Mtaji wa pamoja kwenye mradi wa kilimo- (joint capital)

Crystal clear mkuu,napataje details ya miradi uliyonayo kwa sasa ambayo unaruhusu kushirikisha watu?

Nina mradi mmoja wa miti ya mbao na nguzo, huu nashirikisha watu kwa kutoa usaidizi kwa anayetaka kuanzia kutafuta shamba,kutafuta mbegu,kuotesha ktk vitalu/kununua miche,kupanda shambani na kutunza. Gharama yako ni kutoa malipo ya kazi sawa ninavyotoa mimi basi.

Mradi wangu wa pili haujakomaa, ni mradi wa shamba kubwa la kuku,hapa sitashirikisha kwa sasa, naendelea na ujenzi wa miundombinu, miaka miwili ijayo nitashirikisha. Mradi wa ranch uko ktk hatua za upembuzi kwa mara ya pili. Mara ya kwanza nilifanikiwa sana kufuga mbuzi,kumbe nilikosea eneo, wateja wa ndani wapo wengi sana, baada ya mimi kuanza kupiga bao, Waswahili wakavamia eneo lote linalonizunguka, nikaanza kuendesha kwa hasara, kila siku kesi, mara matikiti yangu yameliwa na mbuzi wako, mara hivi. Kwa hiyo nimepata maeneo mawili mapya ya kufanyia ufugaji mkubwa kabisa.
 

Mamndenyi ni lisuggest 3000 acres ila sikuwa na maana tunaweza kuzipata kwapamoja au hata tukizipata najua sio rahisi kuzi utilize kwa mara moja itachukua muda na ukizingatia jambo gumu kwenye shamba jipya ni kulivyeka, kuondoa visiki na kulisafisha kisha kulima.
Kisima tupo pamoja pia so far kuna Mamndenyi na wengine ni nani?
 
Last edited by a moderator:
xfactor, pia kunaweza kukawepo na arrangement ya yule mtu ambaye anamajukumu mengine yanayomfanya kushindwa kufika kwenye mradi kuchangia zaidi ya yule ambaye yupo busy zaidi na mradi na mwisho wa siku faida inagawanywa sawa kwa sawa.

Ni wazo tu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa maoni niliyosoma naona watu wana positive minds na hiyo ni nzuri. Mimi ninashauri tupate kwanza wadau halafu tukishakaa pamoja tutajadili mambo ya muhimu ya kuzingatia, namna ya kuanza na ni nini cha kufanya. Msiogopeshwe na hiyo figure ya 10m.

Hivyo so far nimeshawatambua Muungano2, faiza foxy, Kisima, Revolution na mamndenyi. Hivyo tusubiri wadau wengine. Kuna wazo lilitoka kuwa tukiwa wengi inasumbua kutokana na interest tofauti na kukosa commitment, hilo ni kweli ila dhamira yangu ya kusuggest wadau wengi ni kwamba kuna baadhi ya taasisi hasa za serikali ambapo mkijiunga kwenye kikundi mnapata urahisi wa kukopesheka....the more the people ndio urahisi unazidi.
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye redi hata mimi ndo napalilia,
Wakati mwingine inatubidi tuachane na huyu kaisari anavyotunyonya
tuingie huko maporini.

Kuingia hicho kikundi chenu inakuwaje?
 
xfactor, pia kunaweza kukawepo na arrangement ya yule mtu ambaye anamajukumu mengine yanayomfanya kushindwa kufika kwenye mradi kuchangia zaidi ya yule ambaye yupo busy zaidi na mradi na mwisho wa siku faida inagawanywa sawa kwa sawa.

Ni wazo tu.

Anaetoa hela akasubiri faida mwishoni hawezi kua sawa na yule alietoa hela na akashinda shamba. Hii inaweza kutatuliwa kwa yule anaeshinda shamba kupewa mshahara kutokana na capital.

Pili contributed Capital inaweza kua ndio share ya member katika proration basis. Yaani kama mtu umetoa 12Mil katika total 120Mil contributed, basi kwenye faida utapata 12/120 x Net Profit baada ya kutoa mshahara wa yule aliekua akishinda shamba + other costs!
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye redi hata mimi ndo napalilia,
Wakati mwingine inatubidi tuachane na huyu kaisari anavyotunyonya
tuingie huko maporini.

