Mtakatifu ni nani?

Mtakatifu ni nani?

Kwa maana ya karibu kabisa tunaweza kusema utakatifu ni hali/hatua ya wewe kuweza kukaa katika mapenzi/kanuni/sheria/njia za Mungu
Mwanadamu yoyote aliyezaliwa ni kwa mfano wa Adam na Eva,tunakuwa tayari waovu kwa kuzaliwa Mith 11:21
Sasa kule kufanywa kuwa mtakatifu sio kwa kutangazwa na kanisa au taasisi fulani,ni kusamehewa dhambi zako kunakoambatana na wokovu
Hebu ona mtiririko wa kufikia utakatifu ulivyo;
wokovu>>utakaso>>utakatifu
Wokovu=uwezo wa kushinda dhambi unaopewa kutoka juu
Utakaso=kuwa na moyo safi
Utakatifu=baada ya kutakaswa
Baada ya hatua hizi wewe sasa unakuwa mtakatifu
Ni kweli utakatifu ni hapahapa duniani ndio maana anasema tafuteni kwa bidii........na huo utakatifu ambao ndio tiketi ya kuingia mbinguni Ebr 12:14
 
Asante sana ndugu.!
 
Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo ya dhambi nami nitawapumzisha Mathayo 11: 28-29. Tena biblia inasema Kwa jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu akamtoa mwanae wa pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele( Yohana 3:16) haya maandiko machache yanaweza kujibu unakuwaje mtakatifu kwanza ni kwa kutubu na kumwamini Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako maana biblia inasema katika Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Mstari wa 10 kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki,na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
 
mkuu hii ndo hatua ya kwanza kabisa ya mtu kuanza safari ya utakatifu so ni lazima uokoke kwanza. Yesu anasema mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa baba, ila kwa njia ya mimi (Yohana 14:6) na hapa ndo kuna kitendawili kwa wale wasiomwamini Yesu. Yani kama mtu ana mpango wa kumwona Mungu huyu ndo njia. sitaki kuongelea habari hii naishia hapa
 
Mtakatifu ni nani? ni mtu yeyote aliye okoka na kumwamini Yesu na anaishi sawa sawa na neno la Mungu. Mkuu soma mwenyewe Waefeso 2:1-21
 
Swali la tatu. Je wewe kama GIPAMA waweza kuwa mtakatifu ndiyo. Andiko lako la Zaburi 16: 4 linaonyesha duniani kuna watakatifu. Yesu mwenyewe alikuwa mwanadamu kama sisi maana aliuvaa mwili ili kutuonyesha kuwa inawezekana Yohana 16:33 Hayo nimewaambia mpate kuwa na amani ndani yenu. Ulimwenguni mnayo dhiki, lakini jipeni moyo, mimi nimeushinda ulimwengu. mkuu huu ndo mchango wangu kwa maswali yako
 
mtakatiifu ni mimi kichwa kikubwa, na ili uwe mtakatiifu kama mim, Lazima siku zote uwe mtaka-tiifu na si mtaka-tifu.
Wataka-tifu ni weng sana hapa dunian; ukiwemo na wewe mtoa post.
 
ukisema mtaka tifu kwa kiswahili fasaha ni mtu ambaye anapenda ugomvi.
 
Mtakatifu/ utakatifu/ kitakatifu

Ni kitu/ mtu/ mahali iliyo/aliye/ kilichotengwa kwaajili ya kitu fulani

Unatengwa kwaajili ya kusudi fulani hicho kitaitwa kitakatifu

Hata ambao hawajaokoka wapo baadhi ni watakatifu sababu wamesha tengwa na Mungu sababu ya kusudi fulani

Lakini Mungu huwa hawaachi wafe ktk dhambi wanapata neema ya kukombolewa baadaye

Matendo 9:15
Lakini Bwana akamwambia; Nenda tu; kwa naana huyu ni chombo kiteule kwangu; alichukue Jina langu mbele ya mataifa; na wafalme; na wana wa Israel.

16 Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayo mpasa kuteswa kwaajili ya Jina langu

## umeona hapo juu; sauli aliku chombo kiteule( kitakatifu cha Mungu)
Na huyo alitengwa toka mwanzo

Haikujalisha historia yake ya nyuma kuwa alikua anaua watu wale wafuas wa Kristo lakini bado Mungu alishasema huyu baadaye atakua hivi na hivi

Ndio maana ukisoma mstar 13
Lakini Anania akajibu Bwana; nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi; mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako wa Yerusalemu....

Rudi juu uone Mungu alivyo mjibu( mstr 15)

Kwahiyo mtakatifu au kitakatifu kinakua tayar kimetengwa toka mbinguni kwa Mungu kwa kusud maalumu.

Kwahiyo hata ww unayesoma hapa unaweza kuwa mtakatifu

Nitarudi tena nikipata nafasi
 
Asante sana na ubarikiwe kwa mchango wako mzuri, naomba urudi tena kwa mwangaza zaidi.[emoji120] [emoji120]
 
"Blessed is who has crucified the world, and who has not allowed the world to crucify him. He who has crucified it (the world) is he who has found my Word and has fulfilled it according to the will of him who has sent me".

Kama alivyosema mkuu Mshana Jr utakatifu ni kiroho zaidi na ni ngumu sana kuweka standard. mi naamini watakatifu wapo wengi sana na hata nje ya hizi dini zetu kubwa tunazo amini.
 
Back
Top Bottom