Crystal clear mkuu,napataje details ya miradi uliyonayo kwa sasa ambayo unaruhusu kushirikisha watu?
Nina mradi mmoja wa miti ya mbao na nguzo, huu nashirikisha watu kwa kutoa usaidizi kwa anayetaka kuanzia kutafuta shamba,kutafuta mbegu,kuotesha ktk vitalu/kununua miche,kupanda shambani na kutunza. Gharama yako ni kutoa malipo ya kazi sawa ninavyotoa mimi basi.
Mradi wangu wa pili haujakomaa, ni mradi wa shamba kubwa la kuku,hapa sitashirikisha kwa sasa, naendelea na ujenzi wa miundombinu, miaka miwili ijayo nitashirikisha. Mradi wa ranch uko ktk hatua za upembuzi kwa mara ya pili. Mara ya kwanza nilifanikiwa sana kufuga mbuzi,kumbe nilikosea eneo, wateja wa ndani wapo wengi sana, baada ya mimi kuanza kupiga bao, Waswahili wakavamia eneo lote linalonizunguka, nikaanza kuendesha kwa hasara, kila siku kesi, mara matikiti yangu yameliwa na mbuzi wako, mara hivi. Kwa hiyo nimepata maeneo mawili mapya ya kufanyia ufugaji mkubwa kabisa.