Mtaani kwenu kuna Tahadhari dhidi ya CoronaViruses?

Mtaani kwenu kuna Tahadhari dhidi ya CoronaViruses?

Juzi kulitokea msiba huku kitaa chetu...kuna mbaba fulani alidondoka tu ikabidi wamkimbize hospitali na akafariki muda mchache baada ya kufika hospitali...Basi kutokana na tukio lilivyokuwa watu wakaanza kudai ni #covid19...Watu tukapuuza tukajua ni maneno ya khanga tu tukaenda msibani kama kawaida japo tunachukua tahadhari kama kunawa na pia walioenda ni wachache hivyo social distance tukaizingatia...Kumbe taarifa haikupuuzwa bhana,ilisambaa mno hadi serikali ikaingilia kati.Saa tatu usiku akaja mwenyekiti na polisi fukuza wote pale ikabaki familia tu...,Wengine tukaambiwa tusubiri majibu ya #covid19...Basi usiku huo baada ya tukio hilo ni kama petroli iliongezwa kwenye moto,wengine wakajihakikishia kabisa,Asubuhi ni #covid19,..#covid19....Saa nne tukapata majibu,kilichomuua marehemu ni Presha na Kisukari....Na sio #covid19...Tukarudi msibani wachache,tukafanya taratibu zinazofanyika na baadaye tukaelekea malaloni..,Mambo yakaisha.
 
Kutoka mwanza Huku mtaani kwetu maisha yanaendelea kama kawaida hamna corona wala covid, watu tunaendelea na harakati tu, mimi nafanyia kazi mjini kati harakati zinaendelea fresh tu.
 
Mtaa unaoishi halo ilivyo ipoje? Mtaani kwetu unaweza kujua hakuna ugonjwa huu kabisa.

Karibia kila kitu kinaendelea kama hamna kitu, watu wanaishi maisha yao bila wasiwasi (mikusanyiko na vijiwe) kilichobadirika ni ndoo za maji mtaani ambazo hazitumiwi.

Watu wanaishi maisha yao na kata yetu yote sijasikia mtu kafa kwa Corono au kahisiwa. Ila ukiingia mitandaoni jinsi wanavyoeleza hali ni tofauti na uhalisia.

Unaweza kudhani watu wanakufa sana au wako hoi sana mitaani.

Je hali ya mtaani kwenu ipo vipi.?

Kachukue buku saba yako Lumumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio wote wanaopata Corona wanakufa

Back
Top Bottom