Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu zako wamekufa wangapi au jirani zako
Kusema ukweli kabisa kutoka moyoni, sijawahi kuona msiba mtaani kwangu tena ni Mwananyamala uswazi kabsaaaa. Hata mimi naona mauzauza tu. Wanakufa viongozi. Nadhani serikali ingechunguza. Yaweza kuwa kuna kitu hakiko sawa mahali. Sabotage inaweza kuwa iko kazini.Mtaa unaoishi halo ilivyo ipoje? Mtaani kwetu unaweza kujua hakuna ugonjwa huu kabisa. Karibia kila kitu kinaendelea kama hamna kitu, watu wanaishi maisha yao bila wasiwasi (mikusanyiko na vijiwe) kilichobadirika ni ndoo za maji mtaani ambazo hazitumiwi.
Watu wanaishi maisha yao na kata yetu yote sijasikia mtu kafa kwa Corono au kahisiwa. Ila ukiingia mitandaoni jinsi wanavyoeleza hali ni tofauti na uhalisia. Unaweza kudhani watu wanakufa sana au wako hoi sana mitaani.
Je hali ya mtaani kwenu ipo vipi.?
Ndugu zako wamekufa wangapi au jirani zako
Corona haipo,mwambieni basi yule mzee aliyejificha kule kijijini arudi huku town aendelee kuchapa kazi.Tanzania kila kitu hewa, Corona hewa, wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa,
Corona imebakia jina Tu Tanzania, Huku kwetu kila ninayekutana naye, anaulizia tu, hivi wamefika wangapi? Sasa endapo kila mtu atakuwa anauliza wamefika wangapi, unagundua kabisa hii Corona haipo, kama ingelikuwepo, basi hata hao wanaouliza watu kufika wangapi wangekuwa nao wanaugulia!
Corona hewa