Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Mh. Dokta ,ndugu yangu anatatizo,kapata majipu madogo madogo Sehemu za Siri na makwapani ,,ni kwa muda mrefu sasa ametumia dawa za Aina mbali mbali Lakini Tatizo ni sugu ,damu yake Ipo Safi ,,,,naomba ushauri wako na tiba pia kama Ipo .Tafadhali
 
Helo dr. Nimekuwa nikisumbuliwa sana na typhoid na amoeba inayojirudia rudia sana. Dose ya mwisho nlipewa chrolofenical vidonge 80 nikanywa nikamaliza, ila nimepata relief ya wiki moja tu na hali ikarudia vilevile. Nlienda kupimwa nikiwa shule hospitali ya apollo bangarole nako nikaambiwa siumwi kitu nitaatach hapa vipimo kama utahitaji. Serioualy nimepata stress na hii hali.pia nlipima h-pyroly nikakutwa positive nikapewa h-pyroly kit nikanywa nikamaliza na nlivyocheki ikatoka neg. Naamini sio ucleus sababu nakula kila kitu sipati shida tofauti na nyuma nlikuwa napaga gesi hadi siku tatu nikitumia vitu vya uchachu.
 
Hallow Doctor
Nilianguka na pikipiki tar 9/4/2018 asubuhi nikielekea kazini na kuumia GOTI vibaya sehemu ya joint ambapo hakuna michubuko kwa nje ila napata maumivu makali kwa ndani.
Baada ya kufika hospital nilifanyiwa x-ray siku hiyo hiyo muda wa saa nane na nusu ambapo majibu yalionyesha kuwa hakuna tatizo lolote kwenye mifupa (joint)
Nilipewa dawa ya kupaka (fastum jell) na vidonge vya maumivu (diclofenac) pamoja na kufungwa clip bandage .Docta wiki hii ni ya tatu naendelea nayo lakini bado napata maumivu makali. Hospital wanasema eti ni maumivu ya misuli ila nayahisi kama sehemu ya mfupa pia niliyogongesha inauma sana na usiku silali hata niandikapo uzi huu ni saa saba usiku.!!!
Je unanishauri nini kuhusu hili goti afadhali hata mchana ila usiku maumivu yanazidi sana. Nategemea majibu yakunisaidia, Ahsante sana.
 
Mkuu mimi pia nasubiri ujibiwe coz hatamimi nina tatizo kama lako
 
Nina tatizo la kupatwa na kwikwi inayodumu kwa muda mrefu sana(zaidi ya wiki) japo inatokea kwa takriban saa nzima na inapungua kwa muda then inaanza tena kwa wiki ama zaidi
-tatizo laweza kuwa nini (kisababishi)?
-na nifanye nini ili ipungue ama kuisha kabisa?
Asante.
 
Mimi nimepalalaizi mguu na mkono wa kulia mwaka jana machi sasa hivi naweza kutembea lakini mguu wa kulia ni mzito nauburula, nifanyeje ili mguu na mkono angalau nisiuburule mguu?
 
Group A
*Colchicine(colcrys)
Trade name(col-benemind)

*nonsteroidal ant-flamatory drugs(NSAIDs)
Trade name (brufen, indocid)

Group B
*Allopurinol (zyloprim)
(Trade name- duzallo)

*probenecid
(Trade name col-benemind )

*febuxostat

*pegloticase

ANAYEJUA DUKA LA DAWA LINALOUZA BAADHI YA HIZO DAWA MKOA WA DAR ES SALAAM IKIWEZEKANA HATA BEI YAKE NAOMBAA
 
Nina tatizo la meno kutoboka.saivi yote meno yangu yana mashimo katikati.nikila kitu cha moto sana au baridi sana.yanauma mnoo.naomba msaada.nifanyeje.na sitaki kuyatoa sababu nasikia ukitoa jino halioti tena.na mim yote magigo yangu yametoboka.sa ntakosa cha kutafunia.sijui nifanyeje.Nina umri wa miaka 20
 
Pole na majukumu ya ujenzi wa Taifa Dr. Mimi binafsi, wife anasumbuliwa sana na fangasi sehemu za siri, ni tatizo linalojirudia mara kwa mara na la muda mrefu, yapata miaka 4 sasa.
Alishafanya vipimo hospitali tofauti tofauti anapewa dawa anatumia vizuri kwa maelezo ya daktari lakini baada ya muda tatizo linajirudia tena.
Kukumbuka ni aina gani ya dawa alizokwishakutumia ni ngumu ila kuna alizokuwa anameza na zingine anaweka sehemu husika.
Nategemea msaada wako Dr.
 
Rafiki yangu anaugonjwa wakuanguka anakuwa kama kazimia alafu anahema kwa kasi nakifua kinapanda sana litakuwa ni tatizo gani?

Wengine wanasema atakuwa karushiwa pepo maana alianza kupatwa na tatizo hilo alipokuwa anasoma tanga.

Mshana Jr
MziziMkavu

msaada tafadhali.
 
Last edited:
Back
Top Bottom