Mtaani vijana wanaharibika kwa ulevi

Mtaani vijana wanaharibika kwa ulevi

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
34,181
Reaction score
41,563
Mimi ni mzee wa miaka 42 ila huwa kujichanganya, hapa nipo kijiwe hapa Dsm, aisee hatima ya vijana. Vijana wamechoka mbaya bora sisi wazee wa kati ( 40 - 55).

Kijana wa miaka 20 sura imepinda ni nini hiki? Taifa hili tusipokiwa makini nguvu kazi hii inakwenda kupotea.

Wadau wenzangu na nyie fanyeni utafiti huko mliko lakini kama hali ndo hii hatuna Taifa, tunakwendaje kujenga nchi na mateja?

Yaani hapa ni kuka, konyangi za kolabo vijana wa kike wa kuume, yaani kuna umoja wa ajabu, afu cha ajabu na mie washaniona teja mwenzao...napewa kuka ila aisee kuka ni kifo cha figo zako.

Hali ni mbaya.

Ni mimi mpiga sumari ..
 
Mwaka jana nilikwenda kumsalimia bi mkubwa wangu kitaani kwetu Tmk, sasa napiga misele nasikia vibinti vya shule age 15-17, vinamsema mwenzao ni mshamba kisa hampi boyfriend wake tigo, nilichoka mno, hao boyfriend wao wenyewe ndio wale madogo waliosokota nywele jioni wanaimbisha singeli kwenye vigodoro.
 
Shida ni kubwa ndio, ila nadhani ni mchakato wa nature kujirestore yenyewe.
Haiwezekani kundi kubwa kuwa tegemezi hadi kufanya wale wanaotegemewa nao kuwa tegemezi!

Lazima kuwe na mlingano.

Baba awe kwa wazazi alafu nae mjukuu amtegemee babu? Hapana kwakweli japo hawajataka lakini ni lazima mapepe yapeperushwe
 
Mimi ni.mzee wa miala 42 ila huwa kujichanganya, hapa nipo kijiwe hapa Dsm, aisee hatima ya vijana.....vijana wamechoka mbaya bora sisi wazee wa kati ( 40 - 55)

Kijana wa miaka 20 sura imepinda ...ni nini hiki? Taifa hili tusipokiwa makini nguvu kazi hii inakwenda kupotea.

Wadau wenzangu na nyie fanyeni utafiti huko mliko lakini kama hali ndo hii hatuna Taifa...tunakwendaje kujenga nchi na mateja?

Yaani hapa ni kuka, konyangi za kolabo vijana wa kike wa kuume, yaani kuna umoja wa ajabu, afu cha ajabu na mie washaniona teja mwenzao...napewa kuka ila aisee kuka ni kifo cha figo zako.

Hali ni mbaya.

Ni mimi mpiga sumari ..
WAPIGA KURA......
 
Watu wa aina hii wako kwenye jamii zote,sio jana leo wala kesho,wapo tu..
Mazingira pia ni changamoto, kuna mtaa niliishi Morogoro, vijana niliokuwa nao labda ni wawili ama watatu wana nafuu, wengine wote wamelost.
Mzee mwenzangu pia ziko sehem ukitembelea utaona vijana wamenyooka,nadhifu,afya njema na wanamaendeleo sana...
 
Back
Top Bottom