Kuingia hicho kikundi chenu inakuwaje?

hakuna kiingilio,
Kiingilio pekee ni ww kununua shamba lako pamoja na sisi ili kwa pamoja tuweze kuchangia management costs kwa uwiano. Hii imefanya gharama za management zipungue, yaani mtu mmoja anatosha kukagua mashamba ya wadau wote wa block ile na kutoa taarifa kwa group. Mfano mlima wenye eka 300, tumegawana watu kumi kila mtu kwa uwezo wake, fire break tunaweka moja, kitalu kimoja, na kuotesha tunaotesha wakati mmoja, ila kwa uwiano, pia tunajua mipaka ya kila shamba.

Hii imefanya hata wenye hela kidogo kuweza kwenda pamoja kwa kudunduliza kupitia mgongo wa group. Group ina wanafunzi hadi mafisadi, kuanzia mwenye eka mbili mpaka mwenye eka 250 wako pamoja bila taabu. Halafu tuna annual meeting zetu, na communication system ya kwetu wenyewe kama group.

Cha kwanza unatuma mail yako, kisha nakuunganisha na group, na utanunua shamba lako ktk location zenye nafasi kwa kuangalia mapendekezo yako. Ndani ya group kuna wadau wanaingia hatua ya pili, ya kufanya uwekezaji huu uwe rasmi na utambulike na serikali.
 

Well said Gonde Nkaka. Tuanze sasa wakuu. Jambo la msingi ni kukutana kwa wote tutakaokubaliana.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu naona umenisahau japo niliomba kwa heshima,nipo mbali lakini naomba nishirikishwe
 
Last edited by a moderator:
Mkuu naona umenisahau japo niliomba kwa heshima,nipo mbali lakini naomba nishirikishwe

Mkuu@xfactor kuna sehemu nilikutambua labda ni mambo ya tehama yamekorofisha. With all due respect you are in. Labda cha kufanya tu ni kuanza mchakato wa mawasiliano kwa wote tulio interested na huu muunganiko ili ikiwezekana tukutane. Naomba wale wote waliosema wapo interested wanitumie PM.
 

I think anzisha group email au whatsap group for easy and fast communication then from there ndio mipango yote iendelee
 

Nami nitajiunja.

Binafsi tangu mwaka jana nimekuwa na wazo kama hilo na tulianzisha chama cha umoja kwa ajili ya kilimo na ufugaji. Lakini target yetu ilikuwa kupata mkopo wa matrekta na zana nyingine muhimu ili tuanze kilimo. Eneo tayari tulilipata yapata ekari 200 lakini kikwazo kimekua masharti ya mkopo wa zana hizo za kilimo, wanataka 80% mkopo uwe 20%. Tupo njia panda tukisubiria serikali kuweza kutukopesha 50% ya zana hizo.

Nadhani naweza kujiunga na ushirikiano huu upya, kwa hiyo naomba niwemo katika list yako.
 
Last edited by a moderator:
Whatapp account ni nzuri zaidi lakini nafikiri hiyo tuitengeneze tukishawapata wadau wenye dhamira ya kweli katika jambo hili
 
Nimewapata sana wakuu, nimekuwa mkimya purposely nione ni wepi hasa wenye uthubutu na nia ya kweli.
Consider me 100% in na nipo tayali kukaa shamba 24 7 per annum hata zaidi ya miaka mitano mpaka kieleweke.
Kinachofuata upande wangu ni kujua lini tunaianza hii mipango na vipi tunatengeneza capital ya kutosha within short time pasipo ulazima wa kukamuana.
TUPO PAMOJA.
 
sasa kama unacapital hiyo kwann usiwekeze faizafoxy?tena kama ni mimi ningefanya kilimo cha kitaalamu sana,angalaukwa shamba heka 8 lenye maji.

Ndo maana wazee hawatakiwi,,hawekezi sababu hataki purukushani
 
Wakuu kuna mdau mwenzetu nimemuomba awajoin watu wote walioonyesha utayari naona teknolojia inanipiga chenga kidogo.
 
Idea imetulia. Nimekuwa natamani kuwa katika vikundi kama hivi. Inawezekana kuanza na mradi mmoja wa 10mil ambao ndani ya mwaka utawapelekea katika miradi mingine. Mimi ninafanya na wenzangu wawili kwa kufuga samaki. We gan share something
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…