MSAADA WA MATIBABU YA NGOZI
Ni zaidi ya miaka kumi sasa nasumbuliwa na tatizo muwasho katika ngozi. Nimefanya jitihada mbalimbali katika kutafuta matibabu bila ya mafanikio. Nimefanyiwa vipimo vya HIV, VDRLA na allergies lakini nashukuru katika uchunguzi wote nimekutwa sina tatizo lolote. Ila pia nimekuwa nikitumia dawa mbalimbali bila mafanikio.
Ngozi yangu ipo kawaida kabisa haina ukurutu/harara zozote. Miwasho hujitokeza zaidi mgongoni na katika sehemu za siri na wakati mwingine huambatana na hali ya unga unga. Vile vile nikitokwa na jasho hujisikia kama nachomwa/chumvi imeingia kwenye jeraha. Na hujitokeza endapo nimechelewa kuoga, mfano ikifika saa 2 usiku kabla sijaoga mwili huwasha sana, nikiwa maeneo yabaridi kama Mbeya, Arusha, nk, au kuogea sabuni zisizo na mafuta kama muarobaini au zile za magadi hivyo ngozi hukauka na kuanzisha muwasho. Sabuni pekee ambayo hunipa nafuu ni Family Medicated soap. Nikitumia aina zingine kama protex, dettol, hazisaidii kabisa.
Tangu nimepata tatizo hili naona kama mwili hauongezeki tena; uzito na ujazo wa mwili uko vile vile kwa zaidi ya miaka 10 tangu nipate hili tatizo.
Naomba usaidizi wako wa kitalamu juu ya tatizo hili.
Asante.