Mtaani vijana wanaharibika kwa ulevi

Ccm mbere kwa mbere
 
VIjana wa sasa wamekata tamaa ndio hao wanasema Mungu hayupo , hawaoni faida ya maisha šŸ˜€ šŸ˜€ šŸ˜›
 
Mzee wa 42? Wewe ni kijana hata hujafika 40 ndio maana 42 unaita mzee.
 
Miaka 42 bado kijana mdogo kabisa. Uzee ni kuanzia miaka 60 nakuendelea.
 
Mzee unavijua visungura?

Wiki ilopita hapo nimekutana na kijana wangu kachoka, kakongoroka, mkangafu ngalangala.
Niliumia sana kwa kweli.
Eti ngalangala🤣🤣🤣
 
Mtaani kwetu yaani tunatumia mjumbe mmoja, mwaka huu tu tumewapoteza vijana watatu na wote walikuwa na uhusiano mzuri na pombe kali za bei rahisi.
 
Wazazi baadhi hawapendi kuwawajibisha watoto wao wakiwa wadogo,yaani mzazi anaishi na mtoto yake utafikiri ataishi nae milele,kumbe miaka michache baadae Kila mtu atakuwa anapambana mwenyewe,Sasa huwo wakati ndio kijana anajikuta hawezi kujisimamia mwenyewe.
 
Hali ngumu ya maisha ndio chanzo Cha hayo yote kutokea.
Vijana wamesoma ila hata internships Hakuna.
Hawana mtaji wa kuanzishia hata kabiashara kadogo unadhani Nini kinatokea?

Ulevi wa kupindukia,ngono zembe,mimba za mapema pamoja na magonjwa ya zinaa.

Hakika kizazi Cha Sasa kinapitia changamoto nyingi Sana.
 
Mimi nina miaka 45 ni kijana ww una miaka 42 unajiita mzee!!??

Mbona una kiherehere na uzee!
 
Du tmk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…