Mtaji wa pamoja kwenye mradi wa kilimo- (joint capital)

Mtaji wa pamoja kwenye mradi wa kilimo- (joint capital)

Nina mradi mmoja wa miti ya mbao na nguzo, huu nashirikisha watu kwa kutoa usaidizi kwa anayetaka kuanzia kutafuta shamba,kutafuta mbegu,kuotesha ktk vitalu/kununua miche,kupanda shambani na kutunza. Gharama yako ni kutoa malipo ya kazi sawa ninavyotoa mimi basi.

Mradi wangu wa pili haujakomaa, ni mradi wa shamba kubwa la kuku,hapa sitashirikisha kwa sasa, naendelea na ujenzi wa miundombinu, miaka miwili ijayo nitashirikisha. Mradi wa ranch uko ktk hatua za upembuzi kwa mara ya pili. Mara ya kwanza nilifanikiwa sana kufuga mbuzi,kumbe nilikosea eneo, wateja wa ndani wapo wengi sana, baada ya mimi kuanza kupiga bao, Waswahili wakavamia eneo lote linalonizunguka, nikaanza kuendesha kwa hasara, kila siku kesi, mara matikiti yangu yameliwa na mbuzi wako, mara hivi. Kwa hiyo nimepata maeneo mawili mapya ya kufanyia ufugaji mkubwa kabisa.
Malila, nimependa sana mawazo yenu na wenzako. Nimefunza mengi sana. Binafsi nilianza kilimo from scratch na kwa sasa mambo sio mabaya sana. Nina ekari kadhaa za miti, ila nataka niwekeze zaidi kwenye kilimo cha umwagiliaji. Nitumie PM namba yako tushee mawazo kidogo. Natamani kuwa katika kundi hili.
 
Last edited by a moderator:

Thanks, angalia inbox yako.
 
Wakuu kuna mdau mwenzetu nimemuomba awajoin watu wote walioonyesha utayari naona teknolojia inanipiga chenga kidogo.

Mkuu umefikia wapi na group email? Maana sijapata email yoyote kuonyesha uhai wake
 
Back
Top Bottom