#TANZANIA: UMEANZA KAZI MWAKA HUU UNALALAMIKIA KIKOKOTOO, SASA WEWE UNALALAMIKA NINI? MSUBIRI RAIS WAKO - MKATA
"Kuna watu hapa wameanza kazi mwaka huu na wao wanatukana kuhusu kikokotoo ,anastaafu 2070 anatukana leo kikokotoo, sasa unamuuliza kwani wewe unastaafu lini? Leo ana miaka 22, mwalimu"
"Unakuta mtu ana ajira mpya hata miaka miwili hajafikisha anaanza kulalamikia kikokotoo, sasa wewe unamlalamikia nani? Maana muda wako wa kustaafu utakapofika Rais hatakuwa huyu aliyepo sasa, wewe msubiri Rais wako wa miaka hiyo utakayostaafu ndipo ulalamike" - Antony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
NB; Haya ndo mawazo ya RC maarufu?