Mtaani ni mwendo wa kupishana na costal za maua tu, tunachimba tunazika

Mtaani ni mwendo wa kupishana na costal za maua tu, tunachimba tunazika

Alaf mtu analumu serikali 🤣🤣 sasa sijui serikali ifanye nini kwenye ugonjwa ambao hauna dawa ....
Acheni mambo ya hovyo kwenye mambo yahusuyo uhai wa watu,serikali haina mkazo wowote kwenye issue ya Corona,
Raisi anakusanya watu Morogoro kwakuzindua machine yakukoboa mpunga akijua kabisa mikusanyiko si salama kutokana na uwepo wa korona.
Tulitarajia raisi yeye angetoa ushauri namna bora yakujikinga na korona lakini anayoyafanya ni tofauti.
Kuna jambo serikali haiko sawa kwenye mapambano dhidi ya korona.
 
shida hata baadhi ya watu waliopatiwa chanjo huko ughaibuni bado msisitizo ni ule ule wavae barakoa wanawe mikono na keep distance that mean that vaccine is useless
Hapana hapa umekosea kidogo chanjo wanapata mbili baadhi ya nchi sasa ya kwanza tu hawaja cover watu wengi wameshasema ikifika majority wamepata chanjo hapo ndio watalegeza masharti lakini kwa hivi sasa hata UK wametangaza wagonjwa na vifo number zinashuka kila siku kwa hiyo trend inaenda chini. Logistic imekuwa shida kidogo ili kuhakikisha chanjo zinafanywa kwa haraka nadhani ikifika nusu mwaka number ya chanjo ikiongezeka tutaona. WHO wamesema kwa ujumla number zinashuka na UK wamesema wagonjwa wamepungua wenye kuhitaji msaada.
 
Nenda marekani watakuonesha maelfu ya makaburi mapya kila siku.

Yani wewe unashangaa hapa kupishana na costa?

Wenzio wanabeba kwenye malori.
NI kweli, lakini kule wanaambiwa kwamba kuna janga kwenye nchi yao, wajikinge; hiyo ndio tofauti ya wao na sisi
 
Hii Corona, ukiona Hadi Who wameishiwa matamko, jua hata hizo kelele za mitandaoni hazisaidii, ukiweza kujilinda jilinde, na mbaya kabisa wale wenye chanjo zao NAO Bado wanavaa barakoa
 
Acheni mambo ya hovyo kwenye mambo yahusuyo uhai wa watu,serikali haina mkazo wowote kwenye issue ya Corona,
Raisi anakusanya watu Morogoro kwakuzindua machine yakukoboa mpunga akijua kabisa mikusanyiko si salama kutokana na uwepo wa korona.
Tulitarajia raisi yeye angetoa ushauri namna bora yakujikinga na korona lakini anayoyafanya ni tofauti.
Kuna jambo serikali haiko sawa kwenye mapambano dhidi ya korona.

Wewe umechukua hatua gani kuepuka jambo hilo pamoja na familia yako?
Maana kujikinga ni hiyari, au aunataka serikari itumie nguvu kwa mtu mwenye akiri timamu kama wewe na familia yako?
Serikali imeshasema tuchukue tahadhali sasa unataka mpaka usukumwe?

1 epuka kchangama na watu
2 vaa barakoa muda wote
3 nawa mikono kila mara
4 kaa distance kuanzia ndani mwako
5 Jifungie ndani (lockdown )

Chukua hatua wewe mwenyewe kuishi ni manufaa yako mwenyewe, na kama police watakufata huko ndani basi njoo ulalamike hapa.

Kwa pamoja tupunguze ma costa barabarabani.
 
Hii Corona, ukiona Hadi Who wameishiwa matamko, jua hata hizo kelele za mitandaoni hazisaidii, ukiweza kujilinda jilinde, na mbaya kabisa wale wenye chanjo zao NAO Bado wanavaa barakoa
Kwa mwanaume mwenye akili hawezi kuacha kuvaa kondomu kwa mwanamke aliyekutana naye siku ya kwanza hata kama kampima Ukimwi muda huo huo.
 
Chanjo haikufanyi usiambukizwe bali ni kinga ya ugonjwa ukiupata usidhurike...wangap wana chanjo ya suruwa na waliugua suruwa,wangapi wana chanjo ya TB na waliugua TB.
Note.Marekani ina watu milioni 300+ waliopigwa chanjo hadi sasa ni milioni 21 tu.
Shida ni kwamba wengi wa tunaojadiliana humu, upeo na uelewa wao ni mdogo sana.
 
Acheni mambo ya hovyo kwenye mambo yahusuyo uhai wa watu,serikali haina mkazo wowote kwenye issue ya Corona,
Raisi anakusanya watu Morogoro kwakuzindua machine yakukoboa mpunga akijua kabisa mikusanyiko si salama kutokana na uwepo wa korona.
Tulitarajia raisi yeye angetoa ushauri namna bora yakujikinga na korona lakini anayoyafanya ni tofauti.
Kuna jambo serikali haiko sawa kwenye mapambano dhidi ya korona.
Raisi alisema shughuli za serikali zitaendelea kama kawaida , Ila chukueni tahadhari mmoja mmoja , mkuu hakuna aliyeshurutishwa aende kwenye huo mkutano , swali la kujiuliza unaendaje kwenye mkutano huku ukijua kuna Korona ?? Kaa nyumbani , jipige rockdown, tumia sanitizer , vaa barakoa , ..uhai wako huwezi kumbebesha mtu mwingine ...
Kama unahitaji chanjo nenda ulaya kapigwe chanjo urudi .....!! Mwaka jana serikali ilisisitiza hayo unayoyataka ni nini tulifaidika? Zaidi ilileta taabu ya kiuchumi mpak hotel za Naura Arusha kudorora na sasa inabid ziuzwe kufidishia madeni Kwa wafanyakazi ....ugonjwa hauna dawa , kila mtu ni roho mkononi around the globe...
 
Kwa mwanaume mwenye akili hawezi kuacha kuvaa kondomu kwa mwanamke aliyekutana naye siku ya kwanza hata kama kampima Ukimwi muda huo huo.
Ni mwanaume mpumbavu pekee anayeenda dukani anunue kinga wakati mwili wake umevalishwa kinga
 
Raisi alisema shughuli za serikali zitaendelea kama kawaida , Ila chukueni tahadhari mmoja mmoja , mkuu hakuna aliyeshurutishwa aende kwenye huo mkutano , swali la kujiuliza unaendaje kwenye mkutano huku ukijua kuna Korona ?? Kaa nyumbani , jipige rockdown, tumia sanitizer , vaa barakoa , ..uhai wako huwezi kumbebesha mtu mwingine ...
Kama unahitaji chanjo nenda ulaya kapigwe chanjo urudi .....!!
Yaani swala la Afya unataka Raisi aseme kitu ha ha haaaaa
Ukienda Ulaya kupigwa chanjo ukirudi unaambiwa "watanzania wanaenda Ulaya kuchanjwa na kuleta corona ya ajabu ajabu"
 
Ukienda Ulaya kupigwa chanjo ukirudi unaambiwa "watanzania wanaenda Ulaya kuchanjwa na kuleta corona ya ajabu ajabu"
Unaenda alaf unarudi unatangaza kwamba nimeenda kupigwa chanjo 🤣... ukifanya hvo lazima upigwe segerea wiki mbili ukila pumba na maji ... Yesu alisema kuwa mpole kama njiwa na uwe mjanja kama Nyoka....
 
Huwa akili za MATAGA hadi wafe wao ,ndo maana mbunge kafa kwa pneumonia wakaambiwa ni ajali ya gari.
Yani Mbunge apate ajali,Tz hii inyamaze tusione hilo gari lilivyoharibika ,tusisikie dereva wake kafa ama kapona ,tusijue hata eneo ambalo alipatia ajali.
Wakianza kufa wao ,mpaka lockdown tutapigwa mkuu
 
Unaenda alaf unarudi unatangaza kwamba nimeenda kupigwa chanjo 🤣... ukifanya hvo lazima upigwe segerea wiki mbili ukila pumba na maji ... Yesu alisema kuwa mpole kama njiwa na uwe mjanja kama Nyoka....
Hahahahahahahah.
Kwani walioenda walitangaza ,si tulisikia tu Meko anawataja.
Ukiona Cocorico ipo muulize
Dr Abas
Athumani Diwani
Kamishina wa Magerza
Mkuu wa Uhamiaji
Yani inawala hapo mhimbili na Lugalo balaa.
 
Tanzania's own Hotel California

"Hotel California"

On a dark desert highway, cool wind in my hair
Warm smell of colitas, rising up through the air
Up ahead in the distance, I saw a shimmering light
My head grew heavy and my sight grew dim
I had to stop for the night
There she stood in the doorway
I heard the mission bell
And I was thinking to myself
"This could be Heaven or this could be Hell"
Then she lit up a candle and she showed me the way
There were voices down the corridor
I thought I heard them say

Welcome to the Hotel California
Such a lovely place (Such a lovely place)
Such a lovely face
Plenty of room at the Hotel California
Any time of year (Any time of year)
You can find it here

Her mind is Tiffany-twisted, she got the Mercedes bends
She got a lot of pretty, pretty boys she calls friends
How they dance in the courtyard, sweet summer sweat
Some dance to remember, some dance to forget

So I called up the Captain
"Please bring me my wine."
He said, "We haven't had that spirit here since nineteen sixty nine."
And still those voices are calling from far away
Wake you up in the middle of the night
Just to hear them say

Welcome to the Hotel California
Such a lovely place (Such a lovely place)
Such a lovely face
They livin' it up at the Hotel California
What a nice surprise (what a nice surprise)
Bring your alibis

Mirrors on the ceiling
The pink champagne on ice
And she said "We are all just prisoners here, of our own device"
And in the master's chambers
They gathered for the feast
They stab it with their steely knives
But they just can't kill the beast

Last thing I remember
I was running for the door
I had to find the passage back to the place I was before
"Relax," said the night man
"We are programmed to receive
You can check-out any time you like
But you can never leave!"
 
Acha ujinga...
Hekaya za kipumbavu
Habari za Jumamosi

Haya mambo haya ndani ya wiki mbili hizi hatujazoea, kupishaha na magari sana sana coastal zenye waombolezaji kiasi hiki, barabarani unaweza kupishana na coastal zilizobeba miili ya wafu zaidi ya 9 kwa siku, hali hii sikuizoea kabisa.

Unaweza kujiuliza kuna ajali gani ilitokea hivi karibuni ikaua ndugu zetu, jamaa zetu, marafiki zetu kiasi hiki hizi maiti zinasombwa wapi ,je hii ni Brazil, au Italia ya 2020 tuliokuwa tunaisikia au ni kuna Boko Haramu siku hizi Tanzania inaua ndugu kwa kuvizia.

Ila ukiona waombolezaji wanaosindikiza miili ya wapendwa wao wote wamevaa barakoa ndo unashituka aaah kumbe kuna ugonjwa wa homa ya mapafu Tanzania (Pneumonia)...basi unaendelea na safari zako, unajiuliza tu kimya kimya sijui wanaenda wapi, sujui ni akina nani, msiba usije ukafika ukaambiwa ni flani kafa ila tu hukupati taarifa mapema.

Ndugu zanguni tujilindine,tusisubiri mamlaka husika ikuambie jilinde na uchukue tahadhari,wabunge wamesema hosptali zimejaa ukienda unaumwa Neumonia kuna mawili ama usubirie mgonjwa ampone au usubirie mgonjwa afe ndo upate Oxygen, unaambiwa hata kwa kuhonga rushwa hupati Oxygeni

Mtu atakayeugua na apate mashine ya oxygen ni wale VIP class no 1.
Mfano augue RC na Waziri augue pneumonia wewe unadhani nani atapata hiyo mashine ya Oxygen haraka ?.

Tuachane upuuzi wa kusema Pneumonia inaua wazee wa miaka 60 na watu wanene ,huo ni ujinga wa kutokuelewa afya.
Tuacheni ujinga wa kusema Pneumonia inaua sehemu ya baridi tu.
Tuacheni ujinga wa kusema Pneumonia tujifukize itaisha ,tunywe malimao tangawizi Sijui vitunguu.
Lini kichomi na homa ya mapafu iliisha kihivyo,dawa zote za asili hufanya kazi taratibu sana .

Unapomchukua mwanamke ujikinge na magonjwa ya zinaa kama UKIMWI serikaki iliwahi kukutuma ununue kondom ?
Ulipopata maradhi ya zinaa serikali ilikuuliza kwa nini hukutumia kondom sana sana si daktari atakushauri ujikinge na uwakinge wengine ?

Sasa kwenye hili la pneumonia si hao hao wataalam wa afya wametushauri tuvae barakoa na kufanya social distance.

Unapokufa familia yako itakulilia itagharamikia mazishi yako wachinje ng'ombe.
Wakifa wao serikali ndo inabeba misiba yao,peps na cocacola watapeleka soda na maji ya dasani,kilimanjaro na Azam atapeleka unga wa maandazi,Mtibwa na Kagera Sugar atapeleka sukari kwa ajili ya chai.

Tuchukue tahadhari ,jana nimetoka kumzika ndugu yangu Professa wa miaka 48 hasara kwa familia kisa pneumonia inauma.

Wao wanaumwa sisi tunaumwa ,hatuna BIMA wao wanazo,hatuna lishe wao wana mafungu,hatuna STK,SU,STL,SL,RAC,sisi tunategemea kukodisha coasta.

Bwana awasaidie wale wote wanaopigania UHAI wote mahospatalini na majumbani kwa ugonjwa wa Pneumonia na magonjwa mengine.

Tujilinde tujikinge ,tuwalinde tuwakinge.

Jumamosi iliyo Njema kwa wote.
 
Back
Top Bottom