Nimeamini! Mtandao wa mafisadi nchini, mwenye kuuvinja sio mfano wa Magufuli tena, anapaswa awe ni mtu katili kuliko Hitila, mwenye sura mbaya kuliko Idd amini dadaa
Kila Mtanzania kwa sasa, hahitaji kuuliza kwa mwenzake kuhusu ufisadi ulivyokithili sasa, watu wako bize kuiba kiasi hata Mh Rais akijisahau haya majizi yanaweza kuondoka na pochi yake
Ni Magufuli pekee aliyeipandisha hadhi nchi yetu, ni yeye pekee aliyeibua miradi kedekede na isiyohesabika, miradi ya kimkakati na kuileta nchi katika uchumi wa kati mdogo! Hivi utamdanganya nani?
Ni Magufuli pekee aliyekuwa na huruma ya dhati kwa wananchi wote hasa wa chini, aliwajali na kutatua kero zao bila kuogopa wenye ukali
Ni serikali yake tu, iliyotaka kuondoa tabaka la walionacho na wasiokuwa nacho,
Wanatufanya kwamba wote tulikuwa chekechea siyo?
Halafu wasomi uchwala hao waliondika daftari Lao hilo, wote wako nje ya nchi na hawataki kurudi,
Hata hivyo, kwa nini wanaitumia nguvu nyingi kiasi hiko? Na ukichunguza zaidi, unagundua tu kwamba, miongoni mwa walioshiriki ni pamoja na waliotemwa kwenye nafasi za uteuliwa utawala wa Magufuli
Hata hivyo, mbona bado ni walewale vilaza na mafisadi?
Watu ambao wamejikusanya kuandika kitabu cha kumchafua Magufuli, ndio hao waliokuwa wakitafutwa wakihusishwa na wizi wa mali za watanzania wengi wao wakakimbilia nje ya nchi
Wasomi uchwala hao, wameandika kitabu kinachohusu serikali ya Magufuli ilivyowekeza katika mji wa Chato ambapo ni sehemu ya Tanzania.
Mantiki yao ni ipi haswa!
Hata iweje, waandike vitabu na vitabu, nyinyi wasomi uchea, tunachukua nafasi hii kuwakumbusha sisi wamachinga, wafanya biashara, wamama ntilie, wananchi wa kawaida, tunawakumbusha tu kwamba, Magufuli hawezi kuchafuliwa na yeyote kwa njia yoyote ile!
Tutaendelea kuguswa na yale ametufanyia kama nchi na wananchi!
Magufuli! Lala salama!
Kuna wajinga wachache wanadhani eti ni rahisi tusahau mema uliyotuachia!