xfactor
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 1,511
- 1,289
Mkuu Revolution tunakuomba urudi kwenye uzi wako huku.
Kama unamaanisha ulichokiandika, basi natuanze sasa hivi. Binafsi ardhi ninayo ila ningekushauri tuanze mdogo mdogo kama wengi walivyopendekeza. Tuanze na ekari10 kwa kilimo cha umwagiliaji. Mimi shamba lililo karibu na chanzo cha maji ninalo na muda wa kujitolea kukaa shamba upo wa kutosha even over a year.
Nikomee hapa kwanza, utakapojibu post hii tutaendelea na mazungumzo hapahapa ili kila mdau apate wasaa wa kushiriki na kuchangia mawazo.
Mkuu Kisima na wadau wengine ninashukuru kwa kuonyesha support kwenye wazo hili. Mawazo ya wadau wengi naona yamejikita kwenye capital kuwa ni kikwazo...kweli hata mimi nalijua hilo lakini nilipotoa hili.wazo niliona hicho ndicho kianzio kizuri ambacho kama group tunaweza kuanza vizuri hata hivyo niliplan hiyo capital tuichange kidogo kidogo even over a year. Najua kabisa kuwa na hii hela kwa mkupuo kwa wengi wetu ni mtihani, hata kwangu pia.
Heshima yako mkuu Kisima nakukubali sana kaka.Mkuu Revolution nathibitisha uwepo wangu kwenye hili wazo japo mimi si mkazi wa Dar ila nitaomba kupewa updates kama mtapiga hatua ili nijue ushiriki wangu utakuwa wa namna gani
Last edited by a moderator: