Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Mkuu kwa case yako hapo juu ugonjwa unaosumbua vifaranga wako ni infectious coryza... ni ugonjwa ambao husababishwa na bacteria....

Hivyo basi nenda kwa duka la mifugo waambie wakupe dawa Sulfadimethoxine (Albon®, Di-MethoxTM) Na kama ukikosa hizo waambie wakupe , sulfamethazine (Sulfa-Max®, SulfaSureTM), Hiyo tetracycline hutumika sana kwa kuku ambao ni wakubwa mkuu.

Na mwisho zingatia usafi wa vyombo vya kulia chakula na maji pamoja na banda....

Nikutakie kila la kheri..... baada ya siku tano urudi hapa kuleta mrejesho......
 
miezi 4 sasa, ila kule kuugua incumbency for 21 days, si mufupa ni miteke madume mazito yanaweza kumvunja?
Hapana mkuu ondoa wasiwasi.... kabisa or kama unawasiwasi zaidi waweza kutumia Artificial Insermination
 
Mkuu hapo tatizo yaweza kuwa ni avian pox (cutaneous form) or yaweza kuwa ni ectoparasite but na imani kuku wako una wa manage vizuri.... na pia yaweza kuwa ni dermatomycosis ambao husababishwa na fungus mkuu.... pia huwa na tatizo hilo la kunyonyoka manyoya....

Thou ningepata picha ingesaidia zaidi mkuu....
IMG-20171110-WA0002.jpg
IMG-20171110-WA0001.jpg
 
Wakuu habari, leo nimeamka asubuh, nlipoingia bandan kuwahudumia bata wangu, nikakuta bata wadogo wawil wamekufa, wakat nashangaa vizuri, mmoja akaishiwa nguvu nae akadondoka, wakat naendelea kutafakar, mwngne tena amedondoka.... sijui tatzo linaweza kuwa nin?

Msaada
 
Ni wapi kati ya mikoa ya kanda ya Kati na Pengine na ziwa naweza pata ng'ombe wa kisasa wenye uwezo wa kutoa Lita kati ya 10 na 20 kwa siku? Nasisitiza hapo Daktari Lita 10 au 20!

Unajua kuna kuwa na maneno mengi ya hamasa nane nane na kwenye baadhi ya mashamba .Kuna jamaa yangu ana ng'ombe hao , hawatoi maziwa kama alivyoambiwa wakati akinunua licha ya marisho na care! Anapata 4 na iwe mapema baada ya kujifungua zinapungua kadri muda unakwenda! Ufugaji wa kibiashara nautamani, mfano unajikunja unapata ng'ombe say 4 ,Lita 10@ sawa 40 ltrs @ 1000= 40,000/ perday x 30 per month= 1,200,000/.

Huku mikoani kwa DSM ni twice. Ushauri wako tafadhali, aina gani ya ng'ombe haswa! Mpwapwa hybrid kuna jamaa yangu kachukua,aliambiwa 8ltrs perday, anapata 4 ,

Ndugu yangu naomba nisaidie hapo maana hata mimi nimepata Sana shida na Ngombe Hawa wa kununua nane nane woote niliambiwa watatoa Lita 20 kwa siku hvyo lita 10 asubuhi na Jioni

Kuna kitu tunakosea haswaa kwenye feeding hatujaweza kutumia majani sahihi ya kulisha ngombe mpaka nilipo anza kutumia Boma Rhodes na Corn Silage ndio ngombe wetu wameongeza maziwa hadi lita 7 au 8 kwa mkamuo tena hao ni Wale chotara yaani mixed breed ya fresian na Ayrshire niliwanunua Arusha sasa kichekesho ni kwamba niliagiza ngombe 10 pure breed ya Fresian kutoka Netherlands Nika ambiwa watatoa lita 18-25 kwa siku walipofika Dar maana woote walikuja kwa ndege wakiwa na mimba ya miezi 6-8 kwa sasa woote wamezaa lakini tatizo kubwa ni kwamba ngombe hao hawana uwezo wa kustahimili joto juu ya 25 degrees Celsius yaani siku ikizidi hapo wanapata heat stress na maziwa wanatoa lita 10 tuuu kwa siku yaani imekua hasara kubwa sana kwetu maana tuliwanunua million 7 kila ngombe hadi kufika Dar kupitia SouthAfrica
 
Naomba msaada nimeamka Leo kwa bwawa lang Nime kuta samaki wang baadh wame kufa cjw Nn tatizo
Mkuu ningekuwa karibu na wewe ningeweza kufika hapo katika shamba lako na kuweza kufanya PM ambayo ingeniwezesha mimi kujua nini tatizo but waweza niambia maji ya bwawa lako la samaki yan hali gani mkuu?
 
Baadae kidogo nitaweka makala hapa namna ya kuweza kujitengenezea chakula chako cha kuku mwenyewe ili kuepuka gharama zisizo na msingi.....
Mkuu nina kitoto cha mbuzi umri wiki nne. Kimeugua ghafla miguu haina nguvu, kinatetemeka ovyo hata kunyonya hakiwezi na shingo inajipinda kurudi nyuma kama mgonjwa wa meningitis. Huu ni ugonjwa gani mkuu, na tiba yake ni ipi?!
 
Back
Top Bottom