Revolution
JF-Expert Member
- Feb 28, 2008
- 960
- 927
Wandugu Habari za leo,
Ninapenda kutoa pendekezo hapa ambalo wadau watakaovutiwa nalo watatoa michango yao ya ku-modify zaidi wazo langu. Kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu ni dhahiri sasa watu wengi wanafanya shughuli za maendeleo kwa pamoja. Kinachatakiwa hapa ni willingness, trust, commitment na creativeness.
Kifupi ninatafuta vijana kumi mpaka kumi na tano, lets say kuanzia miaka 20 hadi 45 ambao tunaweza kuweka mitaji ( mali, nguvu, muda na akili) yetu pamoja na kuanza kufanya miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji, biashara ya kununua, kuweka na kuuza, au biashara nyingine ambayo itaweza kusimamiwa na wajumbe na ikawa ni ya mafanikio makubwa (Ila binafsi ninapendelea zaidi kilimo- kwasababu kikifanywa kwa ufanisi na ueledi kinaweza kuwalipa wajumbe wote kwa kiwango cha juu).
Mimi nipo Dar es salaam hivyo ningefurahi ningepata wajumbe wataokuwa interested kutoka Dar ama la wajumbe wanaweza kutoka mikoani as long as kutakuwa na namna nzuri ya kukutana sehemu ya uzalishaji. mathalani, shambani.
Wazo langu ni kupata wajumbe hao kumi mpaka kumi na tano, kufungua kampuni brela kwa kuisajili, kuomba sehemu ya ardhi kubwa lets say kama ekari 3,000 na kuendelea katika serikali ngazi ya wilaya au taifa kama wawekezaji wa ndani. Lakini kabla ya hapo wajumbe tutakaopatikana tutaanza na kujichanga kwanza kwa mwaka mmoja au mmoja na nusu- ambapo kila mjumbe atatakiwa kuchangia kuanzia Tshs 10,000,000 na kuendelea kwa mwaka kutokana na hisa tutakazoziestablish.
Mnakaribishwa wanaume kwa wanawake, pia mawazo zaidi yanakaribishwa. Naomba wachangiaji walio serious wachangie kama kuna mapungufu yaboreshwe.
WanaJF wanaotaka hii kitu na wanaopenda maendeleo waniPM ili tuanze mchakato wa kutafutana.
NB: Matapeli hawatakuwa na nafasi katika hili.
Nawasilisha.