Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony John Mtaka umekuwa ukisifiwa na wengi Kwa kauli imara za kiongozi. Nakufahamu vizuri, wewe ulianza kama Polisi na ukaacha kazi mara ulipopewa nafasi ya kuwa mkimbiza mwenge kitaifa ukiwa Askari mwenye cheo cha Sgt.
Wewe kama Mtumishi wa Umma msomi unajua na wataalamu wa mafao wanafundisha na kuelekezwa kwamba kustaafu kunaanza siku unapoajiriwa. Kwamba Mtumishi anatakiwa kujiandaa kustaafu siku anayoajiriwa. Kustaafu kupo Kwa Aina 2, kustaafu Kwa hiari na kustaafu Kwa lazima.
Kustaafu kutatokea Kwa umri wa lazima au Kwa hiari ya Mtumishi Kwa Muda àmbao hiari hiyo imetajwa na sheria. Lakini kuna mazingira ambayo kinadharia ni Sawa tu na kustaafu maana baada ya matukio hayo Mtumishi anastahili mafao. Mazingira hayo ni;
1. Kifo ukiwa ajirani.
2. Kufukuzwa kazi.
3. Kuacha kazi.
Mazingira yote niliyotaja hapo juu Mtumishi anapaswa kuyajua na kuyatafakari mara tu anapopata ajira.
Sasa inakuwaje Mh Mtaka uwazodoe watumishi wanaoajiriwa na kuanza kujadili madhara ya Kikokotoo? Unataka waanze lini kujadili maslahi yao? Au sheria inataja Muda maalum wa Mtumishi kuanza kujadili mafao yake?
Binafsi naona tabia ya viongozi wa serikali ya CCM kuwaona wengine hawana akili Ila nyie pekee imeanza kukuingia na wewe. Wataalamu toka mifuko ya hifadhi ya Jamii wamekuwa wakitoa semina mbalimbali kuhusu kustaafu na wanasisitiza hili Kwa watumishi kujiandaa kustaafu. Wanasema mwajiriwa yeyote ni mstaafu mtarajiwa, lakini mwenzetu unaanza kuwapangia watumishi namna ya kuwaza na kuendesha maisha Yao.
Nini kimekupata ghafla na ulitegemewa na wengi Kwa nafasi kubwa zaidi ya ukuu wa mkoa?
Ulipotolewa Dodoma kupelekwa Njombe wengi tulishangaa. Mtu mmoja akaandika humu JF "Mnaoshangaa hamumjui Mtaka, ni mbinafsi asiyeamini mawazo ya wengine". Nilimpinga Sana Kwa sababu Mimi nilikuchukulia tofauti. Naanza kuamini alikuwa sahihi. Tabia ya kuzuia watu kujadili yanayowahusu na kuwataka wasubiri maamuzi ya serikali ni unyanyasaji wa Muda mrefu unaofanywa na Viongozi wa serikali.
Acheni Tabia hii ya kudhani unapoteuliwa kuwa kiongozi mahali basi unatawala mpaka uwezo wa watu kufikiri na kupanga maendeleo yao.
UMESIFIWA UNAKIMBIA SANA ANGALIA USIPITILIZE KWENU.