Mtaji wa 46M faida 540,000, pia mtaji wa 45M faida 576,000

Ndugu biashara ni somo ambalo watanzania wengi hawakufaulu Kuna nyuzi nyingi sana za kuomba mawazo ya biashara gani mtu afanye na anaeomba ana mtaji mkubwa tuu lakini ushauri uliomo inabidi tufikirie kuoa mchaga tuu huenda ukapata wazo zuri la biashara.

1. Jingalie kama wewe ni mtu wa biashara maana biashara unahitaji kujituma kujinyima na ukauzu vinginevyo utarudi kuwa omba omba, zipo biashara unaweka pesa hata 10m lakini profit yake kwa mwezi ni zaidi ya 3m.

Ila Kuna hizi biashara unaweka 20m upate faida 300k kama huna pesa ukafanya inaitwa biashara kichaa ila kama pesa unayo na unafanya hii inaitwa biashara ya kitajiri yaan unainvest Ili pesa Yako isipotee yaan izunguke lakin kimaisha ushafanya Kila kitu na bank kuko vizuri Hizi wanaofanikiwa ni matajiri sababu wanakuwa na target za mauzo kwa kiwango flan hivyo faida anayopata kwenye mauzo sio kitu yeye anasubiri robo mwaka apate incentive yake Bado anakuwa anasaidiwa transport ila kwa mtu ambae hajui anaiga anaumia anaishia kusema lazima kuloga ndio ufanikiwe.

2. Kama wewe sio mtu wa biashara basi tafuta mtu alie kwenye biashara Jenga urafiki nae wa kibiashara kubaliana nae muwekeze pamoja uwe unapata gawio zuri au mfanye awe meneja wako we Mpe Target atakupambania hapo akipata Zaidi usitamani na akikosa usisikilize stori zake, jali pesa Yako.

Tajiri anaspend to invest, maskini ana invest kuspend
 
Hiyo pesa ingiza kwenye Mazao utakuja kunishukuru. Yaani 46M inakuletea laki Tano halafu unapata usingizi?
Kweli wenye michongo hawana pesa na wenye mitaji hawana michongo.

Hiyo pesa unapaswa kuwa imeidabo ndani ya miezi sita na kwa mwaka Uwe na 100M. Ingiza chaka Acha kukaa mjini na pesa yote hiyo inazeeka tu.
 
Tafuta biashara nyingine hiyo ni risk kubwa sana yaani faida ni asilimia 1.3 ya mtaji then unaipata ndani ya miezi miwili are you serious?
 
Ushauri wako ni upi niingie ktk biashara zipi
 
Chaka kama wapi nikapige Moshe gani
 
Location nzega...ila nawaza vitu pia kuagiza labda kuuzia mtandaoni
Mtandaoni kwa Nzega sijui. Ila kwa retail ya vinywaji vikali na pombe ukiwa supplier wa eneo lako hela na mzunguko unapata. Sifa kuu ya Watanzania ni uvivu, umbea, ulevi na pombe.

Makampuni ya mitandao, wauza simu, wamiliki wa clubs na bar, wamiliki wa kampuni za pombe, wenye mahoteli na lodges wote wametumia udhaifu huo.

Mambo mengine yanategemea ukoje, elimu, umri, muda, ukali na ukorofi, akili, etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…