Nimeamini! Mtandao wa mafisadi nchini, mwenye kuuvinja sio mfano wa Magufuli tena, anapaswa awe ni mtu katili kuliko Hitila, mwenye sura mbaya kuliko Idd amini dadaa
Kila Mtanzania kwa sasa, hahitaji kuuliza kwa mwenzake kuhusu ufisadi ulivyokithili sasa, watu wako bize kuiba kiasi hata Mh Rais akijisahau haya majizi yanaweza kuondoka na pochi yake
Watu ambao wamejikusanya kuandika kitabu cha kumchafua Magufuli, ndio hao waliokuwa wakitafutwa wakihusishwa na wizi wa mali za watanzania wengi wao wakakimbilia nje ya nchi
Wasomi uchwala hao, wameandika kitabu kinachohusu serikali ya Magufuli ilivyowekeza katika mji wa Chato ambapo ni sehemu ya Tanzania.
Mantiki yao ni ipi haswa!
Hata iweje, aandike vitabu na vitabu, bado Magufuli hawezi kuchafulika kijinga!
Zaidi, soma: From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)