipo kawaida kabisa haina ukurutu/harara zozote. Miwasho hujitokeza zaidi mgongoni na katika sehemu za siri na wakati mwingine huambatana na hali ya unga unga. Vile vile nikitokwa na jasho hujisikia kama nachomwa/chumvi imeingia kwenye jeraha. Na hujitokeza endapo nimechelewa kuoga, mfano ikifika saa 2 usiku kabla sijaoga mwili huwasha sana, nikiwa maeneo yabaridi kama Mbeya, Arusha, nk, au kuogea sabuni zisizo na mafuta kama muarobaini au zile za magadi hivyo ngozi hukauka na kuanzisha muwasho. Sabuni pekee ambayo hunipa nafuu ni Family Medicated soap. Nikitumia aina zingine kama protex, dettol, hazisaidii kabisa.

Tangu nimepata tatizo hili naona kama mwili hauongezeki tena; uzito na ujazo wa mwili uko vile vile kwa zaidi ya miaka 10 tangu nipate hili tatizo.

Naomba usaidizi wako wa kitalamu juu ya tatizo hili.

Asante.


 
Habari mkuu.
Nina tatizo la fungas ktk vidole vya mikono na miguu,nimejaribu kutumia dawa za kumeza na kupaka lakini bado cjapata nafuu zaidi ya kupungua na kurudia hali yake ile ile.nifanye nini ili niondokane na hili tatizo.shukran
 
Habar Dr. Niliona ki uvimbe sehem ya haja kubwa nikamueleza rfk angu akaniambia niwe nachemsha maji nachanganya na detol ya maji nakanda asbuh mpka jioni kweli kile ki uvimbe kikaisha lkb sasa nina kama wiki mbili nime observe kama kuna uchafu wa maji unatoka sehem ya haja kubwa kwa mbali sana na ham ya tendo la ndoa imepungua je ni nn? Na tiba yake ni nn?
 
Habari mkuu.
Nina tatizo la fungas ktk vidole vya mikono na miguu,nimejaribu kutumia dawa za kumeza na kupaka lakini bado cjapata nafuu zaidi ya kupungua na kurudia hali yake ile ile.nifanye nini ili niondokane na hili tatizo.shukran
wakat tukimngoja dr.mume wangu aliteseka mno na hyo shida na ikawa akivua viatu kutoka kazin mpka akaoshe miguu ila dawa ilo mponyesha n kibiriti upele ndani ya siku 5 tu
 
wakat tukimngoja dr.mume wangu aliteseka mno na hyo shida na ikawa akivua viatu kutoka kazin mpka akaoshe miguu ila dawa ilo mponyesha n kibiriti upele ndani ya siku 5 tu
Hiyo dawa ndo ipi mbona siifaham
 
Uliwahi kupima minyoo?
 
Nimeshapima tena katika nyakati tofauti na sikukutwa na hilo tatizo.
Kwa ujumla hili tatizo linanitesa sana bila dalili yoyote ya kupata ufumbuzi.
Kama hauna minyoo basi, maana mm nliwahi kupatwa na tatizo hilo kipindi nakaa maeneo ya baridi kama njombe ila nlikuja kugundua ni minyoo nkapona kwa dawa za minyoo, ila usikate tamaa endelea kutafuta dawa,
Ikishindikana sana fanya hata maombi.
 
Dokta mi nimekua nikipiga punyeto kwa muda mrefu sasa uume wangu haufai hausimami kabisa na ukisimama hata kabla haujaingia kunako napizz hapo hapo na siendelei. Napoteza kumbu kumbu, sina uwezo wa kufikiri, korodani zinauma... Je naanzaje kutatua matatizo yangu?
 
Ute mweupe kama karatasi usikusumbue siyo ugonjwa ni kipindi cha ovulation na kipindi hicho ukingonoka mimba itaingia ni kipindi cha rutuba kwa mwanamke fertile period kipindi hicho utajisikia sana hamu ya kujaamiiana

Acha kuwaongopea watu wewe. Ute nyeupe pia ni dalili ya infection. Lazima kuangalia dalili zote Na kuelewa hali ya mtu kwanza. Tafadhali kama huna medical degree usipotoshe watu.
 
Dr inabidi uwe unatuvumilia kwa maswali.. Maana maswali mengine unauliswa ni kwa hatuna kidato hata kimoja, pengine tungekuwa nacho yangekuwa yamejibika mashule. Je Dr MTU anatakiwa kupata haja kubwa kwa wingi au kidogo?

Na ndiyo maana Na chukuwa muda wa kumfahamisha mtu vizuri na kikamilifu. Kupata haja kubwa mara moja kwa siku inatosha
 

Habari,

Ndiyo anaweza kupata matatizo mengi baadaye pamoja Na matatizo ya tumbo, kibofu cha mkojo Na viungo vingine.

Tafadhali fika Kituo cha Afya Na umuone daktari bingwa wa upasuaji. Usichelewe wala kudharau tatizo hili
 
Asante sana DR. Ingawa huku Lindi hizo dawa hazipo. Na kidonda kilichosababishwa na Herpes kinatibiwa na dawa gani?

Itabidi utumie dawa hizi:

1. Acyclovir 400mg. Kunywa kutwa mara mbili asubuhi Na jioni kwa muda wa miezi 3.

2. Pakaa Acyclovir cream kwenye eneo hilo kutwa mara mbili kwa muda wa mwezi 1.
 

Tumia dawa hii: Diprosalic Ointment pakaa kutwa mara mbili kwa mwezi moja alafu nipe
Mrejesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…