Ni hivi ukubwa wa mtaji kwenye uwakala inategemea na eneo la biashara yako. Unaweza kuwa na mtaji wa million 10 ila kutokana na eneo ulilofungua biashara ukajikuta hela iliopo kwenye mzunguko ni million 3, kwahyo million 7 ikawa ipo tu imeka.
Najua kinachokumiza kichwa unataka kila mteja akija kwako kutoa au kuweka hela basi apate huduma, achana na hayo mawazo. Huwez kuhudumia wateja wote. Unaweza kuwa na mtaji wa million 10 ila kuna siku atakuja mteja wa kutoa laki 1 na hutakiwa nayo. Unajua kwann? Kuna siku utajikuta hela zimeja kwny simu na ww huna cash.
Million 5 inatosha kabisha kufanya kazi. Binafsi nikiaza hii kazi na mtaji wa laki 7, na niliaza kufanya huduma za kibank mtaji ulisoma kama 3. Sio kila mteja wa bank anatoa hela nyingi, wapo ambao wanatoa mpaka elfu 5. Utawahudumia wateja ambao una uwezo nao, wale wa miamala mikubwa wataenda sehemu nyingine.
Kingine hiyo Kodi ni kubwa sana kwa kuanza uwakala. Maeneo yapo mengi. Sio lazima mjazane mjini wote.