Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Ijue ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona

Watu wengi wanasambaza taarifa za uwongo juu ya Corona kwenye mitandao. Kama daktari na mtafiti wa afya niliyazungumzia baadhi ya hizo taarifa hapa.​
Ukiwa na maswali zaidi kuhusu ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona, unaweza kuuliza kwenye uzi huu na nitakujibu (Tafadhali hakikisha sijajibu swali yako kwenye video zifuatazo). Chukua harakati za kujikinga dhidi ya ugonjwa huu kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya. Asante. Mungu atulinde sote.





 
Habari za kushinda doctor, doctor Nina mtoto wangu wa miaka 3 ana tatizo la kutoa harufu ukeni nimehangaika kumpeleka mahospital mbali mbali sijafanikiwa kupata huduma yoyote na hapa ninapoandika nimepanga kesho niende nae hospital nyingine naomba ushauri na njia ya kufanya ili kuondoa tatizo hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hello Dr. Sajjad
Baba yangu ni mzee wa miaka 90, uzito ni 48kg, kipindi cha baridi au akipigwa na upepo njee huwa anasumbuliwa na kifua kinapiga filimbi na kukohoa sana usiku, tukienda hospital huwa tuu wanampa dawa za kawaida za maji, kwa saivi anatumia ZECUF,ila pia alishatumia ya asili inaitwa KK kutoka dodoma.

2. hana sukari wala complication zingine tofauti na blood pressure na pressure ya macho ambazo anahudhuria clinic nakutumia dawa.

Naomba ushauri wako juu ya dawa na matunzo mazuri na sahihi kwa mzee hasa ambaye huwa mara nyingi amekaa kwani kutembea kwake nikwa shida japo anatembea mwenyewe ila kwa msaada kidogo
 
Habari za mihangaiko Dr

Nimekuja kwako nina tatizo naomba msaada wa ushauri/mawazo ya kitaalamu kuhusu Afya yangu.

Miaka mitano iliyopita nilipatwa na tatizo Kwenye kichwa, yaani ndani ya kichwa eneo la utosi Nilipatwa na mwasho mkali kwa ndani nikaanza kupakuna kadri nilivyokua napakua pakawa kama panamwga maji kwa ndani, nilipolala kuamka asubuhi nikasikia kichwa ni kizito nikakitikisa kushoto na kulia ni kama kulikua na uji mzito ndani ya kichwa ukipeleka kushoto unausikia una hamia upande huo..

Kutokana na changamoto ya kukosa pesa Ya kufanya vipimo Nilidumu na hali hiyo kama mwaka ikawa kama imeisha.

Kilichonifanya kuja kwako leo hii huo Mwasho nimeanza kuusikia tena unanikosesha Amani, Mwenye.

Natamani sana kwenda hosptal Kufanya uchunguzi ila uwezo huo sina, Ndo maana nimekuja kwako mtaalam wa Afya Unaweza kuwa Ulishakuta na Mgonjwa wa tatizo kama langu ukanisaidia kutokana na Uzoefu Wako na taaluma yako

Asante
 
Dokta wa hapa alilala mbele toka mwaka 2018 akawaacha wagonjwa wake solemba.. Wakati klinik aliifungua mwenyewe
 
Habari doctor, Mimi nina tatizo naomba unisaidie.. ngozi yangu sijui ina shida gani, nina makovu ambayo nahisi niliyapata Kuna kipindi niliugua tetekuwanga / surua.. toka 2010 huko mpaka Leo hayajawahi kuniisha, yananinyima amani sana doctor

Kingine nikiumwa hata na mbu, nikijikuna tu natoka hadi kama kidonda hvi, naomba unisaidie dawa au tiba au kipi nifanye kuondokana na hali hii, hasa haya makovu je kuna tube yoyote ya kutumia au mafuta, sabuni au dawa yoyote ile doctor..

Asante, nahitaji msaada wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habar!? Niende kwenye swal tafadhali. Mwanangu ana miez mitatu (3) na wiki 2 tangu mwez huu uanze ikifa usiku analia sana hata kunyonya hataki au ananyonya kwa shida sana.

Kwa kuuliza uliza nimegundua ni chango. Japo kimsingi bina sina ufaham kitaalam juu ya tatzo hli la chango. Kwa wataalam au wajuv tafdhal naomba kufaham juu ya hili pia tiba mana ikifika usiku hakuna kulala had alale yy hata saa usiku.

Na hapo wazaz tumetoka kazn usiku yan uchov juu ya uchov.

Naomba msaada tafadhal
 
Vidonda vya tumbo hutokana na tatizo la acidity. Ni muhimu kujuwa kwanza kama unayo acidity pekee au umeambiwa na daktari kwamba unayo vidonda vya tumbo. Kama unayo vidonda vya tumbo, unaweza kuwa na bakteria ya "H.Pylori". Madawa zake ni tofauti na mtu aliyokua na acidity pekee.

Je uliambiwa nini na daktari?
Me nilipima na kuambiwa Nina vidonda vya tumbo
 
Habari wakuu,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu magonjwa, dawa, tiba na afya kwa ujumla. Kama una maswali kuhusu ugonjwa wowote, vipi kuishi na magonjwa, kufanya mabadiliko kwenye maisha baada yakupata ugonjwa, matibabu, matumizi ya dawa, matumizi ya dawa pamoja na dawa nyingine au athari zake....

Hellow doctor!


Ndg yangu anasumbuliwa na fangasi ukeni kwa muda mrefu, ametumia anibiotics mbalimbali na dawa nyingine nyingi zikiwemo za kuinset ukeni lkn hajapata nafuu kwa maana ugonjwa huwa unaondoka na baada ya muda unarejea. Na hili limewahi hata kusababisha ujauzito kutoka.

Naomba msaada ni wapi tunaweza pata mtaalamu wa kumaliza tatizo hili sugu kwa ndg yetu maana tulianza zahanati mbalimbali za hapa tunapoishi, hospitali ya rufaa mkoa na hata baadaye tulisafiri hadi Regency hospital Dsm na bado tatizo hili halijakwisha.
Tafadhali tunaomba msaada.

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Nasumbuliwa na keloids kifuani, wapi nawezapata sindano maalumu ya kuinject dawa kwenye hizi vimbe? sindano hizi za kawaida hazina uwezo wa ku supply dawa vizuri na pia hua zinapinda. Nipo tayar kiinunua kama itapatikana.
 
Back
Top Bottom