Mtaani ni mwendo wa kupishana na costal za maua tu, tunachimba tunazika

Mtaani ni mwendo wa kupishana na costal za maua tu, tunachimba tunazika

Course Coordinator

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2019
Posts
1,742
Reaction score
3,224
Habari za Jumamosi

Haya mambo haya ndani ya wiki mbili hizi hatujazoea, kupishaha na magari sana sana coastal zenye waombolezaji kiasi hiki, barabarani unaweza kupishana na coastal zilizobeba miili ya wafu zaidi ya 9 kwa siku, hali hii sikuizoea kabisa.

Unaweza kujiuliza kuna ajali gani ilitokea hivi karibuni ikaua ndugu zetu, jamaa zetu, marafiki zetu kiasi hiki hizi maiti zinasombwa wapi ,je hii ni Brazil, au Italia ya 2020 tuliokuwa tunaisikia au ni kuna Boko Haramu siku hizi Tanzania inaua ndugu kwa kuvizia.

Ila ukiona waombolezaji wanaosindikiza miili ya wapendwa wao wote wamevaa barakoa ndo unashituka aaah kumbe kuna ugonjwa wa homa ya mapafu Tanzania (Pneumonia)...basi unaendelea na safari zako, unajiuliza tu kimya kimya sijui wanaenda wapi, sujui ni akina nani, msiba usije ukafika ukaambiwa ni flani kafa ila tu hukupati taarifa mapema.

Ndugu zanguni tujilindine,tusisubiri mamlaka husika ikuambie jilinde na uchukue tahadhari,wabunge wamesema hosptali zimejaa ukienda unaumwa Neumonia kuna mawili ama usubirie mgonjwa ampone au usubirie mgonjwa afe ndo upate Oxygen, unaambiwa hata kwa kuhonga rushwa hupati Oxygeni

Mtu atakayeugua na apate mashine ya oxygen ni wale VIP class no 1.
Mfano augue RC na Waziri augue pneumonia wewe unadhani nani atapata hiyo mashine ya Oxygen haraka ?.

Tuachane upuuzi wa kusema Pneumonia inaua wazee wa miaka 60 na watu wanene ,huo ni ujinga wa kutokuelewa afya.
Tuacheni ujinga wa kusema Pneumonia inaua sehemu ya baridi tu.
Tuacheni ujinga wa kusema Pneumonia tujifukize itaisha ,tunywe malimao tangawizi Sijui vitunguu.
Lini kichomi na homa ya mapafu iliisha kihivyo,dawa zote za asili hufanya kazi taratibu sana .

Unapomchukua mwanamke ujikinge na magonjwa ya zinaa kama UKIMWI serikaki iliwahi kukutuma ununue kondom ?
Ulipopata maradhi ya zinaa serikali ilikuuliza kwa nini hukutumia kondom sana sana si daktari atakushauri ujikinge na uwakinge wengine ?

Sasa kwenye hili la pneumonia si hao hao wataalam wa afya wametushauri tuvae barakoa na kufanya social distance.

Unapokufa familia yako itakulilia itagharamikia mazishi yako wachinje ng'ombe.
Wakifa wao serikali ndo inabeba misiba yao,peps na cocacola watapeleka soda na maji ya dasani,kilimanjaro na Azam atapeleka unga wa maandazi,Mtibwa na Kagera Sugar atapeleka sukari kwa ajili ya chai.

Tuchukue tahadhari ,jana nimetoka kumzika ndugu yangu Professa wa miaka 48 hasara kwa familia kisa pneumonia inauma.

Wao wanaumwa sisi tunaumwa ,hatuna BIMA wao wanazo,hatuna lishe wao wana mafungu,hatuna STK,SU,STL,SL,RAC,sisi tunategemea kukodisha coasta.

Bwana awasaidie wale wote wanaopigania UHAI wote mahospatalini na majumbani kwa ugonjwa wa Pneumonia na magonjwa mengine.

Tujilinde tujikinge ,tuwalinde tuwakinge.

Jumamosi iliyo Njema kwa wote.
 
Nenda marekani watakuonesha maelfu ya makaburi mapya kila siku.

Yani wewe unashangaa hapa kupishana na costa?

Wenzio wanabeba kwenye malori.
Alaf mtu analumu serikali 🤣🤣 sasa sijui serikali ifanye nini kwenye ugonjwa ambao hauna dawa ....
 
Ni kweli mimi jana nilipishana misiba miwili ndani ya coaster halafu ndani wamevaa barakoa wote,kuna mtu nikamuuliza ambaye ana duka maeneo ya barabarani akasema kwa siku inapita minne hadi mitano.
 
shida hata baadhi ya watu waliopatiwa chanjo huko ughaibuni bado msisitizo ni ule ule wavae barakoa wanawe mikono na keep distance that mean that vaccine is useless
Chanjo haikufanyi usiambukizwe bali ni kinga ya ugonjwa ukiupata usidhurike...wangap wana chanjo ya suruwa na waliugua suruwa,wangapi wana chanjo ya TB na waliugua TB.
Note.Marekani ina watu milioni 300+ waliopigwa chanjo hadi sasa ni milioni 21 tu.
 
Majibu ya serikali na wapambe Mbuzi ni mepesi tu, "Kwani zamani watu walikuwa hawafi?"
Huwa akili za MATAGA hadi wafe wao ,ndo maana mbunge kafa kwa pneumonia wakaambiwa ni ajali ya gari.
Yani Mbunge apate ajali,Tz hii inyamaze tusione hilo gari lilivyoharibika ,tusisikie dereva wake kafa ama kapona ,tusijue hata eneo ambalo alipatia ajali.
 
Chanjo haikufanyi usiambukizwe bali ni kinga ya ugonjwa ukiupata usidhurike...wangap wana chanjo ya suruwa na waliugua suruwa,wangapi wana chanjo ya TB na waliugua TB.
Note.Marekani ina watu milioni 300+ waliopigwa chanjo hadi sasa ni milioni 21 tu.
of koss wangapi wana chanjo ya polio na lepros na wamepata tena
 
Unaweza kupewa chanjo ukiwa na virusi tayari
shida hata baadhi ya watu waliopatiwa chanjo huko ughaibuni bado msisitizo ni ule ule wavae barakoa wanawe mikono na keep distance that mean that vaccine is useless
 
Inatisha, lakini watu bado wabishi sana
Ni kweli mimi jana nilipishana misiba miwili ndani ya coaster halafu ndani wamevaa barakoa wote,kuna mtu nikamuuliza ambaye ana duka maeneo ya barabarani akasema kwa siku inapita minne hadi mitano.
 
Tusaidiwe takwimu za birth rate na death rate kwa miezi sita iliyopita

Kuna Dr humu alitoa ushuhuda kwamba awamu ya 5 ukitoa takwimu sahihi inakula kwako lazima utoe takwimu zinazoendana na JIWE anavyopenda....Kama mtu ana TB inabidi usema ana kikohosi ,Uviko unasema Nimonia ,HIV damu imechafuka etc

Ukitaka kujua hali halisi angalia idadi ya coaster zenye maua au nenda Biafra kaulize biashara kwa sasa ya coaster ipoje? Watakwambia Ukweli.
 
Back
Top Bottom