Asante na ubarikiwe. Kwahiyo sasa, mtu anaweza kujiita mtakatifu?
hiyo kujiita mtakatifu mtu anaweza jiita ndio ni kwa sababu ametengwa ktk kusudi fulani.
Sasa anayejiita mtakatifu lazima ajiangalie je na Yeye kaitwa kama Paulo alivyoitwa na Mungu kuwa wewe utakuwa mtu fulani?
Unajua Mungu anaongea na watu kwa njia mbali mbali mfano njia ya ndoto hii ni mara nyingi sema watu hatujui kufasiri ndoto;
Au kwa njia ya sauti kama Musa alivyo itwa kutoka ktk kijiti au paulo huyo huyo alivyo sikia sauti ya Bwana
Matendo 9:3
Hata alipokuwa akisafiri; ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.
4 akaanguka chini; akasikia sauti ikimwambia; Sauli; Sauli; mbona waniudhi?
5 Akasema; U nani wewe; bwana? Naye akasema; Mimi ndimi Yesu unaye niudhi wewe
8 Lakin simaka; uingie mjini; nawe utaambiwa yakupasayo kutenda
## umeona hapo juu Sauli aliitwa kabisa na Mungu kuwa ataambiwa yampasayo kutenda
# Mtakatifu sio lazima awe mtumishi wa madhabahuni; anaweza kuwa hata mtu ambaye haubiri lakin Mungu kamtenga ili afanye jambo kupitia yeye
Na lazima uwe makini na ndoto unazo ota pia Mungu aoengepo na wewe sababu hata shetan anaweza kukudanganya akajivika uungu
Anakupa maelekezo siyo
Halafu ukiamka unaamka na mafunuo ya ajabu
## tuje hiyo mtu anawezaje jiita mtakatifu
Utajiita mtakatifu kwa kujua kabisa mimi nimeambiwa nikae ktk eneo hili na Mungu nifanye kazi hii
Sio leo mwl; kesho nabii; kesho kutwa muumini; mara mchungaji
Hapo hujui umewekwa wapi
Mtakatifu anajua kabisa mimi kazi yangu ni Mlinzi labda nipo maalumu kwa kuombea vijana; au nchi; au familia; yan lazima Mungu akupe sehemu maalum/ kitengo chako na huto yumbishwa na kitu
Tuje huko kujiita mtakatifu; inategemea unajiita kwa madhumuni gana sasa
Sababu unaweza jiita hivyo halafu shetan akapata mwanya wa kukuangusha
Si unajua moyo huwa unajiinua unajiona bora kuliko wengine; hata kama unajijua mtakatifu huna haja ya kujipa cheo mm naitwa mtakatifu Divine... Hapana lazima wakati mwingine hekima itumike sababu
Sababu tunachopigana nacho ni kuwa na mwisho mwema na sio mwanzo mwema
Kuna watu wataanza kukuheshimu wewe badala ya Mungu aliye hai na hicho kitu kibaya sana sababu si wote wenye uelewa unao fanana
Chungu hakiwez pata sifa kuliko mfinyanyanzi mwisho wa siku utafanya mfinyanzi apate hasira akibomoe ili atengeneze kingine kitakacho muheshimu
Kwa kias nikijuacho ni hivyo juu