Mtaani wizi umeshamiri sana, nini kifanyike?

Mtaani wizi umeshamiri sana, nini kifanyike?

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Hali ya usalama mikoa mbalimbali sio nzuri! Wizi ni kama umerudi kwa kasi sana, sasa hivi usalama wetu na mali zetu uko mashakani sana!

Hata hapa JF kila siku lazima ukutane na nyuzi za watu kuibiwa hiyo ni ishara tosha kuwa hali ni tete.

Jeshi la Polisi liko wapi? IGP Sirro yuko wapi? Mbona wakati wa hayati JPM mambo yalitulia, wapi tumekosea? Nini kifanyike?
 
Siku zote wizi upo? Maana sasa hivi utasikia, Mzee fulani asingetangulia tusingeibiwa!
 
Siku zote wizi upo? Maana sasa hivi utasikia, Mzee fulani asingetangulia tusingeibiwa!
Bila kujali nani ni rais lakini wizi unapozidi mitaani siyo jambo zuri. I hate siasa na wanasiasa wa Tanzania kwa sababu huwa wanajipa credit wasizostahili.

Jambo la lahiri ni kuwa jeshi la polisi ni jeshi hovyo sana na limeacha kufanya kazi zake za msingi na kujiingiza kwenye siasa uchwara, kitu kinachofanya lipoteze muda na resources nyingi kuipigania CCM.

Hii imefanya hata watala kushindwa kuwawajibisha viongozi wa polisi utendaji unapokuwa chini ya kiwango kwa sababu wanakuwa wanalipa fadhila zao kwa hao viongozi wanapotuka.

Kilichotokea wilaya ya Hai ni mfano hai. Ilikuwaje Sabaya afanye uhalifu namna hiyo huku jeshi la polisi lipo?
 
Hali ya usalama mikoa mbalimbali sio nzuri! Wizi ni kama umerudi kwa kasi sana, sasa hivi usalama wetu na mali zetu uko mashakani sana!

Hata hapa JF kila siku lazima ukutane na nyuzi za watu kuibiwa hiyo ni ishara tosha kuwa hali ni tete.

Jeshi la Polisi liko wapi? IGP Sirro yuko wapi? Mbona wakati wa hayati JPM mambo yalitulia, wapi tumekosea? Nini kifanyike?
Uyo Magufuli ndo alikuwa anateua mpaka majambazi katika nafasi za ukuu wa wilaya na mkoa, mtu kama sabaya alikuwa anavamia mchana kweupe lakini mlifumba macho leo hii mnaleta nyuzi za ajabu
 
Yule Kamanda Moroto atoe karipio wataogopa na kuacha.
 
Wizi upo awamu zote, acheni kumpa pressure mama yetu.

Mali zako ni zako binafsi, usipozilinda tunaiba.
 
Wahuni sio watu,wamenipiga tukio asubuhi hii,banda la kuku wamekomba lote ,hadi vifaranga
 
Bila kujali nani ni rais lakini wizi unapozidi mitaani siyo jambo zuri. I hate siasa na wanasiasa wa Tanzania kwa sababu huwa wanajipa credit wasizostahili. Jambo la lahiri ni kuwa jeshi la polisi ni jeshi hovyo sana na limeacha kufanya kazi zake za msingi na kujiingiza kwenye siasa uchwara, kitu kinachofanya lipoteze muda na resources nyingi kuipigania CCM. Hii imefanya hata watala kushindwa kuwawajibisha viongozi wa polisi utendaji unapokuwa chini ya kiwango kwa sababu wanakuwa wanalipa fadhila zao kwa hao viongozi wanapotuka. Kilichotokea wilaya ya Hai ni mfano hai. Ilikuwaje Sabaya afanye uhalifu namna hiyo huku jeshi la polisi lipo?
Kusema jeshi la Polisi lina mapungufu ni sawa lakini kusema limeacha kufanya kazi zake na wewe ni kupiga siasa pia.

Je, ukipata tatizo linalohitaji Polisi leo e.g kupotelewa na mtoto, hautaenda?! Si hawapo wameacha kufanya kazi yao.
 
Uyo Magufuli ndo alikuwa anateua mpaka majambazi katika nafasi za ukuu wa wilaya na mkoa, mtu kama sabaya alikuwa anavamia mchana kweupe lakini mlifumba macho leo hii mnaleta nyuzi za ajabu
Punguza stress
 
Back
Top Bottom