Nimejifunza kwamba miongoni mwa skills nzuri sana kuwa nayo maishani ni composure. Ni kawaida sana kwa mtu alienacho kuwaona wasionacho kwamba kuna sehemu wanakosea, ni kawaida yetu binadamu.
Nimesoma comments zote za huyo jamaa sio tu kwenye uzi huu, hata kwenye uzi wangu wa kuomba kazi. Nilichogundua kutoka kwake ni kuwa yeye ni aina ya watu wanaofikisha ukweli mchungu ambao wengi wetu hatupendi ama hatuko tayari kuusikia hasa ukizingatia mtu kama mtoa mada aliekaa darasani kwa takribani miaka 19 kuitafua hio master's aliyonayo.
Shida ipo sehemu moja tu, angesoma vizuri story ya mtoa mada angeona ni kwa jinsi gani amepambana na bado anaendelea kupambana bila kukata tamaa.
Angesoma vizuri angetambua kwamba sio rahisi kubadilisha imani ya mtu alietumia miaka yote hiyo na gharama kubwa katika kutafuta kitu na mambo yakaenda tofauti na alivyodhania na kumtaka atumie mbinu mbadala kwa dhihaka.
Angesoma vizuri angetambua kwamba mtoa mada kashasema alipata shida ya mgongo kwa kufanya vibarua hivi hivi ambavyo yeye anashauri kwa dhihaka mtoa mada avirejee.
Kuna wakati mwingine mtu unatakiwa kujifunza tu ku'skip kitu ambacho unaona kitakufanya utoe kauli za kuumiza binadamu wengine.
Brother mtoa mada ana master's degree ya PA, if all goes well, siku akabahatika kukamata ofisi ya serikali, kipi kimfanye awe mnyenyekevu kwa watu ambao walikua wakimdhihaki wakati hana hio nafasi?
Anyway, ngoja tu tuukubali ukweli mchungu kutoka kwa wanaodiriki kutubeza kwamba elimu haijatusaidia kitu na hatujishughulishi kwakua hatuna maarifa mbadala ya kuishi. Tutazivumilia dharau na masimango yote huku tukitumainia kesho yetu.
And if a day ever comes and the tables turn, I hope we will be humble enough not to take vengeance. Ninachojua ni kwamba inaweza isilete matokeo ya haraka, ila elimu haijawahi kukosa faida. Wacha muda uamue